New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Wapinzani hujikita kwenye mikutano na kupima mahudhurio yake kama kipimo cha kukubalika
 
Kwa aina ya uongozi ulioko upinzani tusitegeemee la maana zaidi ya makelele na malalamishi tu
 
Ambako kote huko ni kuangukia pua ni vyema wapinzani wakaanza vikao nchi nzima kubuni mikakati ya kulinda kura kwenye chaguzi ili tuachane na uwakilishi haramu ambao ndiyo unazaa sera za hovyo za ubinafsishaji
 
Tutaendelea kesho kuoni mikakati ya wapigakura kulinda kura na kuendelea kuwaelimisha hawa wapinzani-tumbo waache kupoteza nguvu zao na masuala ambayo hawatafanikiwa watumie nguvu zao kwenye eneo ambalo wana sauti nalo ni kulinda kura tu yaani hakuna jinsi
 
Usikose kesho kuona mikakati tuliyoitafakari kwa muda mrefu na hiyo itawashikisha adabu sisiemu na watakuwa wapole kama simba kanyeshewa mvua vile 😃 😀 😄 😁 🤣 😂 😃 😀 😄 😁 🤣 😂
 
Sisiemu kujivua gamba kwa kulivunja baraza la mawaziri!


Inapokuja swala la kuendelea kubaki madarakani sisiemu huwa haina cha msalia mtume na huchukua hatua stahiki kwa kuwamwaga makada wake walioshindwa kusoma alama za wakati.

Ni dhahiri sera ya ubinafsishaji wa taasisi za umma siyo chagua la wananchi wa taifa hili hususani kutokana na mchango wake kiduchu kwenye maeneo yote ambayo yalitaifishwa.

Hakuna hata kiongozi mmoja ndani ya sisiemu yuko tayari kutathmini zoezi zima la ubinafsishaji tangia Mkapa aingie madarakani.

Mfano tu, sekta ya madini tu inazalisha zaidi ya dola za kimarekani bilioni 5 kwa mwaka lakini mchango wake kwenye bajeti ya serikali ni chini ya asilimia moja tu.

Wanaonufaika na sera za uwekezaji ni wachache mno huku wengi tunachoambulia ni mzigo wa kodi kuwaruzuku wawekezaji feki.

Kutokana na hii sera ya hovyo na isiyo ya tija sisiemu haina jinsi ni kujivua gamba kwa kulivunja baraza la mawaziri na kuwatupia virago vyao akina maprofesa uchwara Kitilya Mkumbo, na huyo wa uchukuzi ambao kwa pamoja wamedhihirisha hawana ujuzi wala maarifa ya kusimamia kitu kidogo kama bandari na kuongeza mapato, mitambo kusomana n.k

Waziri Mkuu pia kutemwa kwa kuwadhalilisha watanzania hawana uwezo wa kuzisimamia bandari zao miaka 61 baada ya uhuru.
 
Tunaomba radhi tumeahirisha kwa muda usiyojulikana mikakati tuliyoiahidi ya wapinzani ya kulinda kura
 
Kwanza tunatoa pongezi kwa ujasiri na busara kwa kanisa katoliki kumtanguliza Yesu Kristu Mungu wangu pekee Aliyehai na kuuweka uanadamu wao baadaye na kutoa msimamo wa kiroho
 
Baada ya tamko zito tajwa, hatuoni sababu ya kuendelea na mikakati ya kuing'oa sisiemu madarakani
 
Tunaamini watawala watachukua hatua za kuwaondoa madarakani vibaraka wote wa ukoloni mamboleo
 
Haiwezekani miaka 61 baada ya uhuru tuna viongozi wanajivunia kuwa vibaraka wa ukoloni mamboleo na bado wanaendelea kuwa watumishi wa umma
 
Hii serikali imetukosea adabu ni vyema wakarudisha imani kwetu siyo tu kwa kulitengua Azimio la bunge lililobariki sisi kuwa watumwa wa waarabu wa Dubai kwa madai hatuna uwezo wa hata kuzisimamia bandari zetu
 
Walioshindwa siyo sisi bali watawala kwa kukosa dira, mwamko na utashi wa kuleta mabadiliko yanayohitajika ili watoto wetu waweze kuzisimamia bandari zetu kwa uadilifu
 
Back
Top Bottom