NECTA yatangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2017. Shule kanda ya Ziwa zang'aa

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 au zaidi kati ya alama 250 wanazopaswa kupata.

Dk Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80 .

Amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76.

Dk Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 70.36, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.40.

Katibu Mtendaji huyo amesema ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati umepanda kwa asilimia kati ya 4.25 na asilimia 10.05 kulinganishwa na mwaka 2016.

"Kwa masomo ya Sayansi na maarifa ya jamii ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 3.56 na asilimia 13.97 kulinganisha na mwaka 2016.

Kati ya wanafunzi 909,950 waliofanya mtihani, ni wanafunzi 22,972 pekee sawa na 2.52% ndiyo waliofaulu kwa daraja A.

"Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambalo ufaulu ni asilimia 86.86 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Kiingereza, lenye ufaulu wa asilimia 40.30," amesema Dk Msonde.

Soma pia matokeo ya kuanzia mwaka 2008
Katibu Mtendaji, Dk Msonde amezitaja shule 10 bora kitaifa kuwa ni;
St Peter iliyopo Kagera, St Severine (Kagera), Alliance (Mwanza), Sir John (Tanga), Palikas (Shinyanga), Mwanga (Kagera), Hazina (Dar es Salaam), St Anne Marie (Dar es Salaam), Rweikiza (Kagera) na Martin Luther (Dodoma).

Amezitaja shule 10 ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni;
Nyahaa ya Singida, Bosha (Tanga), Ntalasha (Tabora), Kishangazi (Tanga), Mntamba (Singida), Ikolo (Singida), Kamwala (Songwe), Kibutuka (Lindi), Mkulumuzi (Tanga) na Kitwai A (Manyara).

Halmashauri kumi bora kitaifa ni;
Kinondoni (Dar es Salaam), Moshi(M) (Kilimanjaro), Arusha(M) (Arusha), Ilala(M) (Dar es Salaam), Mafinga Mji (Iringa), Mlele (Katavi), Kigamboni (Dar es Salaam), Nzega Mji (Tabora), Mpanda (Katavi) na Chato (Geita)

Aliitaja mikoa iliyoongoza kitaifa kuwa ni;
Dar es Salaam, Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, Katavi na Tabora.

Dk Msonde amesema mikoa iliyofanya vibaya ni;
Singida, Tanga, Songwe, Lindi na Manyara.

Wavulana kumi bora kitaifa ni hawa hapa;
  1. Ibrahim Shaban - Tusiime (Dar es Salaam)
  2. Kadidi Mkama Kadidi- Paradise (Geita)
  3. Acius Job Missingo - St. Peter Claver (Kagera)
  4. Mahir Ally Mohamedy - Feza (Dar es Salaam)
  5. Mbarak Faraj - Feza (Dar es Salaam)
  6. Philemon Damas - St. Achileus (Kagera)
  7. Huruma Godfrey - Mwanga (Kagera)
  8. Hamza Azael Almas - Hazina (Dar es Salaam)
  9. Gibbons Roy - Fountain of Joy (Dar es Salaam)
  10. Erastus Joseph - St. Peter Claver (Kagera)
Wasichana kumi bora kitaifa hawa hapa;
  1. Hadija Aziz Ally - Sir John (Tanga)
  2. Naseem Kareem Said - Sir John (Tanga)
  3. Insiyah Kalimuddin Ally - Sir John (Tanga)
  4. Colletha Masungwa - St. Achileus Kiwanuka (Kagera)
  5. Linah John Lameck - Sir John (Tanga)
  6. Saada Ahmed Omary - Sir John (Tanga)
  7. Khadija Salim Omary - Sir John (Tanga)
  8. Hannat Ramadhani - Dar-Ul-Muslimeen (Dodoma)
  9. Efrosina Geofrid - Omukaliro (Kagera)
  10. Nancy Elirehema Mejooli - Tusiime (Dar es Salaam)
Watahiniwa kumi bora kitaifa ndio hawa hapa;
  1. Hadija Aziz Ally - Sir John (Tanga)
  2. Naseem Kareem Said - Sir John (Tanga)
  3. Ibrahim Shaban - Tusiime (Dar es Salaam)
  4. Kadidi Mkama Kadidi- Paradise (Geita)
  5. Acius Job Missingo - St. Peter Claver (Kagera)
  6. Insiyah Kalimuddin Ally - Sir John (Tanga)
  7. Colletha Masungwa - St. Achileus Kiwanuka (Kagera)
  8. Mahir Ally Mohamedy - Feza (Dar es Salaam)
  9. Mbarak Faraj - Feza (Dar es Salaam)
  10. Philemon Damas - St. Achileus (Kagera)

Kwa matokeo zaidi tembelea hapa====>MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA (PSLE) 2017
 
mwenye taarifa kamili kuhusu ufaulu na takwimu atuletee hapa
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Chares Msonde

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba leo Oktoba 20,2017.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 au zaidi kati ya alama 250 wanazopaswa kupata.

