NEMC: Kunywa bia na kufanya sherehe na matamasha kwenye fukwe ni makosa kisheria

NEMC: Kunywa bia na kufanya sherehe na matamasha kwenye fukwe ni makosa kisheria

NEMC acheni kumchonganisha mama na wananchi wekeni utaratibu wa kuzuia plastic na chupa kwenye fukwe sio kuzuia matamasha
Uchumi hauwezinkukua vila starehe

Tena fukwe ziwe zinasafishwa kila siku ya Jumanne mpaka Alhamisi, ili watu wakienda Wikiendi pawe safi
 
Hao NEMC washamba sana, watu wa vijijini huko kuja mjini na kujidai wanajua kila kitu, kumbe ushamba mtupu.

Watembee duniani waone.
Uingereza kuna Brighton Pier Beach, kusini mwa Uingereza.
Imetengenezwa na kuwekezwa hadi ni kituo cha kuvutia sana na kuingiza pesa nyingi.
Lakini Brighton Beach haifikii robo ya uzuri wa fukwe za Tanzania.

Waende Brazil kuona Capo Cabana na Beach football.
Waende hapa Zanzibar tu na Lamu,Kenya.

Nchi ikianza kuendeshwa na hao washamba wasio na exposure, ni hasara kwa Taifa.
Yaani hii nchi ingepata vichwa 20 kama hiki cha kwako,nchi hii tungekua tumepiga hatua kubwa mno!
 
https://www.nemc.or.tz
NEMC: Mwanzo

MAENEO YA FUKWE AU VYANZO VYA MAJI NI MAENEO NYETI KIMAZINGIRA- Dkt. GWAMAKA


large-1636379548-2.JPG


Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka amesema kuwa maeneo ya fukwe au vyanzo vya maji ni maeneo nyeti kimazingira kwa sababu ni maeneo ambayo yanategemewa na viumbe wa Baharini na Jamii inavitegemea.


Ameyasema hayo alipofanya ziara pamoja na wakaguzi wa mazingira kutoka NEMC katika maeneo ya fukwe za Coco jijini Dar es Salaam. Lengo la ziara hiyo ni kwa ajili ya ukaguzi wa mazingira katika eneo hilo.

Aidha, Dkt. Gwamaka ameeleza kuwa ziara hiyo katika maeneo ya Fukwe za Coco ni kutokana na ujenzi au maendeleo yanayofanyika katika eneo hilo kuangalia kama yamezingatia Sheria ya Mazingira 2004 SHERIA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA YA MWAKA 2004 (NA.20 SHERIA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA YA MWAKA 2004 - [PDF Document] ambayo inasema maendelezo yoyote ambayo ni ya kudumu au ambayo yanaweza kuleta athari zozote za kimazingira basi yafanyiwe Tathmini ya Athari ya Mazingira.

Ameendelea kusema "mazingira ya fukwe za Coco kwa sasa yanaridhisha kutokana na ujenzi wa majengo ya muda yanayovutia yaliyojengwa maeneo hayo ambayo yanatoa nafasi kwa wajasiliamali wenye kipato cha chini kujipatia fedha za kujikimu pamoja na watu kupata sehemu nzuri ya kupumzika na kuweza kula.

Pia nimpongeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na uongozi wake wote kwa jitihada wanazofanya kuwatengea maeneo wajasiliamali wadogo na vilvile kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa utaratibu maalum kama ambavyo ujenzi wa vibanda visivyo vya kudumu unavyoendelea katika fukwe za Coco" .

Dkt. Gwamaka amesema kuwa watashirikiana na Mkuu wa Mkoa pamoja na Manispaa ya Kinondoni ilikuona namna gani wataboresha maeneo hayo ili kukabiliana na changamoto za kimazingira ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa fukwe unaosababishwa na Mabadiliko ya Tabianchi kwa hiyo mahali hapa panatakiwa kufanyiwa maboresho kwa kuweka mawe ambayo yatasaidia maeneo haya yawe endelevu pamoja na kuboresha miundombinu ya maji taka na maegesho ya magari.

Amemaliza kwa kusema kuwa jambo kubwa la kuzingatia maeneo haya ni kuongeza idadi ya vyoo kwani kutokana na muonekano mzuri wa maeneo hayo basi watu wengi watavutiwa kuja hapa.

NEMC tutakuwa bega kwa bega na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha mahali hapa panakuwa salama wakati wote ili eneo hili liwe eneo ambalo wananchi wa kawaida wanaendelea kufaidi matunda ya uhuru wa Nchi, na liwe eneo la mfano kwa wajasiriamali wadogo kwa nchi nzima ya Tanzania

Soma zaidi kutoka chanzo :
Source : Habari | NEMC
Weka hadharani ripoti ya mazingira kuhusu mradi wa kuzalisha umeme pale Selous Game Reserve
 
Mkurugenzi wa Baraza la Kutunza Mazingira NEMC, Dr Samwel Gwamaka asema baraza la mazingira linashauri kuwa si salama kunywa vileo, kufanya matamasha makubwa ktk fukwe za bahari kwani ni hatari kwa umma mpana na pia inapelekea kuharibu mazingira


Source : millard ayo.

