MAJIBU YA KWANINI TUNAKOMALIA UKANDA, UDINI NA UARABU WAO?
Tatizo Mbarawa anasimamia wizara ya miundombinu ambayo siyo swala la Muungano na mambo yanapoharibika inabidi tujiulize kwanini wazenj wanatupora ajira ili wao wajipatie kipato haramu? Tunajua baadhi wamemegewa hisa ya hiyo kampuni siyo bwerere hadi kukubali kujidhalilisha kiasi hiki.
Mlikwisha kukaa chini na kukokotoa ajira za moja kwa moja raia wetu watapoteza baada ya hawa waarabu kuichukua hiyo bandari? Au ni ulafi wenu umewapofua?
Hizi ajira ni kuukana utu wa watu wetu na haki yao ya kujipatia kipato.
Pili, waarabu tuna historia nao. Wao ndiyo walitusomba na kutuuza utumwani kwa hiyo hatuwezi tukaliangalia hili swala kijuujuu tu.
Tatu, bado kuachwa kwenye huu mkataba bandari za Zanzibar ni hoja kwa sababu Mwinyi Sr. alipokuwa Rais aliwauzia waarabu Loliondo mpaka leo hawatoki na wakaazi wa hayo maeneo wameporwa malisho na vyanzo vya maji.
Wakaazi tajwa wamefukarika na hizi sera za wazanzibara kuwawezesha waarabu. Mbona wanapoukwaa urais hatuoni wanawafanyia wazanzibara wenzao hizi dhuluma. Lakini Mwinyi Sr na Kinana tunajua walivuna na wanaendelea kuvuna kwa kuwafukarisha watu wetu.
Hizi ni shukrani za punda ni mateke. Kumalizana na hawa vibaraka wa waarabu inabidi usimamizi wa serikali ya Muungano tuuhamishie kwa Waziri Mkuu ambaye hatateuliwa na Rais bali atajaza fomu na kuomba uwaziri mkuu kama wale wanaogombea ubunge EAC. Ashinde zaidi ya 50% aunde serikali na kutowateua wasiyo wabara kwenye shughuli zote zisizokuwa za Muungano
Historia pia imetufunza watu wetu wakienda uarabuni haki zao za ubinadamu hukiukwa na hata kuvunwa viungo vyao na kutumika kama viraka (spare parts) vya hao waarabu
Hatuwezi kufumbia macho hulka ya waarabu kukiuka viwango vya ajira (Labour standards) na kujipendelea.
Kwanini watupore ajira zetu na huku tuna bandari nyingi ambazo zinahitaji wawekezaji.
Kama mnawapenda sanaaaaaaa wapeni Bwagamoyo, Lindi, Ujiji, Nyasa, Mwanza, Bukoba, Ukerewe,
Why Dar ambayo ni strategic port?
Ukimkamata mwizi leo kweli utamruhusu ajitetee mbona yule mwizi wa jana hujamkamata? Sisi tunashughulika na wewe na hao wengine iko siku yao itafika tu. Hivyo, hoja za ubinafsishaji wa Geita, n.k hazina mashiko. Waliofanya hivyo ni wabara lakini walitudhulumu sasa tukae kimya tunapoona dhuluma zinaendelea kwa utetezi tulidhulumiwa awali au kaeni kimya dawa ituingie maana mbona wabara wenzenu waliwabinya na mlipiga ganzi?
Hatutakaa kimya tukiona maovu yakikithiri. Swala la kugawa raia kwa ukanda latoka wapi? Utudhulumu halafu ujifiche kwenye kichaka cha kuwagawa raia? Anayetugawa si ni wewe ma uchu wako wa mali? Mali zenyewe wala hazikupeleki mbinguni utaziaacha hapahapa tu.
Mkapa alitubinafsisha akajiona yeye ni chuma cha pua lakini sisi tulimtumainia Mwenyezi Mungu na siku yake ilipofika tulimpakia kwenye sanduku lake na tukawakabidhi funza wamalizane naye.
Sijui kwanini mwanadamu unamkubalia shetani akuhadae eti atakutajiriaha kwa kukukosanisha na Muumba? Utabaki salama kweli?
Mbaya kuliko yote hawataiendeleza bandari bali wataikamua na makapi kuturushia.