NECTA yatoa ufafanuzi kuhusu mjadala wa ufaulu kati ya shule ya Wasichana ya Anwarite na ya Wavulana ya Feza

Kisiasa Malisa GJ anaweza akawa na hoja, lakini kitaalamu NECTA wako sahihi kutegema na namna wanavyokokotoa. Mfano, division one za points 7 zipo zaidi ya mia, lakini bado kuna wa kwanza hadi wa mwisho. Kwa maneno ya Malisa GJ wote walitakiwa wawe wa kwanza sio?
 
Nimepandisha matokeo cheki mwenyewe
 
Hili jambo kuna mahali nimelielezea vizuri.
Nakupa home work.
Chukua wastani wa shule hizo mbili kisha njoo uandike tena Uzi mwingine
 
Nafasi za shule zinapangwa kwa kuzingatia wastani wa jumla, yaani overall GPA sasa ukiangalia GPA ya anwarite ni 1.3409 wakati ua feza boys ni 1.3107

Kwa kifupi tu ni kuwa wastani wa feza ni mkubwa kuliko wa anwarite. Nadhani utakuwa umeelewa
Aelewenini ktk huu utopolo, yaani Anwarite 1.3409 na Feza 1.3107 number ipi ni kubwa hapo ambazo unaziita GPA? mbn hamuoni ht aibu?
 
Tatizo la wanaharakati wetu kupenda kubakia relevant mitandaoni.
 
Mbona hilo swali jepesi mkuu.
Kujua nafasi ya shule wanaangalia wastani wa maksi mwanangu.
Kuna mtu anapata one ya 7
kila somo kapata 100
Chukulia wote wamepata hivyo

Kuna mtu anapata one ya 7
kila somo kapata 81

nadhani umeelewa
 
Kwa hiyo zile seminari za kushinda miaka ile kila kukicha nazo zilikuwa zinapewa michongo....🤔 inawezekana....
Je Tosamaganga, Ilboru, Tabora boyz, ?
Kweli kutesa kwa zamu....
Lakini kwa sasa ukweli ni kwamba wazazi wenye hela ndio watoto wao wanafanya vizuri na huu ukweli ndio upo hata kwa nchi za mabeberu..
Na inawezekana hao wa hizo shule za Div 1 walipasi vizuri kwenda za shule za serikali lakini wazazi pesa ndefu wanawapeleka za kulipia ndio maana matokeo yanajieleza.....
 
Sion sababu ya kujadili minor case kama hizi..
Wote wapate one, two, three nk sion tatzo.
Tatzo linakuja tunaoanza kudai impact ya hizo point kwenye maisha yetu ya kila siku
na ujenzi wa taifa.
 
Imagine one zote za Anuarite ziwe ile ya mwisho kabisa; then wale 59 wa Feza ni wani kali, the best ya pointi ^sir-bar.^ Hapo ni wazi kama mchana wa mwanga kwamba GPA ya Feza lazima iwe kubwa kuliko hao jamaa wa wani zote. (Just trying to be reasonable!)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…