Ni kastori ka kimiyeyusho ila ngoja nIkaseme. Mimi nimesoma miaka ile ambayo majina yanawekwa wazi ila smartphone zilizokuepo zilikua ni Motorola razr, nokia xpress music, BlackBerry na NEC.
Ili umiliki Blackberry au NEC inabidi uwe mshua. Xpress music na Motorola ilikua hadi tunaosoma Salma Kikwete tunaweza kupambania tukanunua za wizi kwa Hamisi Wanyai.
Am simply saying utake usitake ili uone matokeo ilikua ni uende internet cafe au uende pale ofisi za Halmashauri Magomeni mkasukumane hadi mchane karatasi za majina.
Anyways, majibu ya four yakatoka. Mimi wakati majibu yanatoka nilikua nafanya kazi kama gardener wa hotel fulani hivi so pesa ya kuingia internet cafe ilikuepo. Tukaenda pale Mwananyamala A watatu mshkaji wangu Andrew na Fadhili.
Fadhili alituzidi umri, alikua kaka mkuu wa shule ya Oysterbay, smart sana aisee.
Kufika pale Mwananyamala A mtu nyomi imejaa tukasubiri tukapata nafasi kucheki matokeo mimi ya kwangu ni yale ningeongeza points mbili tu naangukia 4. Andrew matokeo yanamruhusu kwenda private au chuo, Fadhili katembeza miswaki kote.
Akaishiwa nguvu palepale kwenye kiti.
Mmiliki wa Cafe akasema iletwe Fanta, mimi si nina hela za ugardener? Nikafuata Fanta akanywa kidogo akainuka. Tukatoka nje.
Kufika nje akazima. Tukafosi fanta ipite akapata nguvu akakaa kwenye msingi ulikua upo pale. Hiyo saa nne usiku.
Mmiliki wa Cafe akasema nikaongeze maziwa, Fadhili, akamuona demu wake waliyekua wote Obay ila demu alihama shule akaenda private.
Fadhili akatuambia tumshikilie akamsalimie demu wake. Demu namuona yupo excited, ila tukatii takwa la Fadhili, tukiwa tunampeleka akasema "Huyu alikua mjinga kunizidi ngoja nijue alivyofeli iwe msiba wa wengi harusi, kama vipi niende naye ghetto"
Yule she akamuona Fadhili tukiwa tunamkokota na yeye akaanza kuja upande wetu so tukakutana kati. Alivyofika akaanza na neno hili "Hi, what's wrong with Fadhili?" Kichwani nikaona mh huyu mjinga gani huyu? Hajafocus na matokeo yeye kauliza afya ya mtu?
Fadhili akakusanya nguvu kidogo zilizosalia akamuuliza vipi matokeo she akajibu huku anaonyesha kwa vidole kwamba ana division 2.
Fadhili akapiga yowe akaanguka chini akazima, nikakimbia kufuata maziwa. Narudi nakuta kazinduka na binti kampakata kichwa mshkaji. Akagoma kunywa maziwa
Those days bwana. Yaani una uhakika kila anayejua jina lako full ataona jinsi ulivyo mjinga kuanzia juu mpaka chini