NEEMA KUU: Bwawa la Nyerere kuzalisha umeme wenye thamani sawa na 50% ya makusanyo ya TRA nchi nzima, (Trillion 12 kwa mwaka)

Haitusaidii Mana walisema bei ya umeme hatashuka.
 
So Turbine zilizopo zinauwezo zaidi ya huo, ila MW 2100 ndio working condition?
 
Shule nzuri ila hatuna neno Lissa katika Kiswahili (ukimaanisha muda/wakati).
Saa ni saa tu hakuna wingi. Saa 1,saa3,saa 38,saa 490,nk,nk.
Mfano kutoka Bukoba hadi Dsm ni mwendo wa wastani wa saa 22 kwa basi.
 
Hizo picha zako zitoe zimeharibu uzi huu. Tafuta picha ya MAGUFULI na hilo bwawa uziweke.
 
Huo umeme sio wa wanyonge tena. Ni kwa ajili ya manufaa ya mabepari( kina January & co). Walishatuambia tusitegemee bei kusbuka wala nini. Japo malengo ya JPM ilikuwa kumpunguzia mtanzania gharama kubwa ya umeme.

Wakati wa JPM niliwaza kuwa bwawa lingekamilika tungehitaji sana majiko ya umeme ili tuchemshe na maharage. Mi nilishaweka jiko la umeme standby. Ila ndoto hiyo imekufa.
 
Inaweza karibia huko......
Ila factor moja ya working hrs per day umeisahau ( mashine haziwezi fanya kazi 24/hr).
Lets say ni 12hrs.
Kama hesabu zako zingine zitakuwa sawa means itakuwa Trillion 6 ( 25%).
Ambayo sio mbaya pia.

Je, umeme utakaizalishwa utanunuliwa wote? Maana najua mwingi utapelekwa serikalini ambako hautalipwa na mwingine utaishia kwa vishoka na mwingine utaishia mikononi mwa wanaohonga… zifanye hizi kama external factors za kushindwa kuuza umeme wote!
 
Hayo Maharage uliyotaka kuyachemsha kwa umeme ndio yapo Tanesco sasa, na bei haishuki
 
Hiyo 400 nime-round off kurahisisha maelewano. Pia Sijasema hiyo ni faida au ni net, mimi naongelea kiasi cha pesa ambacho watu hutakiwa kulipa kwa kiwango tajwa cha uniti.
Ww ni mbabaishaji, ulitaka kumsifia kiaina huyo aliyeko hapo kwenye avator yako, lakini kwa bahati mbaya huna akili hiyo, na unaonekana ni mtu uliyefubazwa na propaganda zake.
 
Kimantiki hesabu yako iko sawa, ila kiuhalisia naifananisha na ile biashara ya Matikiti tunayopigiwaga hesabu mitandaoni.
 

Mambo ya kwenye makaratasi yanachosha sana. Tunataka uhalisia wa vitu na siyo maneno. Utaambiwa hivi, ukija kwenye vitendo tofauti kabisa.
 
Yaani unit moja haizidi 50 kuizalisha halafu inauzwa 600, mara 12.
Kweli tozo ni shida

Yes ni parefu nadhani huwa wanafidia pia gharama nyinginezo ikiwemo umeme unaopotea wakati wa usafirishaji...
 
Bosi huwaga unanunua umeme kweli!? Jamaa yupo sahihi ukinunua umeme au LUKU Kuna sehemu hua wanaandika kiasi cha umeme ulichopata kulingana na pesa uliyolipia na huandikwa kwa KWH mfano 43.80KWH kaangalie vizuri tu. Labda upande wa matumizi apo ndo hayuko sawa japo wenyewe TANESCO wamepitia ivo
 
Nna uhakika kwa 200% sisi watanzania hatuwezi kunufaika na mradi huu wa umeme. Nchi hii tuombe Mungu aingilie kati hawa viongozi wote wapite kule waje kizazi kingine kabisa. Bei ya umeme itaendelea kupanda maradufu

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Inaumiza sana, umeme ni mwingi na wa gharama nafuu mno, ila bei hawashushi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…