Chief, ni hivi ngeli ya YU - A - WA matumizi yake huwa na mbadala yaani isipotumika YU kwenye umoja basi itatumika A, lakini kwenye wingi ndio itatumika WA.
Mfano:
Mtoto yualishwa
Mwalimu yuafundisha
Mzee yuazeeka
Hii ngeli ya YU - A - WA ipo kilahaja zaidi na sio kiswahili sanifu kwani si katika hali ya kawaida kumkuta mtu anatumia neno yualishwa, yualia, yuafundisha au yuanakula badala ya kutumia analishwa, analia, anafundisha, anakula.
Kwa Tanzania baadhi ya maeneo ya mwambao pamoja na maeneo ya Visiwa vya Zanzibar, sana sana kisiwani Pemba ndio inatumika lahaja hiyo (lafudhi).