Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Netumbo Nandi-Ndaitwah wa chama tawala cha Swapo nchini Namibia amechaguliwa kuwa Rais, na hivyo kuwa kiongozi wa kwanza mwanamke nchini humo.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC), matokeo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Namibia leo Jumanne Desemba 3, 2024 yameonyesha kuwa Swapo imepata kura 583,300, huku chama kikuu cha upinzani, Independent Patriots for Change (IPC), kikishika nafasi ya pili kwa kura 220, 809.
Kura hizo zimeiwezesha Swapo kupata viti 51 katika Bunge la Kitaifa, na IPC viti 20. Nandi-Ndaitwah mwenye umri wa miaka 72, amekuwa Makamu wa Rais tangu Februari 2024.
Mwaka 2017, alikua Makamu wa Rais wa kwanza mwanamke kupitia Swapo.
Namibia sasa itafuata nyayo za Tanzania kwa kuwa na Rais mwanamke Afrika, huku pia ikiungana na Mexico inayoongozwa na Rais Claudia Sheinbaum.