Kunawakati ujinga kujifariji nao haipendezi kawaida hata kama muwe wajinga kumi lazima tupate wa mwisho na wa kwanza.Haimaanisha kuwa wa kwanza kwenye kundi la wajinga basi itafuta dhana ya ujinga wako....
Kuniambia kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 7.2% ilihali shule zilizofanya ufaulu upande ni shule za binafsi huu nao ni ujinga.Hatuwezi kujisifia kwa ufaulu kuongezeka ili hali kumi wa mwisho wote ni shule za serikali mbali na hilo hata kwenye kumibora hakuna hata shule moja ya serikali huu ni upuuzi.....
Hivi ziko wapi shule kama azania,kibasila,jangwani,tabora,pugu,kibaha na nyengine ambazo tulizifahamu kama shule za vipaji maalumu zote zimefanana kama shule za kata za kawaida.Hivi unaanzaje kujisifia ufaulu ilihali robo tatu ya shule wamepata ziro tena kwa shule zaidi ya moja na wewe unaenda kujificha ndani ya 7.2%!!!!!?.....
Hivi leo hii msonde kutufanya sisi watoto kuongoza iongoze feza na st fransic ujisifu ufaulu umeongezeka.Hebu kaeni chini angalieni wapi mlikosea elimu haitaki siasa,elimu haitaji vyeti vyako vya master na degree,elimu haitaji uzoefu,elimu inataka welidi na usahihi wa maamuzi yake......
Mmetuletea mitihani ya kushade darasa la saba tangu wakati huo mpaka leo shule za serikali hazina maana tena.Mmekuwa mkiangalia WINGI na siyo UBORA na hapa shule binafsi ndipo zinapo tushinda kila siku.wenzetu hata uwe wa kwanza katika shule yako ya serikali ukifika kwao kujiunga lazima wakupime tena kwa mtihani wao....
Mie najua ukianzia katibu mkuu NECTA na watendaji wengine ndani ya idara ya elimu hakuna hata mmoja anasoma shule ya uma ndiyo maana wala hayawaumi matokeo haya bali anaeumia ni yule mtanzania asiyeweza kutoa mamilioni katika shule zenye ELIMU BORA baadala yake anajikuta anawapeleka katika shule za BORA ELIMU mtoto akue basi....
Kaaeni mtafakari matokeo ya kidato cha nne kwa shule za uma siyo mazuri hata kidogo ila kama mtataka kudanganya toto endeleeni kulinganisha gari na baskeli halafu mseme vyote sawa kwa kuwa vinatumika kama usafiri ila NCHI NI YETU WAJINGA NI WETU HATUMKOMOI MTU BALI TUNAJIUMIZA WENYEWE.....