Nilikuwa nasoma FTC wakati huo, halafu kuna jirani yetu home, yeye alikuwa anasoma pale chuo cha ardhi Dar. Sasa wakati wa likizo tukakutana kitaa, mwana alikuwa third year pale ardhi na mimi ndo first year. Si akaniuliza nasoma kupata leve gani pale chuo ninaposoma. Nikamjibu FTC..!! AKANIAMBIA DAH..!! WATU SAA HII WANASOMA ADVANCED DIPLOMA NA DEGREE WEWE UNANGÁNGÁNA NA FTC..!! Aisee, alinipa hasira. Nikapambana mpaka nikamaliza FTC na kuingia FoE na kufanikiwa kupata BSc in Eng.
Wakati mwingine maneno makali tunayoambiwa na wanaotuzunguka, yanatutia nguvu ya kusonga, kwa maana ya kuwa-pruvu wrong walioyatamka