Kutengeneza bia je sio kosa kimazingira na kwa umma mpana? I was just wondering about umma mpana and what that consist of
 
Mkurugenzi wa Baraza la Kutunza Mazingira NEMC, Dr Samwel Gwamaka asema baraza la mazingira linashauri kuwa si salama kunywa vileo, kufanya matamasha makubwa ktk fukwe za bahari kwani ni hatari kwa umma mpana na pia inapelekea kuharibu mazingira


Source : millard ayo.

Ukiwatazama usoni utadhani wanamaanisha wanachokisema, ukiwafuatilia kwa nyuma utakuta na wao wanayafanya, isitoshe wamehamia baharini huku kelele za miziki mitaani zimewashinda
 
Rio De Janeiro, Brazil

COPACABANA

Copacabana Beach & Boardwalk 🇧🇷 | Rio de Janeiro, Brazil |【4K】2021


Copacabana Beach is the most famous beach in Brazil. This video brings the best of a series of other videos from the channel about Copacabana Beach and the Copacabana boardwalk (calçadão) that were recorded between 2019 and 2021.



Source : Vort-V Ambience

Ninachokiona ni kwamba magari hayaegeshwi kwenye ufukwe. Hayaruhusiwi. Sababu zinaweza kuwa mbili. Kwanza, kuepusha beach erosion. Yanayoendelea hapo coco beach ni tofauti, magari yanaegeshwa karibu sana na kingo zake. Wanamazingira wananaweza kutusaidia kupata ufumbuzi. AU waturejeshe kwenye maamuzi yaliyofanyika wakati marehemu Kenja akiwa kiongozi wa jiji. Pili, kuwezesha watembea kwa miguu kuwa huru wawapo kwenye fukwe. Naamini hatua kama hizo zitasaidia zaidi katika kulinda mazingira ya fukwe na usalama wa wataotembelea fukwe hizo.
 
Sheria ya kiboya sana. Badala ya kutumia muda wao kuhakikisha kuna madampo ya kutosha ya taka taka mnahangaika na wanywa bia tamu ufukweni daaah...
 
Nimekumbuka beach zangu mbuli mojawapo ni ya nchi jirani Fernao Verosso prayol
 
Ukitaka kushusha thamani ya fukwe weka hizo sheria za uone.

Kwaiyo beach sahv ni sehemu za ibada?
 
Rio De Janeiro, Brazil

COPACABANA

Copacabana Beach & Boardwalk 🇧🇷 | Rio de Janeiro, Brazil |【4K】2021


Copacabana Beach is the most famous beach in Brazil. This video brings the best of a series of other videos from the channel about Copacabana Beach and the Copacabana boardwalk (calçadão) that were recorded between 2019 and 2021.



Source : Vort-V Ambience

Na hivyo unavyowaona na vinguo vyao, wanapanda hivyo hivyo kwenye basi kutoka wanapoishi mpaka huko beach.

Mimi mshamba wa kijijini nilishangaa na kutoa macho hasaaa!
 
Ninachokiona NEMC ni kujitanua mabega na kujiona wana mkono mpana.
Sheria ya Mazingira inawapa mamlaka wao kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa kutengeneza miongozo ya kuhifadhi maeneo ya pwani au yenye vyanzo vya maji.
 
Weka hadharani ripoti ya mazingira kuhusu mradi wa kuzalisha umeme pale Selous Game Reserve
Wamiliki wa ripoti ya Mazingira ya Selous ni TANESCO siyo NEMC. TANESCO ndiyo wenye mradi na ndiyo wenye haki ya kusema iwekwe hadharani au la.
 
Huu ni uthibitisho tosha kuwa Nchii hii inaongozwa na Washamba.

Mimi nimejirusha sana Mombasa Pirate Beach kwa Vinywaji mbalimbali.

Tanzania inaangamizwa na Washamba wenye mrengo wa Kikomunisti.
 
Arrogan
Wamiliki wa ripoti ya Mazingira ya Selous ni TANESCO siyo NEMC. TANESCO ndiyo wenye mradi na ndiyo wenye haki ya kusema iwekwe hadharani au la.
I do understood you na sikulaumu kwa hilo haya ndio matokeo ya ccm kuharibu mfumo wa kielimu na tunaishia kupata middle class kama wewe,yes mradi kama ni wa TANESCO,kisheria ilitakiwa wapeleke kwanza ripoti yao kuhusu athari ya mazingira kwa mradi huu na pia hawa watu wa mazingira ilitakiwa nao wajiridhishe kuwa mazingira yataathiriwa vipi na ripoti hizi sio siri na public wana haki ya kujua;
 
Back
Top Bottom