Neno langu kwa wasaliti wote wanaorejea CHADEMA: Karibuni nyumbani, ila....

Selasini bado ni pandikizi ama hana misimamo thabiti.. Ni rahisi sana kununulika
Kuna jambo moja hapa JF bado sijalielewa:

Mada za Lucas na wenzake wengi mara nyingi zinakuwa mbele ya uso wa jukwaa hili la siasa; wakati huo huo mada kama hii inakuwa pembeni kabisa isionekane kwa haraka?

Kuna mpangilio maalum wa vipaumbele wa aina za mada?

Mfano mwingine ni habari zinazomhusu Kafulila.

Nimeona nilitoe dukuduku hili mbele kabla ya kujadili mada ili nieleweshwe mpangilio huu unatokana na nini!

Ngoja nigusie mada yako kidogo hapa:

Hali hii ya umalaya wa kisiasa umekuwa ni utamaduni unaokuzwa na CCM.
Hebu jaribu kujenga picha ya hali itakavyokuwa ndani ya CCM wakitolewa madarakani. Kuna mwanachama wa chama hicho atakayebaki kwenye chama bila ya kuwa na uhakika wa kuwa na madaraka kama ilivyo sasa?

Hawa akina Msigwa na wengine wengi, ndiyo sura halisi ya malaya wa kisiasa inayolighubika taifa hili.

Ninakubaliana karibu na yote uliyoweka kwenye mada hii muhimu. CHADEMA sasa ni muhimu wawe na taratibu za kuchuja wanaoingia kwenye uongozi wa chama kwa umakini mkubwa sana.

Uingi wa wanachama wasiokuwa na 'commitment' juu ya chama ni hasara kubwa, na mbaya zaidi, watu hao wanapojipenyeza katika nafasi za uongozi, hiyo inakuwa ni hasara kubwa kwa waTanzania wote bila kujali misimamo ya vyama.

Akina Samia wapo hapo walipo sasa; hata kama hawakuwa na sifa zozote za kuwafikisha hapo walipo.

Hali hii ni lazima ikomeshwe.
 
Hata Mbowe akirudi naye atabaki kuwa mwanachama tu kwani heshima aliyopewa ya kuwa mjumbe wa kudumu wa CC ya Chadema aliikanyaga kwa kukubali kuwa kibaraka wa Samia.
 
Siasa sio mpira wa miguu unaweza kuhama tu au kununuliwa na team yoyote

Kufananisha siasa na mpira wa miguu ni kutokujua thamani ya siasa kwenye Maisha ya watu

Siasa huwezi kulinganisha na simba na Yanga huu ni upumbavu

Siasa ni seriously business inaingia kwenye Kila sekta ya Maisha ya raia

Siasa ni sera na sera ni fikra na fikra ndizo zinatoa Miongozo wa MAISHA ya jamii

Haiwezekani tuwe na viongozi wanaobadilika Ovyo msimamo yao Kwa sababu ya vyeo
 
Sina shaka na Msigwa na Selsini wote walimkimbia Mbowe na siasa zake. Sasa wamerudi kumfuats Lissu na siasa ngumu.
Siasa sio mpira wa miguu unaweza kuhama tu au kununuliwa na team yoyote

Kufananisha siasa na mpira wa miguu ni kutokujua thamani ya siasa kwenye Maisha ya watu

Siasa huwezi kulinganisha na simba na Yanga huu ni upumbavu

Siasa ni seriously business inaingia kwenye Kila sekta ya Maisha ya raia

Siasa ni sera na sera ni fikra na fikra ndizo zinatoa Miongozo wa MAISHA ya jamii

Haiwezekani tuwe na viongozi wanaobadilika Ovyo msimamo yao Kwa sababu ya vyeo
 
Bado Hezekiah wenje nae atarudi Tu nyumbani.
CCM hawana tena pesa zile za kuchezea za Msaada kutoka ulaya, hawa akina msigwa walihaidiwa pesa nyingi na vyeo serikali lkn kutokana na UKATA SERIKALINI wametoswa kama mawe baharini
 
Ujumbe mzuri sana mkuu , kamti kuu wachukue
 
MUOGOPE BINADAMU MWENYE TABIA YA KINYONGA🚶🚶🚶
 

Kama ambavyo sikuwahi kuwaamini akina Slaa, Lowassa na Sumaye hawa akina Msigwa ndiyo kabisa kwangu ni red flag.
Kazi kwenu humo ndani ya chama.
 
