New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Sasa kama siyo watumishi wa umma unawalipaje mafao ya kustaafu huku hawalipwi mishahara?
 
Inakuwaje mshahara mmoja uzae lukuki wa mafao ya kustaafu ili yawahusu wenza na watoto wao ambao wengine ni zaidi ya miaka 18?

Kwanini hawatakiwi kujitegemea kama raia wengine?
 
Kama ni sahihi kwa wenza na familia zao kuwa ni sehemu ya utumishi wa umma ni sababu zipi watumishi wote wa umma kwa kutumia vikokotoo vyao vya mafao hawatendewi sawa na viongozi wa kitaifa?
 
Mahakama zetu hutetea ubaguzi na dhuluma kwa hiyo hawatakosa la kusema kama waliweza kuita UJIRA siyo sehemu ya mafao ya kustaafu watashindwa kweli kutetea ubaguzi katika utumishi wa sekta ya umma?
 
Tujuavyo, mahakama ya rufani ilikosea kutofautisha ujira na mafao ya kustaafu ili kuwapora wastaafu wa kawaida haki yao ya kikatiba kulipwa mafao tajwa kabla ya kuhitimu miaka 60 ya kustaafu kwa mujibu wa sheria
 
Tafsiri sahihi ya UJIRA ni mapato yoyote yale yanayomwezesha mwanadamu kumudu gharama za maisha siyo mshahara wa mwajiriwa tu ndiyo UJIRA
 
Kwa tafsiri hii, mafao ni ujira na unalindwa na katiba siyo kitu cha kufanyia mzaha mzaha kama mahakama ya rufani ilivyofanya ili tu kuwafurahisha watawala na kuwafukarisha wastaafu
 
Tunarudia bila kuchoka sheria kusudiwa ya mafao ya wenza na familia zao ambazo siyo ofisi ya umma kulingana na sheria ya utumishi wa umma ni uvunjwaji wa katiba
 
Inabidi wawe wanalipwa mishahara ndipo waweze kulipwa mafao husika siyo kutegemea mshahara wa mwajiriwa ambaye ni ndugu yao nao kudai ulaji.

Sheria zetu zote zinakataza hayo.
 
Swala la kulipwa mafao ya uzeeni la viongozi wa kitaifa liko kikatiba haliwezi kuboreshwa au kutenguliwa na sheria za kawaida
 
Ushauri wetu kwa wanaotaka kwenda mahakamani baada ya hii sheria dhalimu kutungwa
 
Pamoja tunajua misimamo ya mahakama yetu ni kulinda dhuluma bado nendeni
 
Maamuzi ya kimahakama yanayotetea dhuluma tuendelee kuyakusanya ili kesho yatupe sababu za kushinikiza mageuzi ya idara ya mahakama
 
Tutakapokuwa tunaongelea uozo wa idara ya mahakama tuwe na ushahidi wa kutosha
 
Kenya walifanya mageuzi makubwa ya mahakama zao kwa kuongozwa na dhuluma iliyokuwa ikifanyika mahakamani
 
Pia sisi tuendelee kukusanya ushahidi wa kuisambaratisha idara ya mahakama ili iundwe upya na kuwa muhimili wa haki tu badala ya ilivyo sasa ni idara maalumu ya CCM!
 
Back
Top Bottom