Nelson Mandela alihalalisha uporwaji wa Ardhi ya Afrika Kusini kwa Boers halafu anaitwa Baba wa Afrika. Afrika tumerogwa na nani?

Hayo mataifa yana historia tofauti za utawala.

Walowezi wa Kireno waliondoka kwenye makoloni yao baada ya Uhuru ila huko S.Africa na Zimbabwe hali ilikuwa tofauti.
Waliondoka kwa kutaka au kwa kufurushwa?

Vita walivyokuwa wanaendesha kina Mugabe na Mandela vililenga wao kuwaweka madarakani kwa gharama ya Ardhi ya watu wao au?

Hii ndio shida ya kuwa na viongozi wapumbavu na wakabila.. Nyerere aliwazidi akili mbali Sana hao Kwa kujenga utaifa.
 
Sasa mbona Wazimbabwe tangu enzi za Mugabe mpaka leo wanakimbilia na wamefurika bondeni kwa Madiba??
 
Usisahau pia Nyerere ndiye aliyesema kwa katiba hii anaweza kuja Rais akawa dikteta na akatuachia nayo pia kama urithi.
Mwalimu Nyerere ndie Mwanaume kabisa, kabisa.
Amewarithisha watanzania urithi wa Dunia
Bila yeye mwenyewe kujilimbikizia chochote
Ulale kwa amani Nyerere.
 
Nini kiliwazuia wasijikomboe kutoka huko kuuzwa??
 
endeleeni kubisha kuwa Mandela original alifia jela
Wanabisha kwamba ^alifia jela,^ ama wanabisha kwamba ^hakufia jela^? Mbona hii michanganyo haikomi? Shida nini? Au kwa vile gharama za maisha zimepanda kutoka na dai kwamba ^sirikali^ inapambana athari za vita viwili--Ukraine vs Russia & Uviko-19?
 
Walowezi walipoondoka na yote waliyoyaacha yalikufa pia, maana baada ya Uhuru Angola na Msumbiji ziliingia kwenye Vita vya ndani vya wenyewe kwa wenyewe.

Tanganyika ilikuwa haina walowezi wengi wa kizungu kama Kenya, Zimbabwe na Africa Kusini hivyo iliepuka migogoro ya aina hiyo, isitoshe halikuwa koloni kamili la Uingereza.
 
Eti wakitaka ardhi yao waliyoporwa na Wazungu lazima wanunue au walipe fidia kwa wazungu,huu ni wehu 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220712-222155.png
    52.6 KB · Views: 8
Siku ya maridhiano kati ya Makaburu na waafrika weusi, Desmond Tutu alilia sana hakuamini maneno na msimamo wa Nelson mbele ya hadhara Ile...
 
Wataanza kuuza 20 kwa 20, unatujua vizuri kabisa.
 
Mugabe na Mandela wote ni wapumbavu.Angola na Msumbiji kwani wao waliwezaje? Rhodesia ziliwezaje?

Acheni kutetea wapumbavu nyie.
Angalia sasa huko Angola kama kuna jipya lolote? Ni mijamaa kuendekeza ufisadi gharama za maisha zipo juu, na wenyewe wanatamani kuzamia bondeni huko wakatafute maisha.
 
Hizi ndio akili za Malema hizi, wakishamaliza hayo waje waanze kujutia once 1973 Zimbabwe ilikuwa something else nafikiria [emoji1221] wajiangalie vizuri katika ku handle mambo yao.
 
Angalia sasa huko Angola kama kuna jipya lolote? Ni mijamaa kuendekeza ufisadi gharama za maisha zipo juu, na wenyewe wanatamani kuzamia bondeni huko wakatafute maisha.
Siyo kutamani, ni kwamba kuna Waangola wengi sana wamekimbilia kutafuta maisha South Africa.

Tena miaka ile Mandela akiwa Rais mimi nilikuwa nawaona Waangola ni washamba sana kwa kuvaa visuluwali vya kubana na vishati vya kubana, miaka 20 baadaye eti Bongo hiyo ndio fashion ya vijana wanaita model.

Kweli nimeamini hakuna jipya chini ya juwa.

Kwa wale Wazalendo wapenda ardhi tuachane na yasiyotuhusu, tuwanyang'anye ardhi yetu wazungu wanaochimba madini, tuwanyang'anye wageni wote vitalu vya uwindaji, na tupambane na serikali Ngorongoro kwamba binadamu ni bora kuliko wanyama, kama wakitaka waamishe wanyama na siyo binadamu, hapo ndio nitajuwa kumbe Tanzania kuna Wazalendo.
 
Siku ya maridhiano kati ya Makaburu na waafrika weusi, Desmond Tutu alilia sana hakuamini maneno na msimamo wa Nelson mbele ya hadhara Ile...
Acha kudanganya watu, au usikubali kudanganywa kifara.

Mandela amefanya vikao vingi na De clack tangu akiwa jela anachukuliwa kwa siri kwa Hellicopta na kupelekwa ikulu baada ya kikao anarudishwa gerezani Pose moore, achana na Roben Island.

Mandela angeachiwa huru siku nyingi tu ila wapumbavu kama wewe hamjui chochote kwa nini Mandela alikaa jela muda wote huo.

Mjinga anaponyamaza uhesabiwa hekima, tupe ushahidi wa ni wapi na lini Desmond Tutu alilia?

Tueleze huyu Desmond Tutu ni kwa nini yeye ndio aliteuliwa na Mandela kuongoza tume ya Truth and reconciliation commission? Na kwa nini hakukataa? Una uelewa wowote wa neno reconciliation?

Mungu alifanya jambo kubwa sana kuwanyima Watanzania wa kawaida uwezo wa kuandika lugha ya kingereza otherwise mngekuwa sumu sana, kutoka kuwagombanisha Konde boy na Diamond mngefikia mpaka level za kugombanisha nchi nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…