Neno langu kwa wasaliti wote wanaorejea CHADEMA: Karibuni nyumbani, ila....

Neno langu kwa wasaliti wote wanaorejea CHADEMA: Karibuni nyumbani, ila....

1779704342752.jpg
 
Kuna jambo moja hapa JF bado sijalielewa:

Mada za Lucas na wenzake wengi mara nyingi zinakuwa mbele ya uso wa jukwaa hili la siasa; wakati huo huo mada kama hii inakuwa pembeni kabisa isionekane kwa haraka?

Kuna mpangilio maalum wa vipaumbele wa aina za mada?

Mfano mwingine ni habari zinazomhusu Kafulila.

Nimeona nilitoe dukuduku hili mbele kabla ya kujadili mada ili nieleweshwe mpangilio huu unatokana na nini!

Ngoja nigusie mada yako kidogo hapa:

Hali hii ya umalaya wa kisiasa umekuwa ni utamaduni unaokuzwa na CCM.
Hebu jaribu kujenga picha ya hali itakavyokuwa ndani ya CCM wakitolewa madarakani. Kuna mwanachama wa chama hicho atakayebaki kwenye chama bila ya kuwa na uhakika wa kuwa na madaraka kama ilivyo sasa?

Hawa akina Msigwa na wengine wengi, ndiyo sura halisi ya malaya wa kisiasa inayolighubika taifa hili.

Ninakubaliana karibu na yote uliyoweka kwenye mada hii muhimu. CHADEMA sasa ni muhimu wawe na taratibu za kuchuja wanaoingia kwenye uongozi wa chama kwa umakini mkubwa sana.

Uingi wa wanachama wasiokuwa na 'commitment' juu ya chama ni hasara kubwa, na mbaya zaidi, watu hao wanapojipenyeza katika nafasi za uongozi, hiyo inakuwa ni hasara kubwa kwa waTanzania wote bila kujali misimamo ya vyama.

Akina Samia wapo hapo walipo sasa; hata kama hawakuwa na sifa zozote za kuwafikisha hapo walipo.

Hali hii ni lazima ikomeshwe.
1779704514342.jpg
 
Kama mnavyofuatilia siasa za nchi yetu hivi sasa, kuna wimbi kubwa la wanachama waliokihama chama na kukipigia kelele nyingi za kashfa wakiondoka, lakini sasa hivi wanarudi CHADEMA kwa kasi ya ajabu.

Kama mwanachama na mdau wa mabadiliko ya dhati, naomba niwaambie hawa wanaorejea maneno machache ya ukweli mchungu bila kuwatafuna maneno.Kwanza kabisa.!

CHADEMA ni taasisi imara yenye misingi, na siyo duka la fursa za kisiasa au daraja la kupatia vyeo kwa haraka baada ya njaa kuwakamata huko mlikokuwa mmetorokea.

Tusisahau historia, kwani takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya makada waliokihama chama kati ya mwaka 2015 na 2025 kuelekea chama tawala walifanya hivyo kwa ahadi za vyeo au maslahi ya kiuchumi.

Leo hii, baada ya upepo wa kisiasa kubadilika na wengi wao kuachwa pembeni kwenye teuzi za serikali na ndani ya chama huko walikoenda, wanarudi CHADEMA kwa kasi.

Hatuwezi kugeuza chama kuwa dampo la kisiasa . Hakuna aliyerejea anayepaswa kupewa kipaumbele cha uongozi, kuteuliwa kugombea nafasi yoyote, au kupangiwa safu ya mbele kabla ya kukaa benchi na kuthibitisha uaminifu wake upya kwa muda mrefu.

Ili kuzuia usaliti mwingine wa kiitikadi, ni sharti wapitie mafunzo ya kina ya kiitikadi ili waelewe misingi ya chama ya Ulinganifu na Ustawi (Center-Right).Pili, kurejea CHADEMA kusichukuliwe kama jambo la kawaida la kisiasa;
Ni lazima wanaorejea wakiri hadharani usaliti wao na madhara makubwa waliyokiletea chama kwa kauli na vitendo vyao walipokuwa uhamishoni.

Wanachama waliovumilia dhoruba, wakitukanwa, wakifungwa magerezani, na kupoteza mali zao wakati wasaliti wakifurahia fursa katika vyama vya kidikteta, wanastahili kuombwa radhi ya dhati na ya wazi kabisa.

