Elimu kutumika kisiasa ni jambo la hatari sana maana nchi itazalisha vilaza wa bora liende.Kinachonisikitisha zaidi TZ inamalengo ya kuwa Taifa la viwanda sasa unabaki unajiuliza kwa mfumo huu wa elimu hivyo viwanda si vitaongozwa na wageni wenye ujuzi huku wazawa wakibaki manamba?
Serikali kwa kiu yake ya kutaka kuaminika kua ubora wa elimu umekua na ufauru umeongezeka imejikuta ikifuta adhabu ya penati kwa waliopata F somo la hesabu, awali ilikua kwamba mwanafunzi akiwa na cutpoints zinazomruhusu apate aidha div 1 au 2 lakini akapata F ya somo la Hesabu au uraia basi moja kwa moja atapigwa penati na matokeo yake yatakua sio 1 au 2 bali div 3..Umeona sasa wataka sifa walivyo! Ufaulu wa kidato cha nne 2021umeongezeka kwa kiwango cha kutisha huku one na two ikiwa si kitu tena(thaman ya ufaulu kwisha habari yake) maana wapo waliotakiwa kuwa na div 3 yani wana F ya hesabu ila serikali ilipeta kuongeza idadi ya ufaulu.
Hayo si maajabu maajabu zaidi ni kuwa vijana wanaosoma special wale wenye ufaulu mkubwa sana na vijana wanaosoma shule za Kishua kwa mazingira na ufundishaji kama Feza, St Francis, KEMOBOS nk eti wanapimwa kwa mtihani sawa wa Taifa na kijana anayesoma Nyanembe Sekondari ya kata ambayo picha linaanza shule waalimu hawatoshi kuanzia form 1 hadi four mwalimu wa hesabu na fizikia yupo mmoja shule nzima, darasa moja linawanafunzi zaidi ya 100, madarasa hayaleweki umeme hakuna, maji kilomita buku mwanafunzi ambaye lazima atembee zaidi ya KM 5 kutoka anapokaa hadi shule ndo apate elimu, mwanafunzi huyu hana cha library wala huduma ya Internet desa pekee analotegemea atoboe nalo nekta ni kutoka kwa mwalimu shija ambaye naye mda mrefu anashinda Town akipiga madili ya tuition kweli kabisa mnawapima kwa viwango sawa hawa wanafunzi? Hii ni aibu
Ajabu la ziada elimu hii ni huu uhuni wa kupanga matokeo usioleweka lengo tu ionekane ufaulu umeongezeka tuangalie mfano mdogo hapa Shule Ya ANAWARITE GIRLS ina Wanafunzi 76 Na Wote Wamepata Division 1, Alafu Imekua Shule Ya 11 Kitaifa, Wakati Huohuo FEZA BOYS Yenye Wanafunzi 62 Na Inayo Division 1, 2 Hadi 3 Lakini Imekua Shule Ya 7 Kitaifa(Credit Malisa G) .Hapa unajiuliza Wataalamu Walitumia Vigezo Gani Kuzi Rank Hizi Shule? Wamenunuliwa, bahati mbaya au shida ya kimfumo.
Wanasiasa msitumie elimu kujinufaisha mnaua msingi wa Taifa la kesho
View attachment 2092707
View attachment 2092841
View attachment 2092842