Keshaliweka wazi kuwa hana shida na wananchi wa Palestina, shida yake kuifuta Hamasi na itikadi zake Gaza, ili sakata kama hili lisije kujitokeza tena kwa siku za usoni, hataki 'sizi faya' mpaka atakapomalizana kabisa na Hamas.
Kasema raia wanyonge wanakufa bure kwa sababu ya kuisapoti Hamas na kukubali kuwekwa kama ngao ya mashambulizi na tabu wanazozipata haziwastahili, si zao ni za Hamas yarabi.
Nadhani anarudisha mambo ya miaka ya 1980, kuwapiga Hamas na kuikalia kimabavu Gaza hadi hapo atakapowaundia utawala rafiki anaoutaka yeye.