NECTA yatikiswa; yacharuka

NECTA yatikiswa; yacharuka

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Taarifa nilizopata hivi punde zinadai kuwa NECTA imeguswa vya kutosha na tuhuma zilizoripotiwa leo kuwa matokeo ya Kidato cha Nne yamechakachuliwa.

Tuhuma hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Sekondari ya Green Acres Ndugu Julian Bujugo. Tangu saa sita mchana wa leo,NECTA imeyapitia tena matokeo hayo.

NECTA imeapa kumburuza Kortini Bwana Bujugo ikithibitika kuwa tuhuma hizo si za kweli.

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar
 
Lisemwalo lipo kama halipo laja.

Chanda chema huvikwa pete.

Kama aliyesema ni mwenye shule,iweje necta waweweseke.

ushauri .necta wajitathimini .
 
Wakuu mbona mtu unaweza uka-appeal unatoa pesa mtihani wako unasahihishwa upya.., (Ila tahadhari...) wakisahihisha upya wanakuwa na hasira kweli kweli unaweza ukawa ulipata II ukajikuta wakirudia unapata IV
 
Hapo ndipo patamu. Ikiwa Mkurugenzi kasema uongo, ajutie uchochezi wake, na kama itathibitika kuwa kasema kweli, basi NECTA iwajibike!!!!!!! Tunaomba haya yasiyeyuke kama upepo unaopita, bali jamii tupate ukweli na uhakika wa jambo hili. Walioathiriwa na matokeo hayo, nao wapewe haki yao kwa kupitia (kusahihisha upya) mitihani hiyo. Naamini, mitihani yao bado iko intact.
 
Uongo wa kwanza huu hapa:

"Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts'.

Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa".

Matokeo yanayoonekana mtandaoni ni:
[TABLE="class: cms_table, width: 70%"]
[TR]
[TD="width: 6%"]S1197/0173[/TD]
[TD="width: 4%"]M[/TD]
[TD="width: 6%"]34[/TD]
[TD="width: 4%"]FLD[/TD]
[TD="width: 58%"]CIV-F HIST-F GEO-F KISW-D ENGL-F LIT ENG-F BIO-F B/MATH-F[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Napata sababu za kutilia mashaka tuhuma za Mwl. Bujugo.
 
Wakuu mbona mtu unaweza uka-appeal unatoa pesa mtihani wako unasahihishwa upya.., (Ila tahadhari...) wakisahihisha upya wanakuwa na hasira kweli kweli unaweza ukawa ulipata II ukajikuta wakirudia unapata IV
Je kama ulikuwa na Div. 0, utapata ngapi?????? Kwa kashfa hii, nashauri NECTA wasahihishe mitihani yote upya kwa gharama zao!!!!!!
 
Mimi nilijua tu huyo Bujugo mwongo! Baraza haliwezi kufanya kosa kubwa kiasi hicho.

Kama mkuu wa shule akili zake ni za hivi, wanafunzi wake watakuwaje? Tusi...kali, ptuuu
 
Safi sana. Nilisema kuwa huyu jamaa kachemka hata matokeo ya wanafunzi wake anashindwa kuyasoma.
 
ujanjaujanja sasa basi. fundisha wanafunzi waelewe siyo kuwanunulia ------.
 
"Ngoma inogile" hakuna ujanja ujanja tena kitaeleweka tu ni baraza au waliokimbilia
kwenye Clouds badala ya Necta
 
Kwanza jina watalipata wap!?
Mimi nilijua tu huyo Bujugo mwongo! Baraza haliwezi kufanya kosa kubwa kiasi hicho.

Kama mkuu wa shule akili zake ni za hivi, wanafunzi wake watakuwaje? Tusi...kali, ptuuu
 
Je kama ulikuwa na Div. 0, utapata ngapi?????? Kwa kashfa hii, nashauri NECTA wasahihishe mitihani yote upya kwa gharama zao!!!!!!

Kwani mwanzo walisahihisha kwa gharama za nani mkuu?
 
Taarifa nilizopata hivi punde zinadai kuwa NECTA imeguswa vya kutosha na tuhuma zilizoripotiwa leo kuwa matokeo ya Kidato cha Nne yamechakachuliwa. Tuhuma hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Sekondari ya Green Acres Ndugu Julian Bujugo. Tangu saa sita mchana wa leo,NECTA imeyapitia tena matokeo hayo. NECTA imeapa kumburuza Kortini Bwana Bujugo ikithibitika kuwa tuhuma hizo si za kweli. VUTA-NKUVUTE wa Lumumba,Dar

Zikiwa za kweli na wao wawe tayari kutangulia mahakamani kwa kudanganya
 
Uongo wa kwanza huu hapa:

"Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts'.

Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa".

Matokeo yanayoonekana mtandaoni ni:
[TABLE="class: cms_table, width: 70%"]
[TR]
[TD="width: 6%"]S1197/0173[/TD]
[TD="width: 4%"]M[/TD]
[TD="width: 6%"]34[/TD]
[TD="width: 4%"]FLD[/TD]
[TD="width: 58%"]CIV-F HIST-F GEO-F KISW-D ENGL-F LIT ENG-F BIO-F B/MATH-F[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Napata sababu za kutilia mashaka tuhuma za Mwl. Bujugo.

Mambo ya kukurupuka wakati mwingine sio mazuri pengine aliambiwa na mke wake :A S shade:
 
Huyu jamaa vipi tena? ila hiyo shule nayo huwa siikubali kabisa.
 
Uongo wa kwanza huu hapa:

"Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts'.

Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa".

Matokeo yanayoonekana mtandaoni ni:
[TABLE="class: cms_table, width: 70%"]
[TR]
[TD="width: 6%"]S1197/0173[/TD]
[TD="width: 4%"]M[/TD]
[TD="width: 6%"]34[/TD]
[TD="width: 4%"]FLD[/TD]
[TD="width: 58%"]CIV-F HIST-F GEO-F KISW-D ENGL-F LIT ENG-F BIO-F B/MATH-F[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Napata sababu za kutilia mashaka tuhuma za Mwl. Bujugo.

Hapo jamaa amecheza na MBOGO aliyejeruhiwa na zero 240,900...

Watamdaka kama mwewe anavyodaka vifaranga...
 
Back
Top Bottom