New York: Rais Samia akutana na Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres‬

Wawili hao wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo athari za kiuchumi na kijamii za COVID-19, utekelezaji ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) pamoja na Ulinzi na Usalama Barani Afrika

2F77A28C-6621-4592-84E7-21F9B4FEB38D.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Jijini New York Nchini Marekani Septemba 23, 2021.

559B2196-637B-48D4-8843-F2F77B0F225D.jpeg

Rais Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Jijini New York Marekani, mara baada ya kuhutubia mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 23,2021. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres.
 
Wajameni, haya sasa ndio mambo haya...
Kuna vitu watu tulisema, japo tulibezwa sasa vinatokea na vinajidhihirisha.
Hapa nilisema kitu kuhusu Tanzania ya Samia compared na Tanzania ile, kiukweli kabisa, Tanzania tunakwenda kuwa na Tanzania bora, Tanzania njema na Tanzania nzuri kuliko Tanzania ile, kitu kinachohitajika sasa ni kumpa muda.

Hongera sana Mama Samia, una uwezo na unaweza kututoa hapa tulipo na kutufikisha kule tunapaswa kuwa.

P
 
Kipara kisichokuwa na nywele hakitofautiani na kalio

Tupambane
 
Kwahiyo anaonekana hajui kuongoza sababu Mbowe yuko gerezani?Nyuzi nyingi nikisoma hata kama mama kafanya jema watu wanambeza eti kisa Mbowe yuko gerezani.

Sikieni nyie matomaso kama Mbowe hana kosa mtoeni gerezani kwa sheria na kama ana kosa afungwe tu kwani yeye nani akifanya kosa asiwajibishwe
 
Kwahiyo anaonekana hajui kuongoza sababu Mbowe yuko gerezani?Nyuzi nyingi nikisoma hata kama mama kafanya jema watu wanambeza eti kisa Mbowe yuko gerezani.Sikieni nyie matomaso kama Mbowe hana kosa mtoeni gerezani kwa sheria na kama ana kosa afungwe tu kwani yeye nani akifanya kosa asiwajibishwe
Kitendo cha Mbowe kuwa ndani ni ishara kuwa Samia anaongoza vyema. Mungu mbariki Samia Cc Erythrocyte
 
Ningebahatika kuwa kiongozi nchi jii hata kwa mwaka mmoja basi viongozi wa CCM wangejaa mahabusu kwa kesi zisizo na dhamana huku nikiwaambia wasubiri mahakama itawapa haki!

Wakisota kama miaka 2,namwambia DPP hebu achana na nia!
Halafu natulia nasubiri mwana CCM atakayekuwa anaongea sana,namtengeneza kama wenzake!

Nadhani hii mbinu itawanyoosha na kuwakumbusha madaraka yanapita!
 
Ningebahatika kuwa kiongozi nchi jii hata kwa mwaka mmoja basi viongozi wa CCM wangejaa mahabusu kwa kesi zisizo na dhamana huku nikiwaambia wasubiri mahakama itawapa haki!Wakisota kama miaka 2,namwambia DPP hebu achana na nia!
Halafu natulia nasubiri mwana CCM atakayekuwa anaongea sana,namtengeneza kama wenzake!

Nadhani hii mbinu itawanyoosha na kuwakumbusha madaraka yanapita!
Kwahiyo unamaanisha Mbowe ni malaika?
 
Wajameni, haya sasa ndio mambo haya...
Kuna vitu watu tulisema, japo tulibezwa sasa vinatokea na vinajidhihirisha.
Hapa nilisema kitu kuhusu Tanzania ya Samia compared na Tanzania ile, kiukweli kabisa, Tanzania tunakwenda kuwa na Tanzania bora, Tanzania njema na Tanzania nzuri kuliko Tanzania ile, kitu kinachohitajika sasa ni kumpa muda.

Hongera sana Mama Samia, una uwezo na unaweza kututoa hapa tulipo na kutufikisha kule tunapaswa kuwa.

P
Hivi mumewahi kufaidika nini hasaa kwenye hivo vikao? Maana marais wengi tu wameenda huko na wameongea lakini kwanini uone taifa lako hasa ndo litafaidika zaidi? Libya chini ya Gadafi iliendelea sana kwa jitihada zao wenyewe sio kujikombakomba
 
Jana nilichukia sana yaani Rais wetu anaitwa Samia Sululu kipindi anakaribishwa Dah.

"...Our excellence president of Tanzania Samia Sululu..." How is pain our president kuitwa Sululu instead of Suluhu.
 
Kwahiyo anaonekana hajui kuongoza sababu Mbowe yuko gerezani?Nyuzi nyingi nikisoma hata kama mama kafanya jema watu wanambeza eti kisa Mbowe yuko gerezani.Sikieni nyie matomaso kama Mbowe hana kosa mtoeni gerezani kwa sheria na kama ana kosa afungwe tu kwani yeye nani akifanya kosa asiwajibishwe
Tatizo ukiwafanyia jema, wanatamba na kuanza kusema shetani hajawahi mshinda mungu; , ukiwabana wanalalamika ajabu
Wanasheria wasomi wanasubiri mtu wao atoke kwa huruma ya mama,halafu hawa jamaa hamnazo kweli yaani hawana jema
Kitendo cha Mbowe kuwa ndani ni ishara kuwa Samia anaongoza vyema. Mungu mbariki Samia Cc Erythrocyte
Kwahiyo anaonekana hajui kuongoza sababu Mbowe yuko gerezani?Nyuzi nyingi nikisoma hata kama mama kafanya jema watu wanambeza eti kisa Mbowe yuko gerezani.Sikieni nyie matomaso kama Mbowe hana kosa mtoeni gerezani kwa sheria na kama ana kosa afungwe tu kwani yeye nani akifanya kosa asiwajibishwe
Habari inamhusu samia suluhu na guterez, lakini vijana wa uvccm wameshamuingiza <Mbowe
 
Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres‬

Wawili hao wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo athari za kiuchumi na kijamii za COVID-19, utekelezaji ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) pamoja na Ulinzi na Usalama Barani Afrika

View attachment 1950287
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Jijini New York Nchini Marekani Septemba 23, 2021.

View attachment 1950288
Rais Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Jijini New York Marekani, mara baada ya kuhutubia mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 23,2021. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres.
Mama angekuwa anavaa tu kiafrika kama Hellen wa Liberia au Joyce banda wa malawi kama sikosei

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
Mnataka demokrasia gani wakati mnashinda kwenye mitandao mnatukana tu.

Wapi tulipotukana? Wapi tuliposhinda mitandaoni?

IMG_20210924_084215_979.jpg

SSH na hata Msigwa pale NY wanayo habari ya demokrasia tunayoitaka.

Hujui demokrasia tunayoitaka au ni kujitoa ufahamu tu?
 
Back
Top Bottom