Ngao ya Jamii, Tanzania: Simba SC na Yanga SC, nani kuibuka mshindi?

Ila sio siri nyuzi za sports hasa mpira wa Tanzania zipo low sana, hazina uchambuzi, hakuna cha kujifunza ni watu kuropoka tu.
Badala ya kufanya analysis ambazo ni tactical mtu anasema tu Yanga itashinda au Simba itashinda. Hebu pitieni ESPN muone watu wanavyoanalyze football.
 
Kwa taarifa yako mimi ni mwanachama hai wa Simba Sports Club.
Nilikuwa namwuliza kitu huyo aliyetabiri matokeo.
Alijichanganya ktk maelezo yake.

Wewe ndiyo umejichanganya alisema kati yao hao aliowataja ndiyo watafunga sasa ukuelewa nini?
 
Kwa beki ile ya yanga hofu itoke wapi? Mechi za majaribio iliyocheza yanga zenye uzito ni mbili tu,tena Sgd united waliwafichia udhaifu kwa kuwazawadia goli 2. Kikosi chenu hakieleweki,kipindi cha kwanza kikosi tofauti na kipindi cha pili. Wapi pumzi ya kumfukuzia mnyama. Nisiongee mengi nyie labda mcheze tu na refa ndiyo kiki iliyobakia.
 
Simba lazima wawe na hofu.

Wakifungwa tu wataanza kung'oa viti kama kawaida.

This time around hakuna Malinzi (Yanga). Kuna Karia na Wambura (Simba). Sasa wakifungwa hamna kisingizio cha Malinzi.

Yanga inaweza kufungwa na maisha yakaendelea hadi kutwaa ubingwa. Simba ikifungwa litatokea balaa kubwa. Tayari kuna watu hawamtaki kocha. Kisingizio kingine ready made.

Kwa Yanga pamoja na pressure ya mtani wa jadi bado ni mechi kama mechi nyingine. Wanaweza kupoteza na kushinda nyingine kumi mfulilizo. Kwa Simba bora washinde hii hata wakipoteza kadhaa katika kumi zijazo.
 
hah hah kwani malinzi ndiye aliyekuwa akivunja viti?
Refa anachezesha mpira wa Simba Vs Yanga.
Ajibuba afunga goli halari kabisa,
Refa analikataa. (washabiki wa Simba sc wanamvumilia)
Tambwe anaifunga Simba goli la haramu la mkono.
Refa analikubali (mashabiki wa Simba wanavumilia)
Refa anaamua kuumpa mkude kadi nyekundu na kumtoa nje ya uwanja bila kosa lolote.
(hapo mashabiki wanashindwa kuvumilia)
Wanakasirika na kuanza kuvunja viti.
Kuna baadhi ya waliokuwa wafadhiri wa Yanga na viongozi wa TFF walikuwa wanahakikisha Simba inahujumiwa kila mechi na Yanga inashinda kila mechi. Kumbuka mechi ya FA kati ya Yanga na Costal Union uwanja wa Mkwakwani mwaka 2015.
Mimi nakuambia ingekuwa Yanga ndio wamefanyiwa hayo mambo, ule uwanja ungekuwa majivu siku ile.
Kumbuka ile mechi na Azamu Refa alimpa kadi nyekundu ya halari mchezaji wa Yanga na Wachezaji waliamua kuchapa makonde Refa.
Au kumbuka mechi ya Fainari ya Kombe la Afrika mashariki nimeusahau mwaka kama 2010 vile, Yanga ililala goli moja na URA ya uganda.
Uwanja wa Taifa lile vurugu lake lilikuwa kubwa sana ndani na nje ya uwanja, mageti yalivunjwa na ilibidi FFU waingilie kati, ilikuwa kama vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Mashabiki wa Yanga wana hasira na fujo kuliko wa Simba.
 

Mkuu utaratibu Wa tiketi za mpira wa kesho ikoje Niko njiani narudi Dar
 

Mkuu utaratibu Wa tiketi za mpira wa kesho ikoje Niko njiani narudi Dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…