Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Mgombea Urais anayeongoza nchini Zambia wa Chama cha UPNDP Hichilema, alishashindwa uchaguzi wa Urais mara 5 nchini humo lakini hakukata tamaa, hii anayoongoza sasa ni mara ya 6.
Ni Mwanasiasa aliyeongoza kwa kunyanyaswa na Mamlaka wakisaidiwa na Polisi wa nchini Zambia, Taarifa zinaonyesha kwamba Mwaka 2017 Rais wa Zambia Edgar Lungu alituma vikosi vya Usalama nyumbani kwake kumkamata na kisha kumbambika kesi ya Ugaidi kama zilivyo tawala nyingi za kiafrika. Alikaa gerezani kwa siku 118 hadi pale Wazungu walipoingilia kati, baadaye akafutiwa mashtaka .
Mpaka muda huu anaongoza kwa mbali sana kwenye mbio za Urais wa nchi hiyo , na huenda akatangazwa Rais Mpya wa Zambia muda wowote kuanzia sasa
USITHUBUTU KUJIMWAMBAFAI , MADARAKA NI DHAMANA YA MUDA MFUPI TU, TUTENDE HAKI JAMANI
UPDATES
=========