Nehemia Mchechu bila ya ‘speed governor’ ni tatizo. Ndugu zangu wa mitaa ya ‘Al Muntazir’ Upanga mjipange

Mkajenge nyumba zenu, mmekaa hapo miaka na miaka, acha shirika lijiendeshe kibiashara, yaani uko katika nyumba ya ghorofa moja, unazuia zisijengwe ghorofa 20 ili wapangaji wawe maradufu
 
Hebu acha mdomo mdomo, hama humo serikali inataka kufanya maendelezo, unafanya decoration, hiyo nyumba ni yako? Ulipata consent ya land lord? Quic quid......what is attached to the land is part of the land
 
Leo umetema madini
Ukweli haiwezekan nyumba za ajabu ajabu ziwepo upanga....
Kama unataka shiriki mradi au chanika panakuhusu!!!!
 
Huyo mtu wa hali ya chini anaishi upanga, almuntzar ?
Watu wachache weusi wameshika zile nyumba wanawakodishia wahindi kwa bei ghali huku wenyewe wakiilipa NHC hela kiduchu.
Majina ya wapangaji ni wamatumbi ila wanaoishi ni wahindi
Haya mambo yapo pia kota za urafiki sheklango
 
cjui ni mimi cjakuelewa. Umeongelea vitu vingi mpaka cjaelewa point yako ulitaka kusemaje
 
Mleta mada hauko sahihi, nahisi una maslahi binafsi.

Kuweka sawa hili, ngoja niandike machache kufafanua.

1. Hatuwezi kuwapangia nini cha kufanya NHC kwenye nyumba wanazozimiliki. Lolote watakaloliamua ni haki yao, kwa kuwa nyumba ni zao.
Naunga mkono hoja!.
Nauga mkono hoja na hii ndio sheria ya upangaji.
Naunga mkono hoja, na mkataba unakutaka kabla hujafanya maboresho yoyote, you have to inform the land lord for consent in writings, na siku ukihama ni ama uache kila kitu ulichoboresha, ama ubomoe maboresho yako na kuiresha nyumba kama ulivyoikuta!. Ukijiboreshea ni wewe na haulipwi chochote!.
otherwise uwe na mapatano ya kisheria katika hilo na NHC. Na ikiwa sheria/mkataba utakiukwa ni vyema kukimbilia mahakamani kupinga.
Hapa ndipo hii sera mpya ya ubia ilipoingia!
True
True
Naunga mkono hoja.
P
 
Kwamba pakishajengwa hayo majengo ya kisasa, hao wenyeji watapata uwezo wa kukaa hizo prime area na sio wageni tena!? Bila shaka unaota, ukiamka utakutana na reality. Naomba tu usifie usingizini.
Kama tu ghorofa za Magufuli pale usalama wenyeji wameanza kuambiw mara sijui hawaendani na hadhi ya jengo. Mara sijui wanachafua jengo na figisu za aina hio sitoshangaa humo mjini wakiondolewa kibabe bila fidia.
 
Mleta mada,

Nimejaribu kupitia andiko lako kuhusu sera ya ubia ya NHC na nia ya kuwaondoa wakazi ambao kimsingi ni wapangaji kwenye maeneo yote ambayo ni prime na kisha kujenga maghorofa ili kuendana sio tu na mahitaji ya sasa ya mipango miji, bali pia kukidhi mahitaji ya makazi hususani mijini.

Pamoja na umakini wa kusoma andiko lako, bado sijapata kuona logic yoyote ile zaidi ya majungu na kulialia.

Nimeona kwanza unapendekeza wakazi walipwe fidia! Hivi utakuwa unafahamu kwamba kwenye mikataba ya upangishaji, standard lease agreement yoyote ile, kuna kifungu kipo very clear kinachosema Landlord akihitaji nyumba yake kwa matumizi yoyote anayojua yeye, atatoa notisi tu ya mwezi au miezi mitatu na so called "Mpangaji" anafungasha virago?

Just because wapangaji wa NHC wanekaa kwenye hizo nyumba for over 40 years does not make them the owners wa kuwa eligible kulipwa fidia! Hili liondoe kabisa kichwani kwako.

Halafu huu mjadala wako, ukiachana na mambo mwngine yote, umejaa ubinafsi ndani yake. Nitaeleza kwanini, haiwezekani kuwepo na kijengo uchwara mjini ambacho kinaweza ku-accomodate watu 6, mbaya zaidi hata thamani ya ardhi inakuwa imezidi maendelezo yaliyopo juu, halafu bado unataka Shirika liendelee kung'ang'ania hicho kijengo kisa tu England wanafanya hivyo!? Huu ni ubinafsi usio wa kawaida na roho mbaya ndani yake ya kutotaka Wananchi wengi zaidi wasipate fursa ya kuishi mijini!

Faida za kubomoa vijengo uchwara na kutafuta ubia kisha kuendelea kwa kujenga ghorofa nyingi zaidi sio tu kutaongeza mapato kwa Shirika, lakini pia kutafanya maendelezo kuendana na thamani halisi ya ardhi wakati huo huo kuwapata fursa Wananchi wengi zaidi na familia nyingi zaidi kuishi "Downtown".

