Ngano ni nafaka hatari sana

Ngano ni nafaka hatari sana

Tatizo ni maelezo yako kuwa general nso yanaleta taharuki. Si kila mtu anajikita kwenye 2% wakati unahimiza jamii iachane na ngano. Jamii haiwezi kuachana na ngano kwa sababu ya 2%.
Sijasema watu waache kutumia ngano, nimesema ni vyema watumie nafaka mbadala kama mahindi.
 
Mnaokoteza habari mitandaoni, bila kuzisoma vizuri kisha mnakimbilia kuja kuanzisha nyuzi zenye taarifa zisizo sahihi. Acha nikurekebishe.

Si kila mtu ana allergy na gluten, kwa hiyo ngano haiwezi kuwa hatari kwa kila mtu. Itakuwa hatari tu kama mwili wa mtumiaji utakuwa na mzio na component/compound angalau moja iliyopo ndani ya ngano au kitu kingine chochote, mfano sabuni, manukato, n.k.
Sasa wewe ndio umeelezea vizuri
 
Kuna siku tutaambiwa ukivuta sana hewa ya" Oksijeni" mapafu yataoza subirini tu.
 
Mnapoandika kuhusu habari inayohusu watu wengi acheni kuleta taharuki.Andikeni ukweli.Gluten intolerance haimpati kila mtu mtu anayetumia ngano.Ni asilimia ndogo sana wanapatwa na tatizo hili.
Hivyo hivyo kwa karanga.Kuna watu wana allergy na karanga wakila karanga au hata chocolate yenye karanga wanapata matatizo ya kuhema na kuvimba hasa kwenye koo lakini haifanyi karanga kuwa zao la hatari.Kwani walio na tatizo hilo ni asilimia ndogo tu.Kuna watu wanapata matatizo ya kuhema kwa kula machungwa au wengine kusikia tu harufu ya chungwa likimenywa.
 
Pia inaweza athiri ngozi na mtu kutoka mapele ya kuwasha kama mwenye ugonjwa mkali wa ngozi.

Pia inaweza sababisha matatizo kwenye ubongo na kusababisha mtu atembee kama aliyelewa.

Inasemwa kuwa matatizo haya hutokea hadi kwa asilimia 2 ya watu wote.
Ni vyema tukatumia mikate ya mahindi, ulezi nk. Ngano ni hatari sana.
Ulaya wanategemea ngano miaka nenda rudi sijui wakiona hili onyo watafanyaje
 
Mbona mnatuchanyanya?ugali unaleta udumavu wa akili ngano nayo ni hatari kwa afya.
Haya mambo yatachanganya, kuna siku nasikiliza video ya wazee wa tiba mbadara wa Canada. Si tunaambiwa kuwa red meat ni hatari, wao wanakwambia kutokula red meat ni hatari zaidi maana ina manufaa kwa mwili ndio maana wanyama wanakula redmeat.
Pia kuna mmoja akaongeza shida ni kwamba watu hasa huko mbele wanakaula nyama bila kula vitu vya ndani kama matumbo, n.k.
 
Soma hapa.
Soma conclusion:
Inasemwa kuwa matatizo haya hutokea hadi kwa asilimia 2 ya watu wote.
Ni vyema tukatumia mikate ya mahindi, ulezi nk. Ngano ni hatari sana.
 
Ulaya wanategemea ngano miaka nenda rudi sijui wakiona hili onyo watafanyaje
Suala la gluten kuwa hatari lipo tu muda lakini halijawa big deal. Lakini kuhusu hatari ya gluten lipo tu. Kuna watu wana alergy na gluten hawali kabisa chakula chenye ngano. Hata mimi ninaye rafiki hapa tanzania akila kitu chenye ngano hilo balaa lake anaumwa. Na limeanzs kama miaka 3 iliopita.
 
Ngano ni nafaka hatari sana na watz wengi hatufahamu. Tofauti na nafaka zingine kama mahindi, ulezi, mtama na mchele, ngano ina aina fulani ya protin inayoitwa Gluten. Protin hii ndiyo hufanya ngano ikikandwa iwe kama banzoka wakati ukikanda unga wa mahindi hauwi namna ile.

Sasa hii protin inaweza kusababisha mzio(allergy/autoimmune reaction) ya hatari sana. Kifupi inaweza sababisha mwili ujishambulie. Maeneo yanayoathirika zaidi ni utumbo mdogo. Hili linaweza sababisha kuharisha bila kukoma, tumbo kujaa gesi, udumavu na afya dhaifu.

Pia inaweza athiri ngozi na mtu kutoka mapele ya kuwasha kama mwenye ugonjwa mkali wa ngozi.

Pia inaweza sababisha matatizo kwenye ubongo na kusababisha mtu atembee kama aliyelewa.

Inasemwa kuwa matatizo haya hutokea hadi kwa asilimia 2 ya watu wote.
Ni vyema tukatumia mikate ya mahindi, ulezi nk. Ngano ni hatari sana.


Mikate ya mahindi ipoje??, juu ya yote unga wa sembe siku hizi unatiwa virutubisho (fortification chemicals), sina hakika kama hizo fortifications zina usalama gani!!.
 
Back
Top Bottom