Navyofahamu mimi, 4WD ni injini kuzungusha/kuvuta tairi zote nne. Kuna IST zenye 4WD full time.
Kama ni tofauti, naomba unielimishe mkuu.
Hakuna kitu kama '4WD full time' . 4WD huwa inakua engaged au disengaged kulingana na model ya gar kwa kupress button / kuweka gear ya 4WD either 4H,4L / au kwa baadh kama nissan hard body ukitaka kuengage 4W unashuka kutoka ndani ya gar na kuzungusha vitufe vya duara katikati ya tairi za mbele na kulock gar kwenye 4WD.
Katika mfumo wa 4WD muda wote gar uwa ni zito na hutumia mafuta mengi maana muda wote engine huwa inasukuma gar kwa kuzungusha tairi zote nne za nyuma na mbele kwa wakati wote. Katika mfumo wa 2WD ambao ndio normal na ndio unatumika by default unapoweka gear yoyote engine uzungusha tairi mbili tu either za mbele au nyuma kulingana na model au aina ya gar.
Mbili zinazunguka mbili zinakuwa pushed na zile zinazozunguka hiyo ndiyo 2WD. 4WD inafaa katika mazingira magumu OFFROAD kwenye matope, milima au mwinuko mikali, mabonde, mchanga mwingi, makorongo, etc... Kwa gari ndogo na ya chini kama IST huwezi enjoy 4WD na kuna baadh ya maeneo IST haitapita hata kama utakua umeengage 4WD.
Gari za juu kama Toyota hilux, Toyota SURF, Prado, Landcruiser VX, Nissan hard body, Nissan Patrol, Jeep Cherokee, Ford Ranger, Voltswagen Amarok, Hummer, and the likes, yaan SUVs ndo tamu kwa 4WD kwenye offroad conditions tena ukute ile yenye option ya 4WD + DIFF LOCK.