NECTA 2023: Wanafunzi 359,424 wa Darasa la 4 na Kidato cha Pili wamefeli, Wengine 211,997 hawakufanya Mtihani

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Matokeo ya Mitihani ya Upimaji Kitaifa kwa Wanafunzi wa Darasa la 4 na Kidato cha Pili iliyofanyika Oktoba na Novemba 2023 yameonesha Wanafunzi 147,837 (8.73%) wa Darasa la 4 hawakufanya Mtihani wa Upimaji ambapo Wasichana ni 60,835 (7.04%) na Wavulana ni 87,002 (10.50%).

Pia, Wanafunzi 257,396 sawa na (16.66%) wamefeli kuendelea na Darasa la Tano baada ya kupata Daraja E. Wavulana ni 135,142 (18.22%) na Wasichana ni 122,154 (15.21%).

Aidha, Wanafunzi 64,160 wa Kidato cha Pili sawa na (8.44%) hawakufanya Mtihani ambapo kati yao Wasichana ni 28,951 (7.13%) na Wavulana 35,209 (9.95%).

Waliopata Daraja 0 ni 102,028 sawa na (14.69%) ambapo Wavulana ni 40,498 (12.72%) na Wasichana ni 61,530 (16.34%). Ufaulu kwa Darasa la 4 ni 0.39% na Kidato cha Pili ni 0.62%.




 
Kwenye majibu ya mitihani
Hawaandika miziki ya bongo
Fleva na amapiano singeli
Kweli

Ova
 
Wanafunzi wameendelea kuwa wengi walimu wachache. Shule za kata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…