Neymar Jr amekurupuka kwenda PSG

Neymar Jr amekurupuka kwenda PSG

shamp

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2017
Posts
225
Reaction score
215
BINAFSI sitamsamehe Neymar. Katika umri wa miaka 25, nyakati unazotamani kuona akielekea juu kabisa ya kilele cha ubora duniani, anachagua kuondoka Barcelona na kwenda PSG.

Kwa mchezaji wa aina yake mwenye uwezo kama wake, unatokaje kirahisi katika ligi bora duniani na kuchagua kucheza Ligue 1, ligi namba 5 kwa ubora barani Ulaya?

Tatizo ni nini? Pesa au ni kweli amechoshwa kuwa nyuma ya kivuli cha Lionel Messi? Labda sababu ya kwanza, vijana wa Amerika Kusini mioyo yao haijapishana sana na Waafrika.

Dhiki kali walizokumbana nazo utotoni zilishaichoma mioyo yao na kuiacha ikiwa na hasira kali ya kimaisha. Ilipo pesa, walipo wao.

Hapa kwenye kukimbia kivuli cha Leo Messi, ndiko kunakonipa shaka kidogo. Hapa Neymar anatudanganya, tena uongo mbaya wenye kukera.

Sikatai, kivuli cha Messi kimemficha sana. Ubora wake hauzungumzwi tena. Neymar yule tuliyemsikia akiwa Santos, si huyu wa sasa tuliyenaye hapa Nou Camp.

Chochote atakachofanya kimeshafanya na Messi tayari. Barca wana mfalme mmoja tu, La Pulga pekee. Kwa alipofika Neymar alitakiwa kuondoka Barca.

Lakini kama kweli sababu ni kusaka ufalme wa soka duniani, Neymar alitakiwa kujiuliza mara mbili, ni wapi anaweza kwenda na kutengeneza ufalme wa dunia?

Unakimbiaje kivuli cha Messi kwa kwenda PSG? Dunia ya sasa inaanza vipi kutoa mfalme wa soka katika ligi dhaifu kama ile ya Ligue 1?

Mtazame Zlatan Ibrahimov. Ni mfalme wa PSG. Ni mfalme wa Paris, ni gwiji wa Ligue 1, lakini yuko mbali na hadhi ya wafalme wa dunia. Neymar analijua hili?

Kwa miaka 10 sasa Ligue 1 imeendelea kuwa ligi kubwa ya kawaida duniani. Haisisimui kabisa. Wachezaji bora hudumu kwa msimu kadhaa kisha huamua kusaka malisho sehemu nyingine.

Eden Hazard amepata heshima aliyonayo baada ya kucheza Premier League. N’golo Kante pia. Hivyo hivyo kwa Riyad Mahrez na Didier Drogba.

Mtazame tena Kylian Mbappe? Pamoja na ubora wake, dunia imekuwa na mashaka naye bado. Wengi hawaamini kama ni mkali kama takwimu zinavyosema. Kwanini? Ni takwimu za Ligue 1.

Watu hawaiamini sana ligi ile, ni ngumu sana kuona akiibuka mfalme wa dunia maeneo yale. Neymar asiendelee kutudanganya. Kivuli cha Messi hakiwezi kufutwa kwa nyota anayevaa jezi ya PSG. Ni uongo huu.

Kama kweli Cristiano Ronaldo alimshauri kufikiria mara mbili kabla hajatoka Barcelona, basi CR7 ni mkubwa sana kifikra katika dunia ya soka ya sasa. Tusishangae anavyozidi kufanikiwa.

Ni klabu mbili tu ambazo Neymar angeweza kwenda na kuupata ufalme anaoutaka. Real Madrid na Manchester United. Lakini tayari Madrid wanaye Ronaldo, chaguo sahihi kwake lilikuwa Old Trafford.

Neymar angeweza kusimama na kugombea ufalme wa dunia akiwa na jezi ya Manchester. Pale ndipo mahala anakoweza kushindana na kina Leo Messi na Ronaldo, si PSG.

Ukweli mchungu unaofichwa na Neymar na baba yake ni huu, kinachowakimbiza Barcelona ni pesa tu. Hizi stori za Ufalme ni uongo tu.

Neymar hana shida na mataji tena, hana shida na tuzo ya Ballon d’Or. Shida yake ni pesa tu. Na kwa PSG amekutana na wendawazimu wa biashara, watampatia.

Tayari kuna ofa ya mshahara wa pauni 500,000 kwa wiki. Atapimwa afya katika hospitali ya kifahari kule Qatar, kisha atatambulishwa pale uliposimama mnara wa Paris maarufu kama mnasa wa Eiffel. Maisha yanataka nini tena zaidi?

PSG wanamhitaji Neymar kibiashara. Hawana shida ya miguu yake, wana shida na sura yake. Neymar ndiye mtu pekee duniani atakayeweza kukaa kwenye matangazo ya ndege zao na wakafanya biashara kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
With 25 years old; a contract worth £782,000-a-week for FIVE YEARS is not something you would want to kick into a dust-bin. Hajakurupuka. Dogo keshashinda mataji mengi mno na ni muda sasa wa kuvuta mpunga. Kama ni kukurupuka, labda ni PSG ndo wamekurupuka,
 
Weeeh, uache hiyo hela kisa sifa ya kuwa Baarca??

