New York, Marekani: Rais Samia ashiriki Mkutano kuhusu athari za Mabadiliko ya TabiaNchi

Ni mwaka wa tatu sasa Lisu amekuwa akiwahadaa mazombi wake kuwa atahutubia baraza la usalama na vikao vikubwa kama hivi. Cha kushangaza raisi Samia amefanikiwa kwa muda mchache tu alioingia.
Ni vipi unawalinganisha Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Siasa? Hivi umejitafakari kweli?
 
Unafaida kubwa sn agenda yamsingi inayo enda kuzungumziwa pia ni uharibifu wa hali ya hewa Duniani hilo tu linagusa kila mtu katika huu ulimwengu wa fuju jua hilo kwanza. Ukame wewe huoni, joto ulioni na nk.
Uharibifu mkubwa wa mazingira unafanywa kwa kiasi kikubwa na nchi zilizoendelea, nchi za viwanda. Nchi hizo hasa America zimegoma kabisa kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa na kukataa hata kusaini mkataba wa kimataifa kuhusu mazingira.

Afrika na hasa Tanzania inachangia uchafuzi kwa kiwango gani hadi kutishia uhai wa Dunia? Hii mikutano ipo tangu ulipoanzishwa umoja wa mataifa, Kuna maazimio yapatayo elfu na zaidi yaliyoazimiwa na viongozi watangulizi hayajafanikiwa... Lakini kila mwaka watu wanakutana tu, ndio maana tunasema ni kwenda kuuza sura tu.
 
Kuna uzi humu unasema Lisu atagombea ukatibu mkuu UN

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Sijui iliishia wapi hii ndoto
Kila wanapotengeneza propaganda na kufeli ndo wanavyozidi kupoteza wapiga kura ambao wanagundua uongo wao.
 
Ni vipi unawalinganisha Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Siasa? Hivi umejitafakari kweli?
Kama walijua makamu mwenyekiti wa chama hawezi kuwa na uwezo wa kuhutubia UN na mikutano mikubwa kama hii kulikuwa ni ulazima gani wa kuwadanganya watu kuwa atahutubia leo, kesho mara keshokutwa na kuendelea? Siasa za uongo uongo hivi zikiwachosha wananchi na kuwanyima kura utailaumu tume ya uchaguzi au viongozi wa chama kwa kuendesha mambo kwa njia za kilaghai? Kila mwanasiasa muongo, lkn kama mpinzani unaetafuta kushika madaraka kwa njia ya kura unatakiwa uongo wako ujifiche usionekane. Yani wanachama na wapiga kura wako wasigundue kuwa unafanya siasa zako kwa njia ya kudanganya danganya. Matokeo yake watashindwa kukuamini na kukunyima kura. Kwani wataona ni bora zimwi likujualo ambalo ni chama kilichopo madarakani kwa vile wanakifahamu miaka na miaka.
 
Mama rudi nyumbani huko nikupotezeana pesa zetu

Mabadiliko ya tabia ya Nchi wanazungumuza kila leo hakuna kinachofanyika hasa nchi zilizo endelea!.
 
Kwanini hicho kimini huwa havai hapa nyumbani?
 
Wajameni, haya sasa ndio mambo haya...
Kuna vitu watu tulisema, japo tulibezwa sasa vinatokea na vinajidhihirisha.
Hapa nilisema kitu kuhusu Tanzania ya Samia compared na Tanzania ile. Tunakwenda kuwa na Tanzania nzuri na Tanzania Njema kuliko Tanzania ile.
Hongera sana Mama Samia

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…