Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #8,381
HATA MIMI NI MJINGA! Ripoti ya CAG
Bunge letu limeahirisha kujadili ripoti ya CAG hadi mwezi Novemba.
Awali Rais aliagiza Katibu Mkuu Kiongozi kuanza kushughulikia na kuwataka wahusika kujieleza.
Kwa ujinga wangu nilidhani:
1. Mkaguzi hukagua mahesabu katika sehemu husika.
2. Kisha huibua masuala (queries) yanayohitaji maelezo na vielelezo.
3. Wahusika hujibu masuala hayo na vielelezo hutolewa.
4. Mkaguzi akiridhika, hufuta masuala hayo. Asiporidhika, masuala hayo huorodheshwa katika ripoti.
Kwa hiyo kwa ujinga wangu, nilidhani:
A. Ripoti ya CAG inayopelekwa kwa rais na bungeni huwa imewasikiliza wahusika na kupitia vielelezo vyote.
B. Ripoti ilishafika kwa rais kinachohitajika ni utekelezaji wa alichosema CAG na si kijadili wala kuwahoji wahusika wa ubadhilifu.
C. Kazi ya bunge ni kuisoma na kuionya, kuishauri na kuielekeza serikali kwa ujumla katika muktadha wa utawala wa fedha za umma hapa nchini.
D. Bunge lilimpa rais fedha za kutumia. CAG amekagua na kuishtaki serikali ya rais kwa bunge. Bunge linamsimamia rais kabla halijampa fedha nyingine.
E. Si kazi ya bunge kujiingiza katika kufukuzana na panya na mchwa waliokula fedha hizo.
F. Ili rais na serikali waweze kupata fedha nyingine, inabidi awashughulikie mchwa na panya.
Mchwa na panya wakiachwa wanabadilika kuwa nyoka mwenye sumu kali mwaka unaofuata.
Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app