Sent using Jamii Forums mobile app
mapato ya mchezaji si mshahara tu bali kuna matangazo na mikataba mengine, anaweza akapata mshahara mkubwa PSG lakini mikataba mengine itakuja kwa ligi ile? ngoja tusubiri 2018 wakitoa list ya wachezaji wenye hela tutajua kama zitaongezeka au zitapungua mali zake.
 
With 25 years old; a contract worth £782,000-a-week for FIVE YEARS is not something you would want to kick into a dust-bin. Hajakurupuka. Dogo keshashinda mataji mengi mno na ni muda sasa wa kuvuta mpunga. Kama ni kukurupuka, labda ni PSG ndo wamekurupuka,
Mkuu tuwekee huo mshahara wake kwa fedha ya kitanzania...Ili ieleweke kwa wadau hata wasio penda kandanda..watu wapate uhalisia wa hela ya bwana mdogo neymar.
 
Sidhani kama amekurupuka ila ki uhalisia NEYMAR kuna kitu anacho kitaka

Amesha chukua makombe tayari ambayo kuna baadhi ya wachezaji wanatamani....NEYMAR kwa mafanikio aliyo yapata Barca yana mtosha ikizingatiwa bado ana umri mdogo.....

NEYMAR anacho taka yeye ni kuonekana kisoka angarau hata siku moja na yeye aje kuwa mchezaji bora wa dunia...

CR7 na Mess wana elekea mwishoni sasa, sasa nani ataye weza kuchukua nafasi hizo ni NEYMAR...Uchezaji wa wake akienda PSG ata fanya vizuri sana tofauti akibaki Barcelona..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Keshashinda vikombe vikubwa vya klabu vya spain na ulaya, sasa ni mkwanja tu! Mi naona kafanya kitu sahihi, waliokurupuka ni psg, barcelona wao mkwanja mrefu umeingia! Wakimpata Coutinho kwa 80 sio mbaya!! Sioni liver wakithubutu kukataa mkwanja wa 80mil pounds!
 
Sidhani kama amekurupuka ila ki uhalisia NEYMAR kuna kitu anacho kitaka

Amesha chukua makombe tayari ambayo kuna baadhi ya wachezaji wanatamani....NEYMAR kwa mafanikio aliyo yapata Barca yana mtosha ikizingatiwa bado ana umri mdogo.....

NEYMAR anacho taka yeye ni kuonekana kisoka angarau hata siku moja na yeye aje kuwa mchezaji bora wa dunia...

CR7 na Mess wana elekea mwishoni sasa, sasa nani ataye weza kuchukua nafasi hizo ni NEYMAR...Uchezaji wa wake akienda PSG ata fanya vizuri sana tofauti akibaki Barcelona..

Sent using Jamii Forums mobile app
una mawazo kama yangu!
Ilifika wakati messi angeamua kuondoka barca psg wangetoa crazy money kama mshahara! Hivi mtu kama messi anasubiri nini kuondoka barca??
Neymar kacheza karata zake vizuri sana.
 
BINAFSI sitamsamehe Neymar. Katika umri wa miaka 25, nyakati unazotamani kuona akielekea juu kabisa ya kilele cha ubora duniani, anachagua kuondoka Barcelona na kwenda PSG.

Kwa mchezaji wa aina yake mwenye uwezo kama wake, unatokaje kirahisi katika ligi bora duniani na kuchagua kucheza Ligue 1, ligi namba 5 kwa ubora barani Ulaya?

Tatizo ni nini? Pesa au ni kweli amechoshwa kuwa nyuma ya kivuli cha Lionel Messi? Labda sababu ya kwanza, vijana wa Amerika Kusini mioyo yao haijapishana sana na Waafrika.

Dhiki kali walizokumbana nazo utotoni zilishaichoma mioyo yao na kuiacha ikiwa na hasira kali ya kimaisha. Ilipo pesa, walipo wao.

Hapa kwenye kukimbia kivuli cha Leo Messi, ndiko kunakonipa shaka kidogo. Hapa Neymar anatudanganya, tena uongo mbaya wenye kukera.

Sikatai, kivuli cha Messi kimemficha sana. Ubora wake hauzungumzwi tena. Neymar yule tuliyemsikia akiwa Santos, si huyu wa sasa tuliyenaye hapa Nou Camp.

Chochote atakachofanya kimeshafanya na Messi tayari. Barca wana mfalme mmoja tu, La Pulga pekee. Kwa alipofika Neymar alitakiwa kuondoka Barca.

Lakini kama kweli sababu ni kusaka ufalme wa soka duniani, Neymar alitakiwa kujiuliza mara mbili, ni wapi anaweza kwenda na kutengeneza ufalme wa dunia?

Unakimbiaje kivuli cha Messi kwa kwenda PSG? Dunia ya sasa inaanza vipi kutoa mfalme wa soka katika ligi dhaifu kama ile ya Ligue 1?

