Neno "DEAR" linatumika vibaya au ni Ushamba wangu

Neno "DEAR" linatumika vibaya au ni Ushamba wangu

Kwa miaka ya hivi karibuni matumizi ya neno dear yameongezeka sana, zamani ukimuita mtu dear maana yake kuna mapenzi kati yenu
Siku hizi dear linatumika kwa mtu yoyote yule hasa sisi wadada tunaitana sana hivyo.
Cha kushangaza sasa...Unaweza ukawa unawasiliana na mtu/mdada ambae hamfahamiani hata sura, inaweza ikawa kibiashara au kwa sababu nyingine, anakwambia okay dear, yaani dear dear za kutosha. Hili huwa linanishangaza yaani iweje huyu mtu hanijui kuniita dear amewaza nini. Sipendi hii tabia.

Sasa leo mimi nimefiwa na mjomba wangu jamani kwanza nipeni pole maana nina majonzi ya kutosha. Huyu mjomba tumeishi nae kipindi nipo mdogo, so ni mjomba wangu wa karibu sana. Rambi rambi napokea.

Nikapost whatsapp status rest in peace my uncle..kuna dogo mmoja ambaye ni fundi seremala huwa namtumia kunitengenezea baadhi ya kazi zangu akarespond ile status akasema "pole dear". Nimejibu asante lakini nimejiuliza sana huyu dogo vipi kuniita dear wakati hatuna hata mazoea nae zaidi ya kazi mara moja moja kuniita mimi dear. Sijapenda naona kama ni ukosefu wa adabu.

Je nyie wenzangu neno dear mnalitumia kwa watu aina gani? Mimi nalitumia kwa mpenzi na kwa mashosti zangu wa karibu kabisa.
Kweli tujitahidi kuoa mtu ata aliefika form four tu. Hawa ndio wale Wanakwambia I love you, Ukijibu ''I love you more" Anasema umemuita ng'ombe. Wewe ni kumbafu dear.
 
Ni ushamba wako, kwenye barua official ya kiingereza ya ku address kwa mtu au kampuni iwe maombi ya kazi, mkopo etc, huwa tunaanza na Dear Sir/Madam.... Huyo mtu unamjua!?, dear ni neno la kuonyesha ukarimu kwa mtu, na inaelekezwa kwa mtu unayemthamini. Google utaelewa zaidi.
Uzi ufungwe
 
Shida kuitwa dear na mtu nisiyemfahamu. Dear how?
Ambacho nimeelewa tu ulimdharau yule dogo kisa hana hela na ukaona hana hadhi ya kukuita dear. Umeongea sana kwa mihemko. Ila we ni mshamba ata kama una hela kaa utulie na utulizane. We unataka mtu akufahamu ndio akuite dear ili iweje? Punguza dharau heshimu kila mtu na we uheshimiwe. Ona sasa umeonekana punguani huku. Voda wanavyokuitaga dear customer unawafahamu?😂😂😂
 
Back
Top Bottom