NECTA kuwa na mfumo wa kuficha majina ya watahiniwa katika matokeo, ina faida gani?

NECTA kuwa na mfumo wa kuficha majina ya watahiniwa katika matokeo, ina faida gani?

Heri ya Mapinduzi kwa wazanzibari wotee.

Necta hivi karibuni wameamua kutokuweka majina ya wanafunzi katika matokeo.

Pamoja na mambo ya kulinda taarifa binafsi kwa hili hapana.

Kujua ufaulu wa mtu hauishii kama mambo binafsi. Ni jambo la usalama wa taifa.

Hebu fikiria kwa kipindi ambacho wamekuwa wakiweka majina, bado watu wamefanya udanyifu mkubwa.

Hasa wanasiasa na kule ambako Magu mwenyewe aliogopa kupagusa. ( kwenye majeshi)

Kuweka wazi itasaidia kujua mtu yeyote ambaye ni kiingozi wa umma tufahamu ufaulu wake.

Mambo ya kuongozwa na watu wa elimu za hapa na pale, hulipa Taifa changamoto za kiuongozi.

Vinginevyo, tutatanganywa sana kwa kuficha majina kwenye matokeo.

Mbona leo akina Bashite wanasonga tu. Msukuma hana shida anatusua na yupo proud.

Necta acheni kushiriki dhambi za kujenga taifa kijanja jana.

Mbona shule hazisomwi kwa siri? Wote tunajua fulani anasoma shule, tena mnawatambua hadi best stundents. Acheni wazi tuwajua wazushi ktk mitihani.

Kufeli mtihani haina maana hajaelimika, hofu yenu ipo wapi?

Msishinikizwe na wanasiasa kwa manufaa yao.

Wito huu nautoa kwa wote, Nacte pamoja na NECTA. Hata mamlaka nyinginezo, tujenge taifa la uwazi.
Hakuna faida yoyote zaidi ya kuficha siri za familia za mafisadi kina Rostam Aziz
 
Sasa ww wizara imeshikwa na vilaza utegemee nn yaan sehem ya kutoa watu smart viongozi wake ni sifuri bin zero
 
Sasa hapa umeona mtu kaamua kufuatilia zaidi. Sasa ni wangapi wanapigwa. Dogo anamaliza form 4 anakwambia kapiga 1, lakn hachaguliwi form 5.
Ni hivi kama dogo angeongea no angalau awe na D 2 au na C moja wala tusingempigia simu mwalimu.

Maana tunamjua ni kilaza mbaya A zile zilinistua na kunibidi ni hakiki kwa mwalimu wake bila hivyo mzazi ilikuwa imekula kwake
 
Alofanya mtihani ni yeye, wewe matokeo yake yanakuhusu nini??

Wewe unatangaza matokeo ya kila unavhofanya??
 
Alofanya mtihani ni yeye, wewe matokeo yake yanakuhusu nini??

Wewe unatangaza matokeo ya kila unavhofanya??
Taifa lina interest. Kujua hawa watendaji wa baadae tuwatambue uwezo wao.

Wasije kufoji vyeti wakijidai walipasua.

Pia huku mtaani hatutishani sana, tunajua kama wewe zero ni zero, tunakusaidia upande mwingine utoboe.
 
Taifa lina interest. Kujua hawa watendaji wa baadae tuwatambue uwezo wao.

Wasije kufoji vyeti wakijidai walipasua.

Pia huku mtaani hatutishani sana, tunajua kama wewe zero ni zero, tunakusaidia upande mwingine utoboe.
Mzee matokeo ya mitihani ni siri ya mtu na baraza la mitihani.

Hii kitu imefanya madogo wengi kujining'niza, we akili yako imebase kwa viongozi tuuu.

Hao rekebisheni katiba muwe na sehemu ya kuwabana ila sio watu wengine wapate madhara kisa siasa zako.
 
Back
Top Bottom