Dk Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80 .

http://www.necta.go.tz/matokeo/2017/psle/psle.htm

Amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76.

Dk Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 70.36, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.40.

Katibu Mtendaji huyo amesema ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati umepanda kwa asilimia kati ya 4.25 na asilimia 10.05 kulinganishwa na mwaka 2016.

"Kwa masomo ya Sayansi na maarifa ya jamii ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 3.56 na asilimia 13.97 kulinganisha na mwaka 2016.

"Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambalo ufaulu ni asilimia 86.86 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Kiingereza, lenye ufaulu wa asilimia 40.30," amesema Dk Msonde.

Katibu Mtendaji, Dk Msonde amezitaja shule 10 bora kitaifa kuwa ni St Peter iliyopo Kagera, St Severine (Kagera), Alliance (Mwanza), Sir John (Tanga), Palikas (Shinyanga), Mwanga (Kagera), Hazina (Dar es Salaam), St Anne Marie (Dar es Salaam), Rweikiza (Kagera) na Martin Luther (Dodoma).

Amezitaja shule 10 ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni Nyahaa ya Singida, Bosha (Tanga), Ntalasha (Tabora), Kishangazi (Tanga), Mntamba (Singida), Ikolo (Singida), Kamwala (Songwe), Kibutuka (Lindi), Mkulumuzi (Tanga) na Kitwai A (Manyara).

Aliitaja mikoa iliyoongoza kitaifa kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, na Katavi.

Dk Msonde amesema mikoa iliyofanya vibaya ni Singida, Tanga, Tabora, Songwe, Lindi na Manyara
 
asante mkuu hivi ndivyo inatakiwa
 
Kijana wa jirani amefauru, hongera rais magufuri hizi ni jitihada za chama cha mapinduzi (reply like chakubanga)cc: Joseverest
 
Samahan wakuu kujua kama MTU amefaulu au amefeli unaangalia nini au ni wastani gan unaangaliwa maana me pale naona majina tu na matokeo yao!!!
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Chares Msonde

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba leo Oktoba 20,2017.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 au zaidi kati ya alama 250 wanazopaswa kupata.

Dk Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80 .

http://www.necta.go.tz/matokeo/2017/psle/psle.htm

Amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76.

Dk Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 70.36, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.40.

Katibu Mtendaji huyo amesema ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati umepanda kwa asilimia kati ya 4.25 na asilimia 10.05 kulinganishwa na mwaka 2016.

"Kwa masomo ya Sayansi na maarifa ya jamii ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 3.56 na asilimia 13.97 kulinganisha na mwaka 2016.

"Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambalo ufaulu ni asilimia 86.86 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Kiingereza, lenye ufaulu wa asilimia 40.30," amesema Dk Msonde.

Katibu Mtendaji, Dk Msonde amezitaja shule 10 bora kitaifa kuwa ni St Peter iliyopo Kagera, St Severine (Kagera), Alliance (Mwanza), Sir John (Tanga), Palikas (Shinyanga), Mwanga (Kagera), Hazina (Dar es Salaam), St Anne Marie (Dar es Salaam), Rweikiza (Kagera) na Martin Luther (Dodoma).

Amezitaja shule 10 ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni Nyahaa ya Singida, Bosha (Tanga), Ntalasha (Tabora), Kishangazi (Tanga), Mntamba (Singida), Ikolo (Singida), Kamwala (Songwe), Kibutuka (Lindi), Mkulumuzi (Tanga) na Kitwai A (Manyara).

Aliitaja mikoa iliyoongoza kitaifa kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, na Katavi.

Dk Msonde amesema mikoa iliyofanya vibaya ni Singida, Tanga, Tabora, Songwe, Lindi na Manyara
Mkuu tunaomba na wanafunzi 10 bora kitaifa
 
Zile Shule zetu za Al- Madrasat,Muntazir ,Quiblaten mbona hazipo?
Mwenye jibu jamani atusaidie!
Naombeni jibu mie nijue moja
Wewe huna tofauti na wale watani wangu wanaouwana kikuyu na jaluo....
Siyo vizuri mkuu
 
Back
Top Bottom