Netanyahu: Tunakwenda Kutimiza ahadi yetu kwamba hakutakuwa na Taifa la Palestina eneo hili ni letu

Netanyahu: Tunakwenda Kutimiza ahadi yetu kwamba hakutakuwa na Taifa la Palestina eneo hili ni letu

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,112
Reaction score
34,951
1757683578203.png
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, siku ya Alhamisi alisema kuwa "hakutakuwa na taifa la Palestina." Alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake katika makazi ya Maale Adumim yaliyoko katika Ukanda wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Netanyahu alisaini rasmi hati ya kuidhinisha ujenzi wa maelfu ya nyumba mpya karibu na eneo hilo, kama sehemu ya mpango tata wa kupanua makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika Ukanda wa Magharibi.

Mpango huo unatarajiwa kukata kabisa muunganisho kati ya Ukanda wa Magharibi na Jerusalem ya Mashariki.
Mradi huo uliidhinishwa mwezi uliopita na serikali ya mrengo wa kulia ya Israel. Serikali kadhaa za Magharibi, zikiwemo Ujerumani na Ufaransa, zimeukosoa vikali mpango huo.

Makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika Ukanda wa Magharibi, ambao Israel iliukalia mwaka 1967, ni kinyume cha sheria za kimataifa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki.

Chanzo DW Kiswahili
 
Hapo ni mwendo wa kuviziana, ukijisahau mwarabu kaja kulipua makazi. Inshort hakuna Amani kabisa, unaishi roho juu juu muda wowote nafasi ikipatikana unatupiwa bomu...Nchi mbili ndio solution lakini wenyewe hawataki.
 
Anaota ndoto huku akitoa speech, kuongea ni kitu rahisi sana lakini kufanya hicho ulicho ongea ndio kazi.
 
.
Anaota ndoto huku akitoa speech, kuongea ni kitu rahisi sana lakini kufanya hicho ulicho ongea ndio kazi.
Kabla yake huko nyuma alikuwepo Gen. Ariel Sharon bulldozer, mbabe kwelikweli huyu mpoland Benjamin Mikeikowsy haiingii ndani, naye aliua sana wanawake na watoto kwenye kambi za Shabra na Shatila Lebanon akiwa Waziri wa Ulinzi 1982
Wakati anaondoa majeshi yake Gaza 2005 akiwa Waziri Mkuu aliahidi with utmost arrogance and insolence:
I will leave Gaza, and I will lock the gate, but I will burn Gaza if a single bullet reaches Israel from it!
Baadae IOF yalipoondoka makombora yakarushwa siku chache baada ya Israeli withdrawal kwenye hizo Zionist settlements, na kama kawaida ndege za Israeli zikaruka, burning, crushing, killing, and demolishing the Gaza Valley Bridge na kuharibu power plant, na hakuna hata kipande cha kioo kilichobaki hapa Gaza
Kilichotokea makombora Gaza hayakukoma zaidi ya yeye Sharon kupata stroke akalazwa miaka 2006-2014 hajitambui huku mwili unaoza tararibu akiwa hai mpaka alipokufa na aliiacha Palestine
 

Attachments

  • IMG_6946.jpeg
    IMG_6946.jpeg
    167.3 KB · Views: 31
Back
Top Bottom