Hivyo mleta mada nikuombe sana usiwe kizabizabina wa kukataa maendeleo kwa chuki zako binafsi dhidi ya huyo sijui Mchechu. Mimi binafsi I'm not the fun of him, but kwenye hili lazima tumuunge mkono kwa kuwa litaleta faida kubwa kwa Nchi.

It's about time wapenda mserereko wanaojiita wapangaji wa kudumu wa NHC wote waliopo "downtown" na wao wakaishi Madale kwa kupenda au kutokupenda, au kama hawataki basi wapange nyumba kwa developers wengine hapo hapo downtown. Ila ni lazima wapishe NHC ifanye what's necessary.
 
Kama tu ghorofa za Magufuli pale usalama wenyeji wameanza kuambiw mara sijui hawaendani na hadhi ya jengo. Mara sijui wanachafua jengo na figisu za aina hio sitoshangaa humo mjini wakiondolewa kibabe bila fidia.
Wapangaji wafidie kwa sababu gani?
Yaani mpangaji muda wa kukaa umekwisha, mwenye nyumba ameamua kubadili muundo wa nyumba yake na biashara zake, wewe mpangaji uliyekuwa umepangishwa hapo awali uje udai kufidiwa, ufidiwe nini?
 
Mkuu nakuunga mkono kwa hoja zako zote ulizowasilisha hapa. Ni matumaini yetu kwamba itafafanua kwa watu wachache hapa ambao kwa namna moja ama nyingine wamepotoshwa na mleta mada.

Labda kwa kuongezea, mabadiliko ya NHC kutoka kwenye ujamaa na kufanya kazi kibiashara yakifanywa kisheria kwanza kwa Serikali kuondoa sheria ya Rent Restriction Act mwaka 2005 na kuipa uhuru NHC kutoa kodi ya pango kwa kuangalia hali ya soko. Kuanzia hapo NHC ilitakiwa kisheria kufanya kazi kibiashara.

Hivyo utawezaje kufanya kazi kiabishara ukiwa na vijengo uchwara kwenye maeneo ambayo yana command highest rental charges in the country!? Lazima tu ukubali kubadilika kwa kujenga majengo ya kisasa na kama huna mtaji basi unawaalika wabia wenye mitaji ili kufikia lengo.
 
Wapangaji wafidie kwa sababu gani?
Yaani mpangaji muda wa kukaa umekwisha, mwenye nyumba ameamua kubadili muundo wa nyumba yake na biashara zake, wewe mpangaji uliyekuwa umepangishwa hapo awali uje udai kufidiwa, ufidiwe nini?
Si nyumba zao zilivunjwa ili kujenga hayo maghorofa
 
Ipo siku watu kama nyie mtasema polisi iache kuangaika na panya road uswazi kwa hoja za kwamba kwanza ni watoto waliokulia huko huko kwa ivyo ni matatizo ya malezi ya ovyo huko wacha yawakute.

Halafu hayo maeneo yenu nyumba zenu zinawalinzi wa private security companies wenye miguu ya kuku tena mnawalipa kwa mishahara inayotokana na kodi hizo hizo za hao wa uswazi mnaodai panya road ni tatizo la malezi yao sio serikali.

That’s how cheap hoja zako zilivyo

Hakuna serikali makini itakayo kubali aina ya ubia NHC inayotaka kufanya duniani na wala si business model ya shirika lolote la nyumba duniani, na uwezi kuweka mfano wa mtu mwingine yeyote aliefanya icho kitu duniani.

People do regenerations ya maeneo, majengo and sometimes entire cities, nonetheless responsibly.

Ni hivi hilo jambo sio rahisi morally ndio maana hakuna serikali yoyote itakayo support aina hiyo ya ufanyaji biashara labda serikali ya Tanzania tu.

Hakuna shida kubomoa baadhi ya nyumba lakini hekima ni kuwatafutia wapangaji sehemu kwanza, ivyo ndivyo watu wanafanya mambo dunia ya leo ata kama hayo sio matakwa ya sheria za nchi au mkataba; but it’s canon law today unapobomoa nyumba.

Only in 1920’s watu walikuwa wanaweza fanya hayo mambo ila kwa ethics demands.za leo ata hizo central control economies kama China awawezi fanya ivyo; it’s just immoral.
 
Si nyumba zao zilivunjwa ili kujenga hayo maghorofa
Namaanisha wapangaji wa NHC iweje wadai kulipwa fidia baada ya nyumba walizokuwa wamepangishiwa kuvunjwa baada ya mikataba yao kwisha?

Wale wakazi wa Magomeni kota, zile nyumba zilikuwa ni mali yao kwa 100%, walipovunjiwa nyumba zao kisheria, patano lao na serikali ilikuwa kulipwa fidia ya kukaa kwenye yale majengo. Hilo sina tatizo nalo.
 
mkuu ufisadi una sura nyingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…