Neno gani ambalo ulishawahi kuambiwa dhahiri likakukatisha tamaa?

Neno gani ambalo ulishawahi kuambiwa dhahiri likakukatisha tamaa?

Mi na watoto wengi sitegemei unisaidie na simsaidii hata 10 kila mtu na mpango wake.
 
Kuna mwaka mzee wangu alifariki sasa kuna ishu nikawa nafuatilia kwenye ofisi moja ya serikali nikaambiwa nikamuone boss mmoja nakumbuka jina lake ni shirima....alichonijibu yule mzee sintosahau japo ni more than 20 years ago. Na nilishamlaani sintomsamehe..nilitamani nikajiunge alshabaab nirudi kumuonesha show kwa kauli ile ya kudharau kifo cha mzee wangu na kunifukuza kama mbwa. Ukizingatia jinsi tulivyomuuguza mzee kwa mda mrefu na alivyoteseka. Siku hiyo nilirudi home maza akaniuliza feedback sikumjibu nikaenda kwanza kujifungia geto...badae nikamwambia tu maza ningekua na uwezo wa kupata bunduki leo ningetafuta...na hapo nilikua o level tu. Sometimes nikiona madogo wameingia kwenye makundi ya kigaidi siwalaumu sana. Life pushes them to the limit na hawaoni option sababu kila mtu kama kawatenga

Acha majungu Mzee alifanya nini???????
 
"Hivi nelly ukipaangalia kwenu na kwetu unaweza kuwa na girl kama mimi"

Ilipelekea nika-fail mtihani muhimu sana shule ila mungu sio massawe demu ameolewa ila mimi ndio kama mume vile.


Kuna siku aliwahi kuniambia ile kauli anaijutia sanaa hata kama nilishamsamehe na kuahidi kunipenda mpaka kufa
😂😅 Na ukajitoa akili ukamuamini mwanamke huyohuyo tena... Amecheza na fursa na akili yako tu
 
Kauli kama hizo huambiwa ili ukate tamaa na ushindwe kufikia malengo yako..tatizo ni pale unapoamua kukomaa.huwa wanapoteana...
 
nilikua najiendeleza nasoma chuo kimya kimya huku nafanyakaz, baada ya mwaka kazin watu wakajua kuwa ninajiendeleza, basi wakanidodosa wakajua nasoma course gani, walinicheka sana wakasema mimi kilaza hiyo course nitafeli 😂 na kweli course ilikua na baadhi ya masomo kama matatu yananipiga chenga... Basi walivyo ona mimi nimeanza kusoma kilamtu akaanza kusema ikifika mwakani lazima asome, kuna mfanyakaz mwenzangu alikua anajiona yeye ndio yeye mtaalam wa kilakitu alikua anawaambia watu kwamba mimi nitafeli kwasabab hio course siiwez sina msingi mzuri kuliko yeye mtaalam, next year kweli akasoma the same course niliyosoma mimi na chuo hicho nilichosoma, after 2yrs ilitakiwa a graduate tukashangaa anaanza kusema Supervisor wake amemlostisha kwenye Research kwahio hadi mwakani 😂 kunasiku tupo ofisini ni jamaa fulani wambea sana walikua wanapekua majina ya watu Google wakapekua langu wakaona Research yangu imepandishwa ktk website ya chuo na kwamba nime graduate... Huku na huku wakam Google na jamaa eeeenh si wakakuta chuo wameorodhesha majina ya watu walio Disco jamaa jina lake lipo 😂 aiseee nilicheka sana. Ila nikawaambia washikaj mkaushieni msimtangaze jamaa kwamba ameDisco 😂 wakasema poa baada ya wiki tu umbea uliwashinda kuvumilia wakawaambia watu waingie kwenye website ya chuo waone jamaa alivyo disco... From there kilamtu alianza kuniheshim maana walidhani sija graduate. Yule jamaa alikonda kwa stress baada ya siri yake kuvuja hadi leo ananionea aibu bahat nzuri nilihama kazi nikapata nyingine nzuri zaid
 
Nilienda interview fulani we acha Kuna jamaa alinicheka tukiwa kweny foleni jamaa alimaliza mwaka mmoja kunizidi mimi .... Sasa wakati tunaingia ananicheka kwa vile kaumbo kadogo then sina time na mtu kumbe yeye alikuwa na connection tayar ila huwezi amini leo niko nae ofisi moja .

Siku tunasaini mkataba dah!! Ananiangalia kwa chuki mi sina time nae roho mbaya tu.

Ila roho yangu imegoma kuwa na shobo nae mwaka wa pili na nusu hata namba nimefuta alinionyesha dharau sana kisa yeye ni bonge bong ivi.
Watu wafupi mna shida sana aisee [emoji1][emoji1]
 
Baba Mdogo aliwahi kuja home, akakuta mshua analalamika kuhusu mimi kuhusu kumwambia anipe baraka zake nipambane kivyangu.

Wakachukulia kwamba, nimechoka kuchunga ng'ombe. Baba mdogo akaanza kunitukana akiniambia kwamba usipopenda ng'ombe na ukiziacha hizi ng'ombe hutakuja kufanikiwa kamwe! Kufanikiwa kwako ni kuchunga hawa ng'ombe hadi mwisho!

Alinipa maneno ya kuumiza sana na yenye hasira na ndio chanzo cha mimi kuleta ule uzi wa kujilipua Iringa.

Juzi ananipigia simu nimtumie hela ana shida imem'bana halafu kashindwa kuuza ng'ombe wake.

Ila mi hakunikatisha tamaa bali kama alinijaza nguvu.
 
Kuna mchizi mmoja tulipiga wote o-level, jamaa alikua kichwa sana necta alifumua A za kutosha

Sasa baada ya kumaliza form 4 tukapoteana maana advance kila mtu alishika njia yake.

Sasa baada ya kumaliza advance nikajiunga na chuo kimoja hapa Dsm. Sasa wakati wa harakati za kufanya registration nikakutana nae hapo chuoni

Nilifurahi sana kumuona, nikamuuliza vp umekuja kufanya registration. Jibu alilonipa..me siwezi kusoma chuo kama hiki hakina hadhi.

Kauli yake mpaka leo naikumbuka ingawa haikunikatisha tamaa. Nilisoma na kumaliza chuo hicho hicho alichokiponda na maisha yanaenda fresh tu. Yeye sijui yupo ingawa nasikia yupo kawaida tu, ujiniasi wake haujamsaidia bado

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Baba Mdogo aliwahi kuja home, akakuta mshua analalamika kuhusu mimi kuhusu kumwambia anipe baraka zake nipambane kivyangu.

Wakachukulia kwamba, nimechoka kuchunga ng'ombe. Baba mdogo akaanza kunitukana akiniambia kwamba usipopenda ng'ombe na ukiziacha hizi ng'ombe hutakuja kufanikiwa kamwe! Kufanikiwa kwako ni kuchunga hawa ng'ombe hadi mwisho!

Alinipa maneno ya kuumiza sana na yenye hasira na ndio chanzo cha mimi kuleta ule uzi wa kujilipua Iringa.

Juzi ananipigia simu nimtumie hela ana shida imem'bana halafu kashindwa kuuza ng'ombe wake.

Ila mi hakunikatisha tamaa bali kama alinijaza nguvu.
mkuu watu wanashindwa kufananisha kauli mbaya na hard love,mfano mshikaji akikuambia"we jamaa usipopunguza pombe kaburi lako ntachimba kwa hasira sana".
kauli kama hiyo ni hard love
 
Back
Top Bottom