Kama ni sahihi kwa wenza na familia zao kuwa ni sehemu ya utumishi wa umma ni sababu zipi watumishi wote wa umma kwa kutumia vikokotoo vyao vya mafao hawatendewi sawa na viongozi wa kitaifa?
Mahakama zetu hutetea ubaguzi na dhuluma kwa hiyo hawatakosa la kusema kama waliweza kuita UJIRA siyo sehemu ya mafao ya kustaafu watashindwa kweli kutetea ubaguzi katika utumishi wa sekta ya umma?
Tujuavyo, mahakama ya rufani ilikosea kutofautisha ujira na mafao ya kustaafu ili kuwapora wastaafu wa kawaida haki yao ya kikatiba kulipwa mafao tajwa kabla ya kuhitimu miaka 60 ya kustaafu kwa mujibu wa sheria
Kwa tafsiri hii, mafao ni ujira na unalindwa na katiba siyo kitu cha kufanyia mzaha mzaha kama mahakama ya rufani ilivyofanya ili tu kuwafurahisha watawala na kuwafukarisha wastaafu
Tunarudia bila kuchoka sheria kusudiwa ya mafao ya wenza na familia zao ambazo siyo ofisi ya umma kulingana na sheria ya utumishi wa umma ni uvunjwaji wa katiba
Pia sisi tuendelee kukusanya ushahidi wa kuisambaratisha idara ya mahakama ili iundwe upya na kuwa muhimili wa haki tu badala ya ilivyo sasa ni idara maalumu ya CCM!