New Force/Golden Deer kwanini ajali mnapata nyie tu?

New Force/Golden Deer kwanini ajali mnapata nyie tu?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
1691430708159.jpg

Golden Deer 🦌 imelala chali.

Ndani ya miezi mitatu mna zaidi ya ajali kumi. Achaneni na Sauli hamumuwezi, thaminini uhai, usalama na maisha ya abiria wenu.

Jifunzeni kutoka kwa Scandinavia
1690865282786.jpg

1691430694375.jpg
 
Morogoro. Mtu mmoja amelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito wilayani Mikumi na wengine wametibiwa na kuruhusiwa baada ya basi la kampuni ya New Force walilokuwa wakisafiria kutoka Kyela kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Agosti 7, 2023 jioni eneo la Msimba kwenye mteremko na kona za Iyovi Mikumi ambapo amemtaja majeruhi kuwa ni Elinipenda Kishimbo (26) aliyeteguka mkono.

Kamanda Mkama amemtaja dereva wa basi hilo kuwa ni George Obedi (48) huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva huyo kwa kuwa alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila ya kuchukua tahadhari na hivyo kukutaka na gari jingine uso kwa uso.
 
Back
Top Bottom