Profesa maji marefu hebu tujibu hili swali ni nani alikuchagua?
Wewe ni tunda la uwakilishi haramu utamhubiria nani?
Swali ambalo hawa mafisadi kamwe hawatajibu ni kwanini Nyerere alienda UN na kuwahakikishia tuko tayari kujitawala?
Kujitawala kunaanzia kwa watanzania kuzisimamia njia kuu za uchumi na wala siyo vinginevyo. Tuendeshe vizuri au la hilo ni jukumu letu.
Matatizo ya Tanzania ni ya kimfumo tu ambayo yamezalisha uwakilishi haramu ambao siyo chaguo la watanzania na matokeo wamekuwa vibaraka wa wakoloni mamboleo.
Hatuna sababu yoyote ile watanzania wasisimamie njia kuu za uchumi.
Watanzania hatujashindwa ila mfumo kandamizi ndiyo umeshindwa kututoa kwenye hili tope tulilokwama.
Majibu mepesi ya kuwamilikisha wakoloni nchi yetu ni viraka tu ambavyo vitaongeza misuguano kwenye jamii na amani itaota mbawa.
Majibu ya kudumu ni kutambua mfumo uliopo umezalisha viongozi ambao ni dhaifu na hawawajibiki kwa wananchi na hivyo hawawezi kuyajali masilahi ya wananchi bali wameweka ulafi wao mbele.
Kutatua haya matatizo ni kuwarudishia wapigakura haki yao ya kuwachagua viongozi ambao wataweka masilahi yao mbele.
Lakini tukiendelea na huu mfumo wa kukasimu madaraka kwa wezi wa kura tutaishia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Amani haiji kwa ulimi tu bali kwa dhamira inayojionyesha kwenye matendo ya kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa kuwatendea haki wanakondoo wake.
Watanzania tu ndiyo wana majibu ya kero zetu siyo wakoloni wawe na uwekezaji hawana, wawe na tekinolojia au hawana siyo sababu ya kuudhalilisha utu wetu.
Wanaosema TUMESHINDWA wajue ni wao wameshindwa kuboresha mfumo wa uwajibikaji ambao ndiyo umetufikisha hapa waache kulaumu wataalamu ambao ni wao wanasiasa uchwara ndiyo huwateua kukidhi masilahi yao binafsi ambayo hata hayawapeleki popote.
Mwisho wa siku wanakufa na huwa tunajiuliza hizi harakati za pimbi huyu kumbe kweli alikuwa zezeta hata hakujua yeye ni keki nono kuliko zote za funza na mang'onyo?