Mtazame Zlatan Ibrahimov. Ni mfalme wa PSG. Ni mfalme wa Paris, ni gwiji wa Ligue 1, lakini yuko mbali na hadhi ya wafalme wa dunia. Neymar analijua hili?

Kwa miaka 10 sasa Ligue 1 imeendelea kuwa ligi kubwa ya kawaida duniani. Haisisimui kabisa. Wachezaji bora hudumu kwa msimu kadhaa kisha huamua kusaka malisho sehemu nyingine.

Eden Hazard amepata heshima aliyonayo baada ya kucheza Premier League. N’golo Kante pia. Hivyo hivyo kwa Riyad Mahrez na Didier Drogba.

Mtazame tena Kylian Mbappe? Pamoja na ubora wake, dunia imekuwa na mashaka naye bado. Wengi hawaamini kama ni mkali kama takwimu zinavyosema. Kwanini? Ni takwimu za Ligue 1.

Watu hawaiamini sana ligi ile, ni ngumu sana kuona akiibuka mfalme wa dunia maeneo yale. Neymar asiendelee kutudanganya. Kivuli cha Messi hakiwezi kufutwa kwa nyota anayevaa jezi ya PSG. Ni uongo huu.

Kama kweli Cristiano Ronaldo alimshauri kufikiria mara mbili kabla hajatoka Barcelona, basi CR7 ni mkubwa sana kifikra katika dunia ya soka ya sasa. Tusishangae anavyozidi kufanikiwa.

Ni klabu mbili tu ambazo Neymar angeweza kwenda na kuupata ufalme anaoutaka. Real Madrid na Manchester United. Lakini tayari Madrid wanaye Ronaldo, chaguo sahihi kwake lilikuwa Old Trafford.

Neymar angeweza kusimama na kugombea ufalme wa dunia akiwa na jezi ya Manchester. Pale ndipo mahala anakoweza kushindana na kina Leo Messi na Ronaldo, si PSG.

Ukweli mchungu unaofichwa na Neymar na baba yake ni huu, kinachowakimbiza Barcelona ni pesa tu. Hizi stori za Ufalme ni uongo tu.

Neymar hana shida na mataji tena, hana shida na tuzo ya Ballon d’Or. Shida yake ni pesa tu. Na kwa PSG amekutana na wendawazimu wa biashara, watampatia.

Tayari kuna ofa ya mshahara wa pauni 500,000 kwa wiki. Atapimwa afya katika hospitali ya kifahari kule Qatar, kisha atatambulishwa pale uliposimama mnara wa Paris maarufu kama mnasa wa Eiffel. Maisha yanataka nini tena zaidi?

PSG wanamhitaji Neymar kibiashara. Hawana shida ya miguu yake, wana shida na sura yake. Neymar ndiye mtu pekee duniani atakayeweza kukaa kwenye matangazo ya ndege zao na wakafanya biashara kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawezi kukurupuka ana washauti utitiri plis wanasheria wa hali ya juu unadhani aliamka tu akaropoka??!yule si niyonzima mzee he needs money €876k per week nani atakataa??! Na bado anauza kibiashara...Trophys and achivmnt award wanapenda wazungu wa ulaya tu..Africa na s.america ni pesa tu...Hakuna mtu atakaekuuliza umerudi na uefa ngapi ulaya watakuuliza umerudi na shilingi ngapi??!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BINAFSI sitamsamehe Neymar. Katika umri wa miaka 25, nyakati unazotamani kuona akielekea juu kabisa ya kilele cha ubora duniani, anachagua kuondoka Barcelona na kwenda PSG.

Tayari kuna ofa ya mshahara wa pauni 500,000 kwa wiki. Atapimwa afya katika hospitali ya kifahari kule Qatar, kisha atatambulishwa pale uliposimama mnara wa Paris maarufu kama mnasa wa Eiffel. Maisha yanataka nini tena zaidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungepewa hiyoela wewe ungekataa??
 
Mkuu tuwekee huo mshahara wake kwa fedha ya kitanzania...Ili ieleweke kwa wadau hata wasio penda kandanda..watu wapate uhalisia wa hela ya bwana mdogo neymar.
782,000*3000tsh = 2,346,000,000 tsh (bilioni mbili na milioni mia tatu na 46)

Kwa kifupi ni ela ambayo magufuli aliitoa kwa wizara ya kilimo mwaka jana!! yaani mwaka mzima katoa hiyo alafu kuna chalii anangiza pesa hiyo hiyo kwa wiki!!
 
Mkuu tuwekee huo mshahara wake kwa fedha ya kitanzania...Ili ieleweke kwa wadau hata wasio penda kandanda..watu wapate uhalisia wa hela ya bwana mdogo neymar.
BILLION MBILI na MILION MIA MBILI na THEMANINI na MOJA na Mbili na chenji kadhaa KILA WEEK - awe hajatupia kitu kambani, kutoa pass au kupiga free kick hata moja🙂🙂
 
Back
Top Bottom