Nenda Sabaya lakini bila wewe haya yasingewezekana kutokea wilaya ya Hai

Nenda Sabaya lakini bila wewe haya yasingewezekana kutokea wilaya ya Hai

Kinuju

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2021
Posts
2,386
Reaction score
5,325
Ni kweli chadema na wapinzani wengi wameshangilia sana kifungo cha Lengai Ole Sabaya cha miaka 30 jela lakini ukweli ambao hausemwi ni kwamba wana CCM wengi wamehuzunishwa na kuchukizwa mno na kifungo cha Sabaya.

Kwenye macho ya wazalendo wa nchi hii, Sabaya ni mzalendo wa kweli aliyejitoa kuleta mabadiliko kwa vitendo na siyo maneno kama wanavyofanya wengi.

Bila Lengai Ole Sabaya kuwa mkuu wa wilaya ya Hai haya yangeweza kutokea kwenye wilaya hii.

1. Wilaya ya Hai kupanda kwa ukusanyaji mapato kutoka ya mwisho hadi kuwa ya nne kitaifa
.
Kabla ya Sabaya wilaya hii ilikuwa imekithiri kwa rushwa, ukwepaji kodi na ufyatuaji wa fedha bandia. Leo fedha bandia zimeadimika nchini sababu ya wewe Sabaya kukamata mnyororo wote wa wafanyabiashara waliokuwa na mitambo ya kutengeneza pesa bandia.

2. Mbunge na madiwani wa CCM kushinda na kuongoza Halmashauri
Wilaya hii ilikuwa ngome ya Chadema kwa miaka mingi na kila aliyejaribu alikiona cha mtema kuni kutoka kwa Mbowe na genge lake.
Lakini kupitia Sabaya sasa jimbo la Hai ni ngome ya CCM na itawachukua miaka mingi Chadema kulirudisha tena hasa baada ya Mbowe kupoteza imani kwa wananchi wengi. Lakini pia Mbowe ametangaza kuachana na siasa za majukwaani.

Kwa kifupi mbunge ,madiwani na wenyeviti mbalimbali wa wilaya ya Hai wanakula kupitia jasho la Sabaya.

3. Kurejeshwa kwa ardhi ya waislamu iliyoporwa kwa miaka mingi
Wilaya ya Hai wamepita wakuu wa wilaya wengi lakini hakuna aliyefanikiwa kumaliza mgogoro huo mpaka Lengai Ole Sabaya alipofika na kumaliza kadhia hiyo.

NB: Sabaya ni mfungwa wa kisiasa na wafungwa wa kisiasa huwa hawamalizi vifungo vyao, hata asipotolewa na rais Samia atakuja rais mwingine atamtoa na kumpa cheo.
 
Yooote hayo yalifanyika kwa dhuluma na kuumiza watu.Kuwaumiza nafsi na miili yao.

Hayakufanyika ktk namna iliyo HAKI. Acheni kumpamba na kumvika kuwa innocent huyu mtu, tena ukiondoa kufungwa, ana adhabu ingine mbele ya mwenyezi Mungu kwa damu aliyomwaga.

Hivi umeiona ile crip ya yule bibi akimwomba mungwake kisa huyo jambazi? Angalieni ninyi vijana,njaa zisiwaondolee utu na ubinadamu
 
E4F18907-D0EF-492D-BA61-727259161AE7.jpeg


36373F3B-330E-4E26-8122-A8A114F6E54D.jpeg
 
Yooote hayo yalifanyika kwa dhuluma na kuumiza watu.Kuwaumiza nafsi na miili yao.

Hayakufanyika ktk namna iliyo HAKI.Acheni kumpamba na kumvika kuwa innocent huyu mtu,tena ukiondoa kufungwa,ana adhabu ingine mbele ya mwenyezi Mungu kwa damu aliyomwaga.

Hivi umeiona ile crip ya yule bibi akimwomba mungwake kisa huyo jambazi? Angalieni ninyi vijana,njaa zisiwaondolee utu na ubinadamu
Na kwa taarifa zilizopo, ndiye aliyefanikisha mauji ya komandoo wetu Lijenje.
 
Nani akiagiza Sabaya akamatwe na achunguzwe na hatimaye kufikishwa mahakamani?

Kwahiyo mapato, kupanda, ardhi ya waislamu kurudishwa ilikuwa ni kibali cha yy kufanya uhalifu kwa kuongoza genge lenye silaha, kupora mali za watu, kunyanganya fedha, nk

Kichwa maji wwe hujui hata unachotetea. Pumbavu!
 
Back
Top Bottom