Hapa kazi halali tuu.
Mama Samia hana msaidizi ,hana mtu wa kumpigania.
Hana baraza la mawaziri watiifu kwake ,yamkini hata waziri mkuu wa awamu ya tano anaonekana hayupo kwake mana hajaingia kwenye boti ya mama Samia.
Naendelea kumsihi Mh. Rais wetu kwa wema kabisa na kwa usalama mkubwa kwa uongozi wake na kwa Taifa letu. Hii nchi ni kubwa kuliko mtu aliyeko hai au aliyekufa.
Mwenyezi Mungu ameamua kuwa wengine wapumzike milele na wengine waendelee kujenga nchi.
Mama Samia Mungu amekupa Utawala wa nchi yenye katiba na Jeshi imara sana lililojengwa kwenye misingi imara ya kulinda nchi yetu na sio vibaraka wanaojali matumbo yao. Usimuogope mtu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake.
Mkuu wa Majeshi yupo na ameilinda katiba yetu kwa vitendo anastahili kuvishwa nishani ya utumishi uliotukuka.
Hawa wanasiasa wana ndimi mbili. Walikua wanajinasibu kuwa wanapambana na matumizi manaya ya umma kumbe walikua wanapambana ili kujenga himaya ya mtu mmoja na watu wake.
Hata madege, madaraja marefu kabisa,miradi mingi ya mabilioni , teuzi za madaraka kuanzia chini mpaka juu , mareli yote yalielekezwa nyumbani kwake. Hivyo alitengeneza kundi kubwa na imara sana la kutetea kila alichokua anakifanya yeye na serikali yake kiwe kizuri au kibaya.
Aliteua watu watiifu sana kwake. Watu walioweza kufanya chochote alimradi jamii ifyate mkia na kupiga makofi ma kusifu tuu.
Sasa Mh. Rais wa awamu ya sita ameamua kuwachukua wapambe wa Mtangulizi wake aliyekua ana mipango ya wazi na ya siri ambayo mingi ilivunja katiba kwa makusudi makubwa huku waliokua wanaivunja wakifurahia mateso ya wengine kwa tu ya kumfurahisha mtu .
Sasa ni awamu ya Sita. Mh.Rais kupanga ni kuchagua .
Ama uendelee nao hao ambao hawakukutii tangu mwanzo mana walikuona ni mpole na hawajawahi kuwaza kuwa ingetokea siku moja ukawa mkuu wa nchi na ukawatawala kwa misingi ya katiba na ukaja na slogan yako na wakapaswa kuiheshimu.
Piga chini Wale wote ambao wamekalia ofisi bila uteuzi wako. Bora lawama kuliko fedheha.
Watu wanakaa kwenye mitandao wanamkashifu rais aliyeko hai na kumfanya ni duni dhidi ya alisiyepo.!!!!!!!!!! Kweli tumefikia hapoo!!!!!!
Jeshi la polisi lisikubali kurudi nyuma wakati sheria zipo .
JWTZ wametekeleza wajibu wao kwa dhati kabisa.
Kwenye nafasi zisizo za kisiasa sasa turudi enzi za kuwateua watu kutoka kwenye majeshi yetu ya polisi na JWTZ hasa makanali na maCapt kuwa wakuu wa mikoa na Wilaya na sio hao wasiofuata katiba ya nchi na kuamua kujipangia wanavyotaka.
Piga chini wote waliotuhumiwa kwenye ripoti ya CAG bila kupepesa ili ujenge uadilifu kwenye taifa hili. Watu wanadhulumu sana fedha za umma hasa kwenye miradi.
Nenda stand moja pale Korogwe ,ilijengwa kwa mabilioni ya fedha na aliyeifungua aliwasifu sana na kuwapandisha vyeo wajenzi wale. Mimi kama mtumishi wa Mungu aliye hai nikajiuliza mabilioni haya yameishaje pale. Nilikosa majibu kabisa.
Leo miaka minne tuu ile stand imebaki mashimo na inafukuliwa upya pesa zinazidi kuteketea.
Hatuwezi kwenda mbele kwa hali hiyo. Bunge limegeuka kuwa uwanja wa kuyetea maovu ya wapigaji wachache ndani ya serikali.
Ni wakati sasa wa mh. Rais kuwateua watu waaminifu ,watiifu kwake na kwa katiba ya nchi.
Eti wanasema team fulani imerudi. Kama ni watanzania wenye nia njema basi Mungu ameamua hivyo ,watende kwa uadilifu alimradi hawamwonei mtu.