Neno 'Samaki' lipo kwenye ngeli gani?

Neno 'Samaki' lipo kwenye ngeli gani?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Wakuu,

Neno Samaki lipo kwenye ngeli ipi?

Je ni ngeli ya a-wa
Au ngeli ya i-zi

Ahsante
 
Yu-A-Wa
mfano
Umoja samaki amekufa
wingu samaki wamekufa
Mkuu umeongelea ngeli ya Yu - A- Wa lakini mfano uliotoa hausadifu kulingana na matumizi ya ngeli husika.
Mfano mzuri wa matumizi ya ngeli hiyo ni:
Umoja - Mtoto yualia/mtoto analia
Wingi - Watoto wanalia
[emoji106]
 
Asante,Ngeli ya yu-a-wa inakuaje?
Yu na a zinatumika kwa viumbe hai mara nyingi kama sijakosea Ngeli yu inatumika kwa baadhi ya viumbe na pia kuonesha mahari kiumbe alipo(mahali)
 
Ok, mfano wa sentensi inakuwaje maana imenichanganya
nimevuta picha nimesahau nikitambo sanaa ila ngoja niwekee hii akija mtu anaielewa Ngeli ya Yu atanisahisha
Mfano
Umoja.. Samaki yupo
wingi ..samaki wapo
 
Dah! Haya mambo ndo yalisababisha nipate Kiswahili "C" haya!

Ya-wa tena?!

Ashukuriwe ambae alileta mambo ya kusoma vitabu na kwenda kutirika kwenye paper manake hadi namaliza Form IV, ilikuwa nikishasoma comprehession na kujibu maswali, kisha nikienda kwenye Fasihi, nikimaliza tu; huyoooo, nasepa zangu na mambo sijui ya tungo changamano sijui nyambulisha Kiima na Kiarifu, sijui mofimu (hivi ndo kinini hiki?!) nawaachia wenyewe coz' always hizo parts 2 zilikuwa zinanihakikishia C!!
 
Dah! Haya mambo ndo yalisababisha nipate Kiswahili "C" haya!

Ya-wa tena?!

Ashukuriwe ambae alileta mambo ya kusoma vitabu na kwenda kutirika kwenye paper manake hadi namaliza Form IV, ilikuwa nikishasoma compression na kujibu maswali, kisha nikienda kwenye Fasihi, nikimaliza tu; huyoooo, nasepa zangu na mambo sijui ya tungo changamano sijui nyambulisha Kiima na Kiarifu, sijui mofimu (hivi ndo kinini hiki?!) nawaachia wenyewe coz' always hizo parts 2 zilikuwa zinanihakikishia C!!
uko vizuri mkuuu Mbona
 
Mkuu umeongelea ngeli ya Yu - A- Wa lakini mfano uliotoa hausadifu kulingana na matumizi ya ngeli husika.
Mfano mzuri wa matumizi ya ngeli hiyo ni:
Umoja - Mtoto yualia/mtoto analia
Wingi - Watoto wanalia
[emoji106]
Mkuu ngeli ya Yu hutumika kama mbadala wa ngeli ya A kwenye baadhi ya sentensi... mfano Yuaja
 
Back
Top Bottom