NEEMA KUU: Bwawa la Nyerere kuzalisha umeme wenye thamani sawa na 50% ya makusanyo ya TRA nchi nzima, (Trillion 12 kwa mwaka)

NEEMA KUU: Bwawa la Nyerere kuzalisha umeme wenye thamani sawa na 50% ya makusanyo ya TRA nchi nzima, (Trillion 12 kwa mwaka)

View attachment 2719361
Umeona hapo 20,000 unapata unit 56

20,000 gawanya 56 ni 357
Ukifanya kabla ya kodi hio 16,000 gawanya 56 ni kama 297

Hizo ndio gharama za umeme za Unit za kawaida kabla na baada ya Vat na Makato mengine.

Hivyo hio figure ya 600 ni Uongo, na mpaka umefikia hio figure kuna possibility kubwa wewe ni tegemezi unatupigia tu kelele humu.

Pia Kwenye Biashara huwezi tumia bei ya mwisho ya mlaji halafu ndio useme ni thamani ya Raw Material.

Leo nikienda Shamba la mpunga halafu nilipigie thamani kwa idadi ya sahani za wali za mama ntilie ni sahihi?
Na hiyo bei ni kwa viwandani.
 
Mkuu umesahau kitu kinaitwa power loss (upotevu wa umeme njiani) wakati wa kuusafirisha kutoka hapo Nyerere dam kwenda Kwa watumiaji.
 
 
Kabla ya yote turudi darasani kidogo, maana sitaki tuanze kuulizana maswali obvious , mara sijui source ni ipi, nk. haya twende kazi.

Unit moja ya umeme hapa Tanganyika inauzwa kwa wastani wa shs. 600/=. Unit moja ya umeme ni kitu wanaita Kilowatthour (KWh). Kilowatthour ni nini hasa? Kilo inamaanisha ‘Maelfu’ (thousands , 000), Watt ni neno linalowakilisha kiwango cha nguvu (power), in this case ni nguvu ya umeme. Sasa hour ni lisaa (dakika 60).

Kwa mantiki hiyo, Unit moja ya umeme (1KWh), ni kipimo cha kiasi cha umeme ambacho kama utautumia kufanya kazi inayohitaji ‘power’ (nguvu) ya watts 1000 , basi unit hiyo itaisha baada ya lisaa limoja (dakika 60).

Haya sasa, tuliza akili halafu twende taretibu. Bwawa la Nyerere linatajwa kuweza kuzalisha Megawatt 2100. Hii inamaanisha nini?

Mega ni neno linalomaanisha millions (000,000), hivyo kwa tafsiri rahisi kabisa, bwawa hili linauwezo wa kuzalisha nguvu (power) ya umeme ya Watts ‘MILLION 2100’ , tukitaka kuiweka kati Kilowatts, tunagawanya hiyo namba kwa ‘1000’ , ambapo tunapata kwamba hilo bwawa linazalisha umeme wenye nguvu ya KILOWatts MILLION 2.1.

Hadi hapo tupo pamoja naamini, maana wewe unaesoma hapa naamini unaakili walau za kuemdea chooni, hivyo lazima hadi hapo umenielewa. Sasa basi , tubadilishe hicho kiwango kuwa ‘Killowatt hour’ (KWh) ambayo ndio unit moja ya umeme sasa.

Mashine za kufua umeme huo wa 2.1 million Kilowatts, zikizalisha umeme kwa muda lisaa limoja, maana yake tumezalisha Unit za umeme zipatazo Million 2.1 , yaani 2.1 million Kwh.

Unit moja ya umeme hapa Tanganyika ni 600/=; sasa kwa unit milioni 2.1, unapata milioni 1,260 ; ambayo ni bilioni 1.26 kwa lisaa. Hivyo basi kwa masaa 24 (siku 1), mitambo inazalisha umeme wenye thamani ya shillingi bilioni 30.24; kwa mwezi ni mara 30 ya hiyo, ambayo tunapata wastani wa Trillion 1 kwa mwezi.

Sasa kwa miezi 12 tunafanya mara 12, hivyo tunapata Trillion 12 kwa mwaka, ambayo ni 50% ya makusanyo yote ya TRA kwa mwaka mzima.

Sasa cha ajabu, huo umeme utauzwa nje, na bado watoto kule kondoa wataendelea kukalia vumbi darasani kwa ukosefu wa fedha za kununulia madawati, huku kesi za ICSD dhidi ya Tanesco wanazojishtaki wenyewe zikiendelea kupamba moto.

Bishana na data (Hoja), usibishane na mimi.

View attachment 2719181


View attachment 2719190

View attachment 2719193

=========================

Hio megawatt 2100 inazalishwa kwa mda gani?Kule juu umesema 1 KWh isije kuwa hio megawatt 2100 ni megawattyear 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Hio megawatt 2100 inazalishwa kwa mda gani?Kule juu umesema 1 KWh isije kuwa hio megawatt 2100 ni megawattyear 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
MW2100 ni rate ya uzalishaji, ukiiwasha kwa sekunde, dakika, au mwaka mzima ni wewe..
 
 
 
Back
Top Bottom