NEMC yazifungia Bar, Kumbi za Starehe 89 zikiwemo Wavuvi Kempu, Boardroom, Ware House

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Samuel Gwamaka amesema jumla ya baa na kumbi za starehe 89 zimefungiwa baada ya kubaini kupiga kelele na mitetemo iliyozidi viwango vinavyotakiwa.

Dkt. Gwamaka amesema baa na kumbi hizo za starehe zimebainika katika operesheni iliyofanyika ndani ya wiki moja katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.

Ameeleza hayo leo Jumatatu, Mei 8, 2023 wakati akitoa mrejesho wa msako walioufanya kati ya NEMC na jeshi la polisi kubaini baa na kumbi za starehe zinazopiga muziki kwa sauti ya juu ambayo ni kinyume cha sheria ya mazingira ya mwaka 2014.

"Tumebaini na kufunga baa na kumbi za starehe 19 za Kinondoni, 25 Ilala, Kigamboni 22 na Temeke 12, jijini Dodoma ni tano na Mwanza ni sita. Maeneo haya tulioyafunga ni sugu na haikuwa mara kwanza kuwaonya hawa tuliowafungia,” amesema

Huku akiongeza kusema, "Huko nyuma tulishawaonya na kuwaadhibu kwa kuwapiga faini, lakini waliendelea kukaidi, miongoni baa sugu ni Bodroom, Wavuvi Camp, Wherehouse, Avoco, Kitambaa Cheupe.Wengine ni Element, Chako ni Chako, Rainbow Gentlemen, Liquid na Soweto."

Kwa mujibu wa bosi huyo wa NEMC, wamefikia uamuzi wa kuwafungia kwa sababu sio mara kwanza kwa baa na kumbi hizo kufanya makosa hayo, licha ya NEMC kuwaonya kwa nyakati tofauti.

Amesema baada ya kuwafungia baadhi ya wamiliki wa baa na kumbi wamefika ofisi za NEMC kuomba msamaha.

MWANANCHI
Nampongeza Mkurugenzi.Hawa watu hawajali Wala hawaambiliki. Kuna baa inaitwa kwa mkinga hapa ukonga Mazizini wanatusumbua sana.
 
Muda huu nimetoka las carinyo pamekuwa pa baridi utafikiri walevi (wanywaji) wanaomboleza msiba. Nimeenda Uhuru Peak wamezungushia mabati nadhani wanakarabati, nimeenda Masai pamepoa sana.
nimeenda twitter muziki mdogo sana hata DJ hayupo.
Hapa nipo njiani naenda kulala kwenye stoo yangu.
 
Hata me huangalia mpira las cainyo kama wamepachinja basi wapuuzi...
 
Wameanza na bar, itafuata kupiga marufuku Kitimoto .

Chukulia kila bar ina wafanyakazi si chini ya 20 na bar zaidi ya 89 zimefungiwa.
Inamaana watu zadi ya 1,780 ajira. Zao zimesitishwa.

OKTOBA 2025 SIYO MBALI!
 
Bar hazijafungwa, wamefungiwa kupiga muziki, fungua na uza kimya kimya, Kwakweli ni KERO sana.

Wasiishie kwenye BAR, washuke kwenye MAKANISA maana wanapiga muziki usiku kucha, hawapumziki, na hata mchana na kero.
 
Na huku kawe wasitusahau....Kuna baa mpya IPO eneo la jeshi karibu na makazi ya watu....inapiga mziki usiku kucha hasa wikiendi...Ila waende kwa ustaarabu maana wazee wa kazi wanakuwepo pale.
Wazee wa kazi ndio kina Nani?
 
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Samuel Gwamaka amesema jumla ya baa na kumbi za starehe 89 zimefungiwa baada ya kubaini kupiga kelele na mitetemo iliyozidi viwango vinavyotakiwa.

Dkt. Gwamaka amesema baa na kumbi hizo za starehe zimebainika katika operesheni iliyofanyika ndani ya wiki moja katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.

Ameeleza hayo leo Jumatatu, Mei 8, 2023 wakati akitoa mrejesho wa msako walioufanya kati ya NEMC na jeshi la polisi kubaini baa na kumbi za starehe zinazopiga muziki kwa sauti ya juu ambayo ni kinyume cha sheria ya mazingira ya mwaka 2014.

"Tumebaini na kufunga baa na kumbi za starehe 19 za Kinondoni, 25 Ilala, Kigamboni 22 na Temeke 12, jijini Dodoma ni tano na Mwanza ni sita. Maeneo haya tulioyafunga ni sugu na haikuwa mara kwanza kuwaonya hawa tuliowafungia,” amesema

Huku akiongeza kusema, "Huko nyuma tulishawaonya na kuwaadhibu kwa kuwapiga faini, lakini waliendelea kukaidi, miongoni baa sugu ni Bodroom, Wavuvi Camp, Wherehouse, Avoco, Kitambaa Cheupe.Wengine ni Element, Chako ni Chako, Rainbow Gentlemen, Liquid na Soweto."

Kwa mujibu wa bosi huyo wa NEMC, wamefikia uamuzi wa kuwafungia kwa sababu sio mara kwanza kwa baa na kumbi hizo kufanya makosa hayo, licha ya NEMC kuwaonya kwa nyakati tofauti.

Amesema baada ya kuwafungia baadhi ya wamiliki wa baa na kumbi wamefika ofisi za NEMC kuomba msamaha.

MWANANCHI
Ukiwa na viongozi wa TAASISI wasio na mindset za biashara haya ndo madhara kama tatizo ni kelele za muziki wawafungie muziki nankuwapiga faini huku huduma zingine za vinywaji chakula na Ngonobziendelee. Kwankuwafungia serikali imekosankodi, Kuna wafanyakzi wengi hii chain ukiikata gafla ni shida.... Hili lakufunga ni solution na muda mfupi TU
 
Hivi wamefungiwa au wamepiga marufuku miziki? Sijaelewa
 
WASIPOFUNGIA MISIKITI NA VILE VIPAZA SAUTI VYAO ALFAJIRI, HILI ZOEZI NI BATILI
 
TTG sijaiona hii bar isipofungiwa nitashangaa. Inapiga sana kelele.
 
Wanatusumbua sisi matajiri hatuwezi kuiala kwa amani. Fungia hizo takataka
 
Matokeo ya malumbano ya hoja i t v wiki iliopita watajua hawajui tutafungua miziki ya magari cjui fine watapiga toyota au mwenye gari
 
Back
Top Bottom