Neno gani ambalo ulishawahi kuambiwa dhahiri likakukatisha tamaa?

Mi na watoto wengi sitegemei unisaidie na simsaidii hata 10 kila mtu na mpango wake.
 

Acha majungu Mzee alifanya nini???????
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜… Na ukajitoa akili ukamuamini mwanamke huyohuyo tena... Amecheza na fursa na akili yako tu
 
Kauli kama hizo huambiwa ili ukate tamaa na ushindwe kufikia malengo yako..tatizo ni pale unapoamua kukomaa.huwa wanapoteana...
 
nilikua najiendeleza nasoma chuo kimya kimya huku nafanyakaz, baada ya mwaka kazin watu wakajua kuwa ninajiendeleza, basi wakanidodosa wakajua nasoma course gani, walinicheka sana wakasema mimi kilaza hiyo course nitafeli ๐Ÿ˜‚ na kweli course ilikua na baadhi ya masomo kama matatu yananipiga chenga... Basi walivyo ona mimi nimeanza kusoma kilamtu akaanza kusema ikifika mwakani lazima asome, kuna mfanyakaz mwenzangu alikua anajiona yeye ndio yeye mtaalam wa kilakitu alikua anawaambia watu kwamba mimi nitafeli kwasabab hio course siiwez sina msingi mzuri kuliko yeye mtaalam, next year kweli akasoma the same course niliyosoma mimi na chuo hicho nilichosoma, after 2yrs ilitakiwa a graduate tukashangaa anaanza kusema Supervisor wake amemlostisha kwenye Research kwahio hadi mwakani ๐Ÿ˜‚ kunasiku tupo ofisini ni jamaa fulani wambea sana walikua wanapekua majina ya watu Google wakapekua langu wakaona Research yangu imepandishwa ktk website ya chuo na kwamba nime graduate... Huku na huku wakam Google na jamaa eeeenh si wakakuta chuo wameorodhesha majina ya watu walio Disco jamaa jina lake lipo ๐Ÿ˜‚ aiseee nilicheka sana. Ila nikawaambia washikaj mkaushieni msimtangaze jamaa kwamba ameDisco ๐Ÿ˜‚ wakasema poa baada ya wiki tu umbea uliwashinda kuvumilia wakawaambia watu waingie kwenye website ya chuo waone jamaa alivyo disco... From there kilamtu alianza kuniheshim maana walidhani sija graduate. Yule jamaa alikonda kwa stress baada ya siri yake kuvuja hadi leo ananionea aibu bahat nzuri nilihama kazi nikapata nyingine nzuri zaid
 
Watu wafupi mna shida sana aisee [emoji1][emoji1]
 
Baba Mdogo aliwahi kuja home, akakuta mshua analalamika kuhusu mimi kuhusu kumwambia anipe baraka zake nipambane kivyangu.

Wakachukulia kwamba, nimechoka kuchunga ng'ombe. Baba mdogo akaanza kunitukana akiniambia kwamba usipopenda ng'ombe na ukiziacha hizi ng'ombe hutakuja kufanikiwa kamwe! Kufanikiwa kwako ni kuchunga hawa ng'ombe hadi mwisho!

Alinipa maneno ya kuumiza sana na yenye hasira na ndio chanzo cha mimi kuleta ule uzi wa kujilipua Iringa.

Juzi ananipigia simu nimtumie hela ana shida imem'bana halafu kashindwa kuuza ng'ombe wake.

Ila mi hakunikatisha tamaa bali kama alinijaza nguvu.
 
Kuna mchizi mmoja tulipiga wote o-level, jamaa alikua kichwa sana necta alifumua A za kutosha

Sasa baada ya kumaliza form 4 tukapoteana maana advance kila mtu alishika njia yake.

Sasa baada ya kumaliza advance nikajiunga na chuo kimoja hapa Dsm. Sasa wakati wa harakati za kufanya registration nikakutana nae hapo chuoni

Nilifurahi sana kumuona, nikamuuliza vp umekuja kufanya registration. Jibu alilonipa..me siwezi kusoma chuo kama hiki hakina hadhi.

Kauli yake mpaka leo naikumbuka ingawa haikunikatisha tamaa. Nilisoma na kumaliza chuo hicho hicho alichokiponda na maisha yanaenda fresh tu. Yeye sijui yupo ingawa nasikia yupo kawaida tu, ujiniasi wake haujamsaidia bado

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
mkuu watu wanashindwa kufananisha kauli mbaya na hard love,mfano mshikaji akikuambia"we jamaa usipopunguza pombe kaburi lako ntachimba kwa hasira sana".
kauli kama hiyo ni hard love
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