Neymar arejea Kikosi cha Brazil kwa Kombe la Dunia 2026!

Halafu kwenye historia ya World Cup,hakuna kocha aliyeshinda hilo kombe kwa kuifundisha team ambayo sio ya nchi yake,
Foreign coach has never won FIFA World Cup.
Inashangaza sana kuona mataifa makubwa kisoka wakizidi kuwaamini na kuwapa kazi makocha wa kigeni kufundisha timu zao za Taifa.

Hata kama professionalism imeshima hatamu bado Kila raia anaipenda nchi yake, hivyo hataumia timu anayoifundisha ikichabangwa na timu ya Taifa ya nchi alikotikea.

Imagine England wanakutana fainali na Germany, unafikiri England wakichapika bwana Thomas Tuchel, ataumia kama ambavyo Sam Allardyce angeumia?
 
Neymar ndio Brazil's all time top scorer with 79 Goals,
Pia ni second most capped player nyuma ya Cafu.

So,kwangu ni sahihi kwa Neymar kuitwa team ya taifa coz hata fitness yake yupo vizuri kwa sasa.
 
João Pedro naye alikuwa na msimu mzuri lakini kaachwa, Pedro anaweza kukupa kitu cha tofauti kidogo ikiwa Thiago ameshindwa kukupa uwanjani...Sema hii brazili ninavyoiona mmhh.
 
Brazil ya 2002 iliyochukua kombe la dunia ya kina Ronaldinho, Ronaldinho, Cafu, Roberto Carlis na Ronaldo ilisuasua sana hata kufuzu. Ilifuzu kwa mbinde kombe la dunia 2022 Korea/Japan lakini ikawa bingwa.
 
Kama vipi weka basi hicho kikosi chote cha wachezaji 26 na timu wanazotokea.
 
Neymar ni fundi wa mpira,kuitwa kwake tu si kwa bahati mbaya bali amestahili,kilichobaki ni yeye kuuonyesha ulimwengu kuwa bado yupo kwenye chati na ataisaidia vipi timu yake brazil katika michuano hii. Nimtakie tu kila lenye kheri kwake mwamba Neymar.
 
Hawa Brazil watachapika mapema sana... Acha waendelee kuwaita hawa mabishoo wakina Neymar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…