New York: Uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour Tanzania - Starring Samia Suluhu Hassan, President of The United Republic of Tanzania

New York: Uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour Tanzania - Starring Samia Suluhu Hassan, President of The United Republic of Tanzania

Mbona pambano la Tyson na Ivanda enzi hizo ni mida hii na Wabongo kibao tulisubiri , Leo tukio la Rais and there is no one!
P
... and there is no one! Hii nchi ni yao wanatosha wao na chama chao. Siku itakapozinduliwa hapa nguo za kijani zitatawala nchi na majigambo kila kona, beberu atakuwa nabii.
 
wana habari wa Kitanzania hawakujipang kwa tukiohili?

mbona kama vile hakuna wanahabari walio abatana na msfara huu?!

Je, hawajui majukumu yao ktk tukio hili?
hajui kama dunia inafuatilia kwa karibu tukio hili kubwa?

jamani eeeh.....changamkeni hii ndio fursa kubwa na adhimu!

Pongezi kwa Rais wetu Mama Saamia kwa Ubunifu wa hali ya juu.
 
Watu wenye "kamba ndefu" mkuu, ndio wenye sauti katika serikali ya leo

Tunauzwa 'right, left and center' tukiona wenyewe, na hatuna la kusema.
Kuna sehemu kuna liboss jinga kweli kweli linajifanya liaminifu linadhibiti halina hata gari linapanda daladala huku linakula kwa mama lishe hovyo Sana linajifanya liaminifu wenzake juu wanaenda kuzila tu bila hata huruma.
Halafu likistaafu masikini litajutia linadhani litazikwa na tuzo.
Unalipa kodi juu wanaenda zila.Then Hakuna hatua zozote zinachukuliwa
 
Rais anazinduaje filamu yake yeye mwenyewe? Kwa nini Will Smith na Chris Rock wasingefanya kazi hiyo? Au hata Obama au Bill Clinton?
 
Hapa ndio hoja ya uzalendo inapoibuka,
yaani mtu uko tayari kukesha kumuangalia Tyson lakini Rais wako...!
P
Mkuu Paskal,usidanganyike na uzalendo katika taifa hili.Trust me hata URUSI akituvamia na kutupiga TZ, bado wa TZ tutamshangilia PUTIN na kufurahia wanajeshi wa SAMIA wanavyopelekewa moto (ambao ni ndugu zetu)
 
Walengwa wa hiyo filamu ni wazungu, sio sisi members wa jf ambao wengi ni watanzania. Labda kama lengo ni kuturungishia. Hivyo sitegemei sisi watanzania wengi kuvutika na hiyo filamu maana sio walengwa wa filamu hiyo. Naona umehamasika na hilo tukio mpaka unadhani na wengi wetu tumehamasika hivyo hivyo. Ila si vibaya maana ww umehamasika utuletee hizo clips kadhaa tuone huo uhondo unaokupagawisha.
Sisi member wa JF tunajulishwa matumizi ya kodi yetu katika mchakato mzima wa kuipata filamu ya Royal Tour
 
Hapa ndio hoja ya uzalendo inapoibuka,
yaani mtu uko tayari kukesha kumuangalia Tyson lakini Rais wako...!
P

Hamna cha uzalendo, maana siku hizi uzalendo umegeuka kuwa ni sehemu ya kujipendekeza kwa watawala ili kupata vyeo. Ni hivi Paskali, watu wanapenda hiyo michezo, lakini hawana hela ya kwenda kutalii. Hata ukijifanya mzalendo na huna hela ya kwenda kutalii ni kazi bure. Isitoshe uzalendo unatoka wapi kwa utawala ulioingia kwa ule uchaguzi wa 2020, au unadhani watu wamesahau madhila ya uchaguzi ule?
 
Mkuu Paskal,usidanganyike na uzalendo katika taifa hili.Trust me hata URUSI akituvamia na kutupiga TZ, bado wa TZ tutamshangilia PUTIN na kufurahia wanajeshi wa SAMIA wanavyopelekewa moto (ambao ni ndugu zetu)
Sidhani hata unaelewa ulichoandika .
Huko Ukraine wanakufa wanajeshi tu?
 
Sijui hii if ya siku hizi imekuwaje?!. Ingekuwa ni ile JF ya enzi zile, saa hizi ungekuta tuna updates zaidi ya members 10!.
Yaani unamaanisha kati ya hao waalikwa zaidi ya 400, hakuna mwana JF yoyote kutu update!.
P
Maisha yanaenda kwa kasi sana kaka, although wanalamba asali hawana muda wa kuwapa wenzao updates!
 
Back
Top Bottom