New Force/ Golden Deer acheni uhuni kwa mizigo ya abiria

New Force/ Golden Deer acheni uhuni kwa mizigo ya abiria

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,730
Reaction score
9,088
Ninapenda kutoa huu mkasa kama ifuatavyo. Tarehe 12/1/2023 nimetuma mzigo kutoka DSM kwenda Mbeya kama inavyoonekana kwenye risiti. Nimekabidhi ofisi ya Mbezi imeandikwa Golden Deer na Newforce ipo flow ya pili mwisho kabisa jirani na sehemu ya chakula. Mzigo nilitwgemea tarehe 13 Januari ufike Mbeya tarehe 14 Januari asubuhi aliekwenda kupokea ofisini Mbeya akaambiwa haupo.

New Force receipt.jpg

Kilichofuata ni kuzungushwa na kujibiwa ovyo kutokupokelewa simu, tarehe 15 nikaenda Mbezi nikaambiwa gari zetu yani New Force hazina Matanboy ina dereva wawili mmoja anakua kama Tan boy hivyo wanasahau kushusha mzigo, nikawauliza ni mizigo yote au wangu tuu. Hiyo siku waliupakia niliwaskia wakisema gari ina namba DKB ulikuwemo humo.

New Force one.jpg

Mzigo nikaambiwa umeachwa Makambako, nikajiuliza huu ndio utaratibu wa New Force. Tukazinguana nikaambiwa unarudishwa Dar tena kwa dharau nikajibiwa kama vipi tukulipe tu thamani ya mzigo wako. Wanajisahau mimi nikienda kuuza napata faida wao wanajibu ovyo. Kuna jamaa nilipotoka pale ofisini akanidokeza akaniambia hao jamaa ndio michezo yao ukizubaa huo mzigo hutoupata nenda Polisi. Bahati ninajuana na watu wengi humo njiani.

Mzigo wangu jana 16 Januari ukashushwa Makambako na New force inayotoka Tunduma, leo mchana kuna msamaria mwema pale Makambako kanisaidia kaupakia Super Rojas umefika Mbeya tangu tarehe 12 hadi leo.

Hii kitu imeniuma mimi ni vile najuana na wadau wengi sasa raia wasio na connection si ndio wanadhulumiwa.?

Huyo jamaa hapo Tarimo hajui chochote na ndio nimekabidhi kwake.

MIMI NAWASIHI SIO SALAMA KUTUMIA HIYO OFISI YA NEW FORCE HAPO MBEZI, HAO JAMAA SIO WAAMINIFU. ADMIN HII NI KWA NIA NJEMA KUSAIDIA RAIA.
 
Manzi yangu ashashushiwa begi na kuachiwa ambalo sio lake. Ila honestly Amna gari waaminifu kama kimbinyiko ya njombe Dodoma. Walimfatilia jamaa aloshusha begi adi kwake mafinga aise
Kimbinyiko wapo makini Sana kwenye mizigo na wanakua tayari kulipa thamani ya mzigo kama ukipotea

Pole mkuu
 
Nimeona una sambaza bandiko hili sehem tofauti tofauti kwenye mitandao mingine ya kijamii, sijui lengo ni nini?

Hayo mambo yanatokea sana kwenye sector ya usafirishaji.

Hata kwenye bombadier. Obama akija Kenya kwa mara ya kwanza akiwa senator mizigo yake ilikuwa misplaced pia.

Obama loses luggage on first trip to Kenya

Ije kuwa kwenye mabasi ya bongo?
 
Golden deer sijui New Force ni wababaishaji. Wanajiamini maana biashara ya nyanda za juu kusini wameishika kasoro Songea maana Superfeo anawapelekea moto balaa na G7 yake wana adabu kidogo, ila Mbeya, Tunduma na Sumbawanga jamaa wanaringa sana manina zao..
 
Nimeona una sambaza bandiko hili sehem tofauti tofauti kwenye mitandao mingine ya kijamii, sijui lengo ni nini?

Hayo mambo yanatokea sana kwenye sector ya usafirishaji.
Ana haki ya kutoa dukuduku lake na kuwaonya wengine wachukue tahadhari kabla ya hatari.

Makampuni ya usafirishaji yanatakiwa kuacha ubabaishaji. Scandinavia waliweza nyie mnashindwa nini?

DHL wanawezaje?
 
Wachina wanajidai sana, wanasema nani wa kuwashitaki? Tupeleke kokote tutakushinda
Golden deer sijui New Force ni wababaishaji. Wanajiamini maana biashara ya nyanda za juu kusini wameishika kasoro Songea maana Superfeo anawapelekea moto balaa na G7 yake wana adabu kidogo, ila Mbeya, Tunduma na Sumbawanga jamaa wanaringa sana manina zao..
 
Kuna siku nilisafirisha mzigo uzito wa kg15 una kaupana 90X50 ila nikaambiwa elfu 60 nikaomba sababu hakuna nikawauliza gunia la maindi la kilo 100 tunalipa 30000 itakuwaje haka kamzigo.

Mabasi yana tatizo kwenye wafanyakazi wake sio uongozi wa juu
 
Tatizo limeanzia juu na wafanyakazi wana take advantage.
Scandinavia waliweka jedwali la uzito na gharama ya kusafiria na mzani ulikuwepo pale.

Ukiwa na kilo 10 unakuwa unajua kabisa kiwango wa wewe kulipa
 
Kuna siku nilisafirisha mzigo uzito wa kg15 una kaupana 90X50 ila nikaambiwa elfu 60 nikaomba sababu hakuna nikawauliza gunia la maindi la kilo 100 tunalipa 30000 itakuwaje haka kamzigo.

Mabasi yana tatizo kwenye wafanyakazi wake sio uongozi wa juu
Kuna hii hali ya no morale, no job satisfaction, passengers captivity, motivation poor, extreme exploitation, maringo ya waajiri, frustrations za matajiri, umafia, supervision poor, uongo, yaani vurugu tele, mtanzania anataka close supervision na monitoring kila dakika
 
Back
Top Bottom