Ngao ya Jamii, Tanzania: Simba SC na Yanga SC, nani kuibuka mshindi?

Ngao ya Jamii, Tanzania: Simba SC na Yanga SC, nani kuibuka mshindi?

Mechi ya ngao ya Jamii, itachezwa jumatano tarehe 23/08/2017 na hii ni kuonyesha ufunguzi mpya wa Ligi kuu ya Vodacom ambayo itaanza mwishoni mwa wiki.

Kila mtu anaipenda timu flani kati ya Simba SC na Yanga SC, na siku hiyo ni lazima mshindi apatikane hata kwa penati.

Nani kuibuka mbabe? Simba SC au Yanga SC.

Mandla.
Ila sio siri nyuzi za sports hasa mpira wa Tanzania zipo low sana, hazina uchambuzi, hakuna cha kujifunza ni watu kuropoka tu.
Badala ya kufanya analysis ambazo ni tactical mtu anasema tu Yanga itashinda au Simba itashinda. Hebu pitieni ESPN muone watu wanavyoanalyze football.
 
Kwa taarifa yako mimi ni mwanachama hai wa Simba Sports Club.
Nilikuwa namwuliza kitu huyo aliyetabiri matokeo.
Alijichanganya ktk maelezo yake.

Wewe ndiyo umejichanganya alisema kati yao hao aliowataja ndiyo watafunga sasa ukuelewa nini?
 
Kwa beki ile ya yanga hofu itoke wapi? Mechi za majaribio iliyocheza yanga zenye uzito ni mbili tu,tena Sgd united waliwafichia udhaifu kwa kuwazawadia goli 2. Kikosi chenu hakieleweki,kipindi cha kwanza kikosi tofauti na kipindi cha pili. Wapi pumzi ya kumfukuzia mnyama. Nisiongee mengi nyie labda mcheze tu na refa ndiyo kiki iliyobakia.
 
Simba lazima wawe na hofu.

Wakifungwa tu wataanza kung'oa viti kama kawaida.

This time around hakuna Malinzi (Yanga). Kuna Karia na Wambura (Simba). Sasa wakifungwa hamna kisingizio cha Malinzi.

Yanga inaweza kufungwa na maisha yakaendelea hadi kutwaa ubingwa. Simba ikifungwa litatokea balaa kubwa. Tayari kuna watu hawamtaki kocha. Kisingizio kingine ready made.

Kwa Yanga pamoja na pressure ya mtani wa jadi bado ni mechi kama mechi nyingine. Wanaweza kupoteza na kushinda nyingine kumi mfulilizo. Kwa Simba bora washinde hii hata wakipoteza kadhaa katika kumi zijazo.
 
hah hah kwani malinzi ndiye aliyekuwa akivunja viti?
Refa anachezesha mpira wa Simba Vs Yanga.
Ajibuba afunga goli halari kabisa,
Refa analikataa. (washabiki wa Simba sc wanamvumilia)
Tambwe anaifunga Simba goli la haramu la mkono.
Refa analikubali (mashabiki wa Simba wanavumilia)
Refa anaamua kuumpa mkude kadi nyekundu na kumtoa nje ya uwanja bila kosa lolote.
(hapo mashabiki wanashindwa kuvumilia)
Wanakasirika na kuanza kuvunja viti.
Kuna baadhi ya waliokuwa wafadhiri wa Yanga na viongozi wa TFF walikuwa wanahakikisha Simba inahujumiwa kila mechi na Yanga inashinda kila mechi. Kumbuka mechi ya FA kati ya Yanga na Costal Union uwanja wa Mkwakwani mwaka 2015.
Mimi nakuambia ingekuwa Yanga ndio wamefanyiwa hayo mambo, ule uwanja ungekuwa majivu siku ile.
Kumbuka ile mechi na Azamu Refa alimpa kadi nyekundu ya halari mchezaji wa Yanga na Wachezaji waliamua kuchapa makonde Refa.
Au kumbuka mechi ya Fainari ya Kombe la Afrika mashariki nimeusahau mwaka kama 2010 vile, Yanga ililala goli moja na URA ya uganda.
Uwanja wa Taifa lile vurugu lake lilikuwa kubwa sana ndani na nje ya uwanja, mageti yalivunjwa na ilibidi FFU waingilie kati, ilikuwa kama vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Mashabiki wa Yanga wana hasