NECTA Wasalimu amri, mitihan ya kidato cha 4 sasa kurudiwa upya.

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
11,492
Reaction score
5,047
Kutokana na ufahulu mbaya wa wanafunzi wa kidato cha 4 wa mwaka 2012, sasa mitihani hiyo kurudiwa upya na serkali itagharamia gharama zote na hii ni kwa ajili ya kuliepusha taifa aibu ambayo haijawahi tokea nchini kwa anguko la elimu.

Mods naomba msihamishe habari hii wala kunipiga ban, Mimi ni mjumbe tu na mjumbe siku zote hafi.
Mungu ibariki Tanzania.
 


Usemi huo husemwa hivi: "Mjumbe hauwawi" sio mjumbe hafi maana kufa hakutokani na kuuawa tu.

Hata hivyo, matusi hayatumwi. Ukitumwa kumtukana mtu wewe ulietumwa utakuwa ndie ulietukana si aliekutuma!
 
chanzo cha habari?
 
Give the source, otherwise utakula BAN
 
Naunga mkono hoja. Kama ningekuwa napewa nafasi ya kupendekeza, kwa hakika hata mimi ningependekeza iwe hivyo, maana kwa hali hii, 2015, vyuo vikuu na VETA na vyuo vya diploma havitakuwa na wanafunzi. Kwahiyo ni bora tu kurudia mitihani. Wanafunzi watangaziwe ili warudi kwenye vituo vyao kwenda kufanya mtihani mwingine. Kuacha wanafunzi 250000 wapoteleee mtaaani hii si sawa kabisa. Lakini haya yalitakiwa yafanyike kabla ya kutoa matokeo. lilikuwa ni suala tu la kutangaza kwamba matokeo ni mabovu kwa hiyo mtihani unarudiwa.
 
hukumsikiliza vizuri aliyekutuma au na yeye hajui jinsi ya kutoa maelezo?
Siku nyingine ukitumwa, rudia ulichotumwa kwa aliyekutuma ili uone kama ndio hicho na pia uliza maswali ili uelewe vizuri ulichotumwa.

Hapa umekuwa kama sponge liliodumbukizwa kwenywe maji tu.
 
Sijui kama wakirudia watafanya vizuri bila kuwepo maadalizi mazuri na ya muda wa kutosha ya kuwaandaa/kuwafundisha.
 
Tatizo sio kurudia mtihani kwanza ingekuwa vizuri watueleze sababu za kwanini matokeo haya yamekuwa mabaya, maana wanaweza sema paper irudiwe halafu wakawafaulisha wengi huku wakiwa hawana uwezo kama wanavyofanya huko darasa la saba na form 2, hicho kitakuwa kitu cha hatari sana kuliko hata haya matokeo maana tutakuwa na watu wengi wenye vyeti ila wasio kuwa na uwezo, bora ilivyo sasa tunatakiwa tuangalie tufanye nini kuboresha elimu sio tu watu kufaulu sana, ila je wankuwa na uwezo sawa kulingana na kiwango cha elimu?wasituchezee hao watatupa marks nyingi wkt kichwani ni zero wakati wao wanapeleka watoto wao kwenye ichi zenye elimu bora huku kwingine
 
Sijui kama wakirudia watafanya vizuri bila kuwepo maadalizi mazuri na ya muda wa kutosha ya kuwaandaa/kuwafundisha.
Kitakachofanyika ni kulegeza ugumu wa mitihani. Tuta-sacrifice quality for the quantity.
 
hahahaha wanafunzi mliopata ziro na four mna mambo ya ajabu! no wonder why serikali haiwapendi!
 
waliopata zero miaka ya nyuma ya 2012 watawasaidiaje? huu uamuzi ni wa kijuha zaidi ngoja tuone.
 
You said it very well. Tuna hizo kesi za wanafunzi kufika chuo kikuu wakiwa hawajui hata kuandika essay. hilo ni tatizo na tumekuwa nalo hili kwa muda mrefu sana. Ila sasa ndiyo hivyo, inaonekana bado hakujagunduliwa mechanism ya kushughulikia hilo tatizo. Lakini kama pia tutaacha hawa wanafunzi 250000 waingie mitaani bila vyeti, itakuwa ni hatari zaidi, kama hatuwezi kuwarudisha wafanye tena mtihani basi hata tushushe passmarks. Kwa maana ya baadala ya div 4 kuanzia marks 40 ianzie 30 na ziro ianzie 20 au 10, ili angalau wale waliojaribu japo kujibu maswali kadhaa wapandishwe kidogo na kupata vyeti vya kuwapeleka hata kusomea ufundi.
 
Ndugu zangu mnisamehe nimeshau kuweka source, habari hii ipo kwny gazeti la habari leo, pia Kahama fm wametangaza habari hii.
 
Sasa wakirudia hizo maksi za ziada zitatoka wapi!!. Huko sasa kutakuwa ni kudanganyana na kuharibu pesa za walalahoi. Kilichovunwa hakiwezi kupandwa tena. Tujifunze yaliyotokea tugange yajayo. Huko ni kwenda kubadilisha matokeo na wala si kwenda kusahihisha upya!!, tusijindanganye jamani!!. Watabadilisha hayo matokeo lakini akili za hao watoto hazitabadilika. Tutaendelea kula mavi yetu wenyewe. Maamuzi mengine huwa yanatia kinyaa kabia.......
 
Sijui kama wakirudia watafanya vizuri bila kuwepo maadalizi mazuri na ya muda wa kutosha ya kuwaandaa/kuwafundisha.






walikaa shuleni miaka minne hawakufanya vizuri, sasa tangu wamalize ni zaidi ya miezi minne na hawajasoma wala kufundishwa pale ambapo hawakufundishwa watajaza nn sasa? mungu aibariki T
anzania na watu na viongozi wake
 
walekebishe na mishahara ya waalimau,pamoja na mazingira ya kufundishia,lasivyo watakuwa wanacheza malida each year! Chezea mateacheri ww.pamoja pamoja hadi kieleweke!
 
Kama wanafunzi ni walewale.. Walimu ni walewale.. madarasa ni yaleyale.. Serikali ni ileile.. baraza ni lile lile.. tunategemea kweli kupata matokeo tofauti..? Hizi ni hatua za zimamoto hazitasaidia hata kidogo.. Jana kuna member ameweka matokeo ya tokea mwaka 2009 mpaka 2012.. Kilichonishangaza ni kwa watanzania kustuka kwa matokeo ya mwaka 2013 wakati graph ya failure ilikuwa inapanda with an alarming speed..!

2012 Form 4 results

DIV 1: 1,641 (0.4%)
DIV 2: 6,453 (1.6%)
DIV 3: 15,426 (3.9%)
DIV 4: 103,327 (26.0%)
DIV 0: 240,903 (60.1%)

2011 Form 4 results

DIV 1: 3,671 (1.09%)
DIV 2: 8,112 (2.41%)
DIV 3: 21,794 (6.84%)
DIV 4: 146,639 (43.60%)
DIV 0: 156,085 (46.41%)

2010 Form 4 results

DIV 1: 5,363 (1.53%)
DIV 2: 9,944 (2.83%)
DIV 3: 25,107 (7.14%)
DIV 4: 136,777 (38.9%)
DIV 0: 174,407 (49.60%)

2009 Form 4 results


DIV 1: 4,419 (1.78%)
DIV 2: 10,493 (4.21%)
DIV 3: 27,310 (11.2%)
DIV 4: 130,651 (52.61%)
DIV 0: 65,708 (26.46%)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…