Hassan Mambosasa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2014
- 3,359
- 4,528
Huu ndiyo ukweli na hii si mara ya kwanza na hata hiyo sauti yenyewe kule hawatumii kubwa hivyoKwa wavuvi camp jamaa hawajatenda haki kule kuna makazi ya watu ..? Hapa wanamwandama tu yule mzungu s bure
Nampongeza Mkurugenzi.Hawa watu hawajali Wala hawaambiliki. Kuna baa inaitwa kwa mkinga hapa ukonga Mazizini wanatusumbua sana.Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Samuel Gwamaka amesema jumla ya baa na kumbi za starehe 89 zimefungiwa baada ya kubaini kupiga kelele na mitetemo iliyozidi viwango vinavyotakiwa.
Dkt. Gwamaka amesema baa na kumbi hizo za starehe zimebainika katika operesheni iliyofanyika ndani ya wiki moja katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.
Ameeleza hayo leo Jumatatu, Mei 8, 2023 wakati akitoa mrejesho wa msako walioufanya kati ya NEMC na jeshi la polisi kubaini baa na kumbi za starehe zinazopiga muziki kwa sauti ya juu ambayo ni kinyume cha sheria ya mazingira ya mwaka 2014.
"Tumebaini na kufunga baa na kumbi za starehe 19 za Kinondoni, 25 Ilala, Kigamboni 22 na Temeke 12, jijini Dodoma ni tano na Mwanza ni sita. Maeneo haya tulioyafunga ni sugu na haikuwa mara kwanza kuwaonya hawa tuliowafungia,” amesema
Huku akiongeza kusema, "Huko nyuma tulishawaonya na kuwaadhibu kwa kuwapiga faini, lakini waliendelea kukaidi, miongoni baa sugu ni Bodroom, Wavuvi Camp, Wherehouse, Avoco, Kitambaa Cheupe.Wengine ni Element, Chako ni Chako, Rainbow Gentlemen, Liquid na Soweto."
Kwa mujibu wa bosi huyo wa NEMC, wamefikia uamuzi wa kuwafungia kwa sababu sio mara kwanza kwa baa na kumbi hizo kufanya makosa hayo, licha ya NEMC kuwaonya kwa nyakati tofauti.
Amesema baada ya kuwafungia baadhi ya wamiliki wa baa na kumbi wamefika ofisi za NEMC kuomba msamaha.
MWANANCHI
Hata me huangalia mpira las cainyo kama wamepachinja basi wapuuzi...Muda huu nimetoka las carinyo pamekuwa pa baridi utafikiri walevi (wanywaji) wanaomboleza msiba. Nimeenda Uhuru Peak wamezungushia mabati nadhani wanakarabati, nimeenda Masai pamepoa sana.
nimeenda twitter muziki mdogo sana hata DJ hayupo.
Hapa nipo njiani naenda kulala kwenye stoo yangu.
😂😂😂😂 Yan we unawAza kuzagamua tu daaaah 😂😂😂😂Sema uzuri wakishazifungia bei elekezi huwa inashuka pia
[emoji23][emoji23]Huku utanunua kesi.
Adhana ni dk 1.30 tu ......Hazizidi dakika 5 pia ni saa nzuri utuamsha mapema kuwahi usafiri
Bar hazijafungwa, wamefungiwa kupiga muziki, fungua na uza kimya kimya, Kwakweli ni KERO sana.Wameanza na bar, itafuata kupiga marufuku Kitimoto .
Chukulia kila bar ina wafanyakazi si chini ya 20 na bar zaidi ya 89 zimefungiwa.
Inamaana watu zadi ya 1,780 ajira. Zao zimesitishwa.
OKTOBA 2025 SIYO MBALI!
Wazee wa kazi ndio kina Nani?Na huku kawe wasitusahau....Kuna baa mpya IPO eneo la jeshi karibu na makazi ya watu....inapiga mziki usiku kucha hasa wikiendi...Ila waende kwa ustaarabu maana wazee wa kazi wanakuwepo pale.
Ukiwa na viongozi wa TAASISI wasio na mindset za biashara haya ndo madhara kama tatizo ni kelele za muziki wawafungie muziki nankuwapiga faini huku huduma zingine za vinywaji chakula na Ngonobziendelee. Kwankuwafungia serikali imekosankodi, Kuna wafanyakzi wengi hii chain ukiikata gafla ni shida.... Hili lakufunga ni solution na muda mfupi TUMkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Samuel Gwamaka amesema jumla ya baa na kumbi za starehe 89 zimefungiwa baada ya kubaini kupiga kelele na mitetemo iliyozidi viwango vinavyotakiwa.
Dkt. Gwamaka amesema baa na kumbi hizo za starehe zimebainika katika operesheni iliyofanyika ndani ya wiki moja katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.
Ameeleza hayo leo Jumatatu, Mei 8, 2023 wakati akitoa mrejesho wa msako walioufanya kati ya NEMC na jeshi la polisi kubaini baa na kumbi za starehe zinazopiga muziki kwa sauti ya juu ambayo ni kinyume cha sheria ya mazingira ya mwaka 2014.
"Tumebaini na kufunga baa na kumbi za starehe 19 za Kinondoni, 25 Ilala, Kigamboni 22 na Temeke 12, jijini Dodoma ni tano na Mwanza ni sita. Maeneo haya tulioyafunga ni sugu na haikuwa mara kwanza kuwaonya hawa tuliowafungia,” amesema
Huku akiongeza kusema, "Huko nyuma tulishawaonya na kuwaadhibu kwa kuwapiga faini, lakini waliendelea kukaidi, miongoni baa sugu ni Bodroom, Wavuvi Camp, Wherehouse, Avoco, Kitambaa Cheupe.Wengine ni Element, Chako ni Chako, Rainbow Gentlemen, Liquid na Soweto."
Kwa mujibu wa bosi huyo wa NEMC, wamefikia uamuzi wa kuwafungia kwa sababu sio mara kwanza kwa baa na kumbi hizo kufanya makosa hayo, licha ya NEMC kuwaonya kwa nyakati tofauti.
Amesema baada ya kuwafungia baadhi ya wamiliki wa baa na kumbi wamefika ofisi za NEMC kuomba msamaha.
MWANANCHI
... kauchochoro muhimu sana hako!Hapo mwishoni mwa taarifa naona kuna nafasi ya mazungumzo na kusamehewa
... wanasema haizidi 5 min. hivyo ni himilivu!WASIPOFUNGIA MISIKITI NA VILE VIPAZA SAUTI VYAO ALFAJIRI, HILI ZOEZI NI BATILI