Tarehe 20 Aprili 1964, akiwa na umri wa miaka 45, akiwa tayari anatumikia kifungo cha miaka 5, kilichoanza 1962, alisimama kizimbani katika kesi iliyojulikana kama kesi ya Rivonia, Mandela alikiri kuwa alikuwa mmoja wa waasisi wa Umkhoto we Sizwe na kuwa alihusika katika juhudi za ku sabotage utawala wa makaburu. Alisema hivyo akijua thika kuwa anaweza kuhumiwa kifo. Lakini aliwaambia makaburu kuwa yote tayari kufa kwa ajili ya imani yake. Akahumiwa kifungo cha maisha. Kwa miaka 18 ya kifungo hicho alipasuwa mawe, alilala kwenye sakafu na alikuwa kwenye selo isiyokuwa na choo. Na kwa muda wote huo hakutetereka katika imani yake. Mwaka 1985 Mandela alikataa ofa ya kuachiwa kutoka jela kwa sharti la kuacha shughuli za ukombozi. Alibaki jela mpaka 1990.
Alipotoka jela alikuta kuna mapambano makali kati ya ANC na Inkatha Freedom Party cha Chief Buthelezi. Mandela akamfanya Buthelezi Waziri wa Mambo ya Ndani. Na alimuachia nchi mara 22 kama acting President.
Ingawa alikuwa na uwezo wa kuendelea kuwa Rais, Mandela alikataa kugombea na mwaka 1999 akaachia urais.
Wakati viongozi wake wenzake wanakataa uwepo wa Ukimwi, Mandela alisema wazi kuwa mwanae alifariki kwa ukimwi!
Kwa kumshutumu Mandela kwa kuwauza watu wake, kunaonyesha wazi msivyoijua historia ya huo uafrika mnaojifanya kuutetea.
Amandla...