Waliorejea wanapaswa kuweka pembeni kiburi chao chote, washushe vitisho vyao, na wakubali kwa unyenyekevu mkubwa kuanza upya kama wanachama wa kawaida kabisa kuanzia ngazi ya msingi ya matawi.

Huwezi kuondoka ukiwa nahodha aliyetupa machela baharini, halafu ukarudi ukataka kupewa usukani wa meli mara moja!
Tatu, maneno matamu ya majukwaani, machozi ya mamba, na sifa za kishabiki hazitatosha hata kidogo kufuta majeraha makubwa ya usaliti; matendo ya kila siku ndiyo yatakayorudisha imani iliyopotea.

Historia ni mwalimu mzuri sana na inatupasa kukumbuka jinsi chama kilivyoyumba wakati wa vuguvugu la "Mamluki na Wasaliti" wa mwaka 2013/2014, na hata jinsi baadhi ya wabunge na madiwani walivyonunuliwa mchana kweupe mwaka 2017/2018 chini ya mkakati uliogharimu mamilioni ya kodi za wavuja jasho kwa kisingizio cha "kuunga mkono juhudi".

Kurudi kwa watu hawa bila kuchujwa kwa mifumo thabiti ya kiusalama (Intelligence ya Chama) ni kuwakaribisha maadui sebuleni huku tukijua wana njaa ya madaraka.

Kila anayerejea lazima aonyeshe utiifu wa asilimia mia moja kwa Katiba ya chama, miongozo, na maamuzi yote ya vikao halali vya chama.

Viongozi na mifumo ya usalama ya chama ipo macho sana sasa hivi, na jaribio lolote la kurejea kama mamluki au "pandikizi" litagundulika mapema na kushughulikiwa kwa kufukuzwa bila muhali, huruma, wala mjadala wa pili.

Mwisho kabisa wakuu, kurejea kwa waliokiacha chama kuwakumbushe wanachama watiifu umuhimu wa kulinda misingi, kushikamana, na kutovunjika moyo wakati wa dhiki kwani ukweli daima hushinda uongo na hila.

Mapokezi ya wanaorejea yaambatane na umakini mkubwa sana na tahadhari ya hali ya juu, huku macho ya kila mwanachama yakiwa wazi kulinda usalama, siri, na mikakati yote ya chama kuelekea chaguzi kuu zijazo.

CHADEMA ni salama na ni kimbilio kwa kila Mtanzania mwenye nia njema na ya kweli ya kuikomboa nchi, lakini ni moto mkali utakaomteketeza kila anayetaka kukichezea na kukitumia chama hiki kama kitega uchumi chake binafsi.View attachment 3593924
Asante kwa ujumbe mzuri bila shaka viongozi wataufanyia kazi
 
WanaCHADEMA mnaokihama chama chenu kuja CCM kwa nia ya kupata vyeo hakikisha una elimu kubwa pia hata huko CHADEMA una impact kubwa. Msigwa alikuwa na tamaa ya cheo ila kwa elimu yake duni asingeweza kuteuliwa hata kama mamlaka ya uteuzi ingekua na nia ya kumteua. Kisiasa Msigwa alikuwa heavyweight huko unyumbuni CHADEMA ila bahati mbaya kama ilivyo kwa Lema, Sugu na Yericko, alikuwa na elimu duni.
Mbona wenye elimu mbalimbali wana vyeo vikubwa ?
 
CHADEMA ni kama kenge tu mpaka damu iwatoke masikioni ndio watasikia.

