Nembo ya "Kenya Bureau of Halal Certification" ina maana gani katika bidhaa ya kitanzania? Nchi yetu haina hiyo Taasisi?

Msituongeze mizigo ya kulipa kodi. Kwanza hizi bodi na taasisi zimezidi kila kukicha na kodi mpya kuwalipa mishahara yao.
 
Maji hayo yanauzwa Oman na middle east ili kukamata foreign currency, sasa soko linataka walaji walindwe na utaratibu mzima wa uandaaji au uchakataji pamoja na ufungaji wake hayo maji na kusiwe na shaka kwamba ni halal, manake yanastahili kunywea na binadamu.

Manake wengine wanageuza au kusafisha maji ya chooni kuwa maji ya kunywa sasa maji ya namna hii sio halal au alcohol. Wengine wako serious katika vitu wanavyokula na kunywa mbali ya TBS, ISO wanatafuta body zingine ili wafikie soko pana zaidi.
 
Hiyo ni certification inayolenga watu wa mlengo fulani..siyo mandatory but it's for business
 
Sidhani kama kuna Halal Bureau of Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ipo na inatoa mafunzo kwa taasisi kubwa zinazo hudumia vyakula na vinywaji kwenye hotel na ndege au kwenye vyakula vinavyo fungashwa kama kuku, beef, n.k.

Ndugu yangu ameshiriki mafunzo yao mara nyingi tu kwa miaka tofauti.
 
Halaal Certificate Ni Mtaji wa Heoa za Kufadhili Ugaidi.. hauna maana yeyote Ile kwa Secular States.
Una maana kubwa sana kwa International consumers,hayo mambo ya Secular State hayana maana kwa mfanyabiashara aliye serious kwa ajili ya kuwauzia watu maalum. Halal meat kwa mfano kwa Muislam au mtu mwingine anayetaka nyama iliyochinjwa inamfaa,kwani ni ishara kuwa siyo KIBUDU nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msituongeze mizigo ya kulipa kodi. Kwanza hizi bodi na taasisi zimezidi kila kukicha na kodi mpya kuwalipa mishahara yao.
Kwanini kuna kampuni inayolazimishwa kufanya "Halal certification?"
 
Kwa wasioelewa tu ni kwamba hizi nembo za halal zipo katika nchi mbali mbali ulimwenguni na dhumuni lake ni kwa ajili ya kuielezea bidhaa kuwa inatumika na waislam pamoja na wale wanaokula vyakula vinavyoliwa na wote. Je ni halali kivipi? Kuna baadhi ya nchi ukiingia kwenye mall/supermarket/ hotel/restaurant na maduka mbali mbali utakuta wanachanganya bidhaa zote kiasi kwamba kuna vitu wasivyotumia waislam (visivyoliwa na wote) pia vimechanganywa (mfano kitimoto) au hata baadhi ya vyakula hutumika mafuta yake. Hivyo basi nembo hiyo imewekwa kwa ajili ya bidhaa ambazo hazitokamani na hivyo wasivyotumia waislam.

Kuna Hotel/mighahawa pia ukiingia unakutana na neno halal mlangoni, hiyo inamaanisha kuwa humo ndani hawauzi kitimoto/kinachotokana navyo.

Binafsi niliwahi kuingia hotel flani South Africa kama sio kudadisi sana basi ningelishwa kitimoto, ila bahati nzuri pia nilikutana na mhudumu mstaarabu na baada ya kumdadisi akaniambia wao wanauza vyakula lakini sio halal, katika kutaka kujua halal ni nini ndipo nikafahamishwa na kuelekezwa ulipo mghahawa wanaouza halal.

Maana kuna watu washanasibisha halal na kufadhili ugaidi bila kuwa na uhakika nalo swala hilo.

ᴸᵉᵍᵉⁿᵈᵃʳʸ [emoji377]
 
Wakristo no haramu kwao kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu. Hata vikipambwaje ni haramu kuliwa kwa mkristo yeyote labda Kama hakutambua hizo alama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thanks for your contribution
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…