Umesoma wapi nimefananisha na mpira wa miguu? Daa, wabongo tuna tatizo la kusoma kwa ufahamu. Na pia sijasema tuwe na viongozi wanaobadilika hovyo bali nimesema wanaobadilika kulingana na hali halisi.
 
Hapana mkuu 'macho' kwa hili la Msigwa tusilihusishe na mchezo wa kisiasa hata kidogo.

Ningekubaliana na wewe kama huyu Msigwa asingejihusisha na kujitangaza na kukisema chama alivyofanya alipohamia huko CCM.

Msigwa ni 'case study' sahihi kabisa ya ubovu wa siasa zilizoingizwa na CCM ndani ya taifa hili.
Siasa imekuwa ni biashara zaidi kuliko kutumikia watu na taifa',; na hali itaendelea hivyo hivyo hata CCM wakitolewa madarakani iwapo maswala ya aina hii ndiyo yatakubalika kama kawaida ya siasa

Kuyakataa haya ni lazima kuanzie kwa wananchi. Mtu wa aina hii katika nchi zenye misimamo hapati kura za wananchi; na hata uongozi ndani ya chama hapati

Kwanza muulize, CHADEMA ingeathirika baada ya yeye kwenda kuchochea moto; angepata wapi nafasi ya kuja tena na kujifanya yeye ni sehemu ya CHADEMA tena?.
 
Msigwa hana chembe chembe za usaliti . Namuamini 100%
 
Msigwa hana chembe chembe za usaliti . Namuamini 100%
Kama wewe si Msigwa basi ndugu yake au amekulipa kumsafisha, hakuna binadamu anayeweza kumuamini binadamu mwingine kwa 100% katika mazingira yoyote sasa tuweka mfano wa Msigwa ambaye kwanza ni mwanasiasa(never trust politicians) na pili ni msaliti mbobevu(habitual traitor) ambaye ana uzoefu wa kutafuna kauli zake mwenyewe.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu Kalamu kuna jambo moja ambalo nina uhakika nalo kwa asilimia kubwa kabisa. Siku CCM ikiondoka na tukapata viongozi wenye akili walau kidogo tu, na pia katiba nzuri, hizi sarakasi za kuhama vyama hovyo hovyo zitapungua sana. CCM ni kama shetani wa Tanzania na karibu kila kibaya kibaya kinachoendelea kwenye siasa sasa hivi ni kwa sababu yake. Kwa mfano suala la Msigwa. Kama Abdul asingetoa fedha kwa Mbowe, Msigwa asingehama. Msigwa alihama kwa sababu alishughulikiwa na Mbowe kwani alikuwa team Lissu. Ndiyo maana hakuwa anasema vibaya viongozi wengine kama Lissu. TAFAKARI: Je, utakubaliana na mimi kuwa hata Lissu angekuwa ameshindwa ule uchaguzi kuna uwezekano mkubwa angekuwa nje ya CHADEMA huku anaikosoa? Yes. Msigwa alifanya kosa kuingia CCM, na mbaya zaidi kumsifia kilaza Samia...
 
Yes. Msigwa alifanya kosa kuingia CCM, na mbaya zaidi kumsifia kilaza Samia...
-Aliusifia uchaguzi wa Oct,2025.
-Alifanya jitahada kubwa(kwa kauli zake) kupambana kuisambaratisha, kuidhoofisha pia kujaribu kuiua kabisa CHADEMA na kama kingekuwa kimekufa sijui angerudi kwenye chama kipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…