1. Hivi ni nani asiyejua vituko vya huyo Jose Selasini alivyomfanyia Mbatia kule NCCR na wala sio miaka mingi ni juzi juzi tu. Lile halikuwa shambulio kwa Mbatia au NCCR bali kwa watu wenye akili timamu lile lilikuwa ni shambulio kwa demokrasia. Leo kawa mtakatifu anapokelewa CHADEMA kama shujaa kisa tu ni vimeseji vyake anavyoandika andika mitandaoni. Mna uhakika gani akipata nafasi hapo CHADEMA hatafanya aliyoyafanya kule NCCR?
2. Huyo Msigwa ndio kabisa aliitukana CHADEMA matusi ya nguoni na kuizushia mambo kibao ya uongo majukwaani naye leo anapokelewa kama shujaa. Ametubu lini?. Mbona aliondoka kwa kufanya "press" leo hii anarudi kwa kutweet. Kila siku kutamba majukwaani eti chama makini kuna umakini gani wakati mtu aliyeondoka anarudi kwa kutweet tu je hakuna utaratibu maalum maana watu watahahakikishaje kuwa ni kweli chama kimeridhia kurudi kwake na kwa masharti gani. Je mkipewa nchi taratibu, kanuni na sheria mtaweza kweli kuzisimamaia kama jambo dogo tu hili linawashinda kulisimamia?
3. Yale yale ya Dr. Slaa mpaka akaAndika kitabu kuituhumu CHADEMA mambo mazito lakini mpaka leo hajakana kama kile alichoandika si kweli lakini karudishwa CHADEMA.

Kwa kifupi CHADEMA hawajielewi kuwa wao ndio tumaini la watanzania. Wao na CCM ndio kama Simba na Yanga kwenye nchi hii. Kwa hiyo wasijiangalie wao kama viongozi tu na kujiamulia mambo kiholela na kuleta ushikaji kwenye mambo ya msingi. Wajue kuwa wana mashabiki ambao ndio wengi kuliko wanachama na maskini ya Mungu hao mashabiki hawajui hata kadi ya uanachama ni nini. Mkiendela kufanya mambo ya hovyo hata hao mashabiki wenu watatafuta vyama vingine vya kushabikia kama mnabisha katafuteni leo hii NCCR, CUF na hata TLP vilipoteaje kama sio kupoteza "trust" kwa mashabiki wao na wala hata sio wanachama kwani wanachama huwa wanahesabika lakini mashabiki huwa hwahesabiki.

Kama kweli CHADEMA inataka kuendelea kuwa chama kikuu basi hao wote wakina Msigwa, Selasini na wengineo waliorudi na watakaorudi basi wawe chini ya uangalizi kwa miaka mitatu au zaidi na kwa kipindi hicho wasiruhusiwe kupewa cheo chochote wawe tu wanachama wa kawaida. Hii itawapa moyo sana wale waliobaki kukipigania chama kwa jasho, machozi na damu. Pia itasaidia sana kuwafanya watu wawe loyal kwa chama wakijua kuwa nikihama tu mtaji wangu unaondoka na mimi na nikirudi lazima nianze kutengeneza mtaji upya kwa kukaa miaka mitatu bila wadhifa wowote. Kumbuka kuwa wakati hao wakina Msigwa, Selsini, na wengineo wakiwa huko walikokuwa wenzao walikuwa wana pita hali ngumu sana na wapo walioumia kimwili na kisaikolojia. Je hao waliopitia maumivu leo hii watajisikiaje wakiona hao jamaa wanapokelewa kwa mbwembwe na bashasha na wanapewa nyadhifa ili hali wao wanabaki na maumivu tu? Je sio mwanzo wa mgawanyiko wa ndani kwa ndani ya chama?

Ni mtizamo tu.
 

Too bad Msigwa. Your credibility is zero!

Akheri ya huyo kijana wako wa miaka 18 aliyekukumbusha jambo ambalo limekuchukua miezi kadhaa ukiwa kimya ; ukisubiri uteuzi uje!

Ni hivi: hii njia uliyochukuwa ya kujirudisha kwa nguvu ndani ya chama ulichokiasi; kwa kujitangazia mwenyewe ni moja ya makosa makubwa uliyofanya.
Ungetumia njia nyingine mbadala ingesaidia kidogo.

Wewe katika siasa za kweli, kama zitarudi Tanzania, wewe huna nafasi kabisa ndani yake.
Wewe sampuli yako ni hii inayoendeshwa na CCM sasa hivi, sampuli ambayo waTanzania wanatafuta kuizika kabisa kwa kuondoa CCM.
 
Yericko WHO?

Hiki kikaragosi bado kinayo mategemeo ya uteuzi toka kwa Samia mhalifu?
Aisome hii
"Karma shows NO mercy. The pain you give someone else: the lies, betrayal & disrespect. it always returns home harder & louder.🎯"
 
Back
Top Bottom