Nembo ya "Kenya Bureau of Halal Certification" ina maana gani katika bidhaa ya kitanzania? Nchi yetu haina hiyo Taasisi?

Nembo ya "Kenya Bureau of Halal Certification" ina maana gani katika bidhaa ya kitanzania? Nchi yetu haina hiyo Taasisi?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu;

Logo ya "KENYA BUREAU OF HALAL CERTIFICATION" ina maana gani katika bidhaa ya kitanzania? Nchi yetu haina hiyo taasisi?

View attachment 1355019

Tazama hilo kopo chini ya QR (Quick Response) Codes
View attachment 1355020

Kenya Bureau of Halal Certification (KBHC) is a Not-for Profit making entity whose aim is to ensure that all products comply with maximum hygienic and humanitarian standards required by Islamic dietary laws. KBHC monitors these products at every point, from the source to the consumer.

This is done by means of thorough inspection and continuous checks by KBHC trained inspectors , thereby eliminating doubts and granting the general public full confidence and assurance when choosing to buy ‘Halal' products.

Consuming Halal is an order from God (Allah SWT) therefore it is important for a consumer to have full confidence that the product he/she intends to buy is ‘Halal' (permissible), ‘Tayyib' (pure) and does not contain anything doubtful. KBHC was born and operates essentially out of one concern only: to be able to provide assurance that what we are consuming is HALAL.

NB: Uislamu ni dini safi kama ulivyo ukristo. Sote kwa pamoja tukemee wanaoeneza chuki za kidini kwa njia mbalimbali kama vile kuchana Quran pamoja na vitabu vingine vitakatifu.

OUR MOTTO: USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Msituongeze mizigo ya kulipa kodi. Kwanza hizi bodi na taasisi zimezidi kila kukicha na kodi mpya kuwalipa mishahara yao.
 
Wabongo bwana kila neno kwao neno
Screenshot_20200212-202446.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maji hayo yanauzwa Oman na middle east ili kukamata foreign currency, sasa soko linataka walaji walindwe na utaratibu mzima wa uandaaji au uchakataji pamoja na ufungaji wake hayo maji na kusiwe na shaka kwamba ni halal, manake yanastahili kunywea na binadamu.

Manake wengine wanageuza au kusafisha maji ya chooni kuwa maji ya kunywa sasa maji ya namna hii sio halal au alcohol. Wengine wako serious katika vitu wanavyokula na kunywa mbali ya TBS, ISO wanatafuta body zingine ili wafikie soko pana zaidi.
 
Hiyo ni certification inayolenga watu wa mlengo fulani..siyo mandatory but it's for business
 
Sidhani kama kuna Halal Bureau of Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ipo na inatoa mafunzo kwa taasisi kubwa zinazo hudumia vyakula na vinywaji kwenye hotel na ndege au kwenye vyakula vinavyo fungashwa kama kuku, beef, n.k.

Ndugu yangu ameshiriki mafunzo yao mara nyingi tu kwa miaka tofauti.
 
Halaal Certificate Ni Mtaji wa Heoa za Kufadhili Ugaidi.. hauna maana yeyote Ile kwa Secular States.
Una maana kubwa sana kwa International consumers,hayo mambo ya Secular State hayana maana kwa mfanyabiashara aliye serious kwa ajili ya kuwauzia watu maalum. Halal meat kwa mfano kwa Muislam au mtu mwingine anayetaka nyama iliyochinjwa inamfaa,kwani ni ishara kuwa siyo KIBUDU nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msituongeze mizigo ya kulipa kodi. Kwanza hizi bodi na taasisi zimezidi kila kukicha na kodi mpya kuwalipa mishahara yao.
Kwanini kuna kampuni inayolazimishwa kufanya "Halal certification?"
 
Kwa wasioelewa tu ni kwamba hizi nembo za halal zipo katika nchi mbali mbali ulimwenguni na dhumuni lake ni kwa ajili ya kuielezea bidhaa kuwa inatumika na waislam pamoja na wale wanaokula vyakula vinavyoliwa na wote. Je ni halali kivipi? Kuna baadhi ya nchi ukiingia kwenye mall/supermarket/ hotel/restaurant na maduka mbali mbali utakuta wanachanganya bidhaa zote kiasi kwamba kuna vitu wasivyotumia waislam (visivyoliwa na wote) pia vimechanganywa (mfano kitimoto) au hata baadhi ya vyakula hutumika mafuta yake. Hivyo basi nembo hiyo imewekwa kwa ajili ya bidhaa ambazo hazitokamani na hivyo wasivyotumia waislam.

Kuna Hotel/mighahawa pia ukiingia unakutana na neno halal mlangoni, hiyo inamaanisha kuwa humo ndani hawauzi kitimoto/kinachotokana navyo.

Binafsi niliwahi kuingia hotel flani South Africa kama sio kudadisi sana basi ningelishwa kitimoto, ila bahati nzuri pia nilikutana na mhudumu mstaarabu na baada ya kumdadisi akaniambia wao wanauza vyakula lakini sio halal, katika kutaka kujua halal ni nini ndipo nikafahamishwa na kuelekezwa ulipo mghahawa wanaouza halal.

Maana kuna watu washanasibisha halal na kufadhili ugaidi bila kuwa na uhakika nalo swala hilo.

ᴸᵉᵍᵉⁿᵈᵃʳʸ [emoji377]
 
Wakristo no haramu kwao kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu. Hata vikipambwaje ni haramu kuliwa kwa mkristo yeyote labda Kama hakutambua hizo alama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wasioelewa tu ni kwamba hizi nembo za halal zipo katika nchi mbali mbali ulimwenguni na dhumuni lake ni kwa ajili ya kuielezea bidhaa kuwa inatumika na waislam pamoja na wale wanaokula vyakula vinavyoliwa na wote. Je ni halali kivipi? Kuna baadhi ya nchi ukiingia kwenye mall/supermarket/ hotel/restaurant na maduka mbali mbali utakuta wanachanganya bidhaa zote kiasi kwamba kuna vitu wasivyotumia waislam (visivyoliwa na wote) pia vimechanganywa (mfano kitimoto) au hata baadhi ya vyakula hutumika mafuta yake. Hivyo basi nembo hiyo imewekwa kwa ajili ya bidhaa ambazo hazitokamani na hivyo wasivyotumia waislam.
Kuna Hotel/mighahawa pia ukiingia unakutana na neno halal mlangoni, hiyo inamaanisha kuwa humo ndani hawauzi kitimoto/kinachotokana navyo.
Binafsi niliwahi kuingia hotel flani South Africa kama sio kudadisi sana basi ningelishwa kitimoto, ila bahati nzuri pia nilikutana na mhudumu mstaarabu na baada ya kumdadisi akaniambia wao wanauza vyakula lakini sio halal, katika kutaka kujua halal ni nini ndipo nikafahamishwa na kuelekezwa ulipo mghahawa wanaouza halal.
Maana kuna watu washanasibisha halal na kufadhili ugaidi bila kuwa na uhakika nalo swala hilo.

ᴸᵉᵍᵉⁿᵈᵃʳʸ [emoji377]
Thanks for your contribution
 
Back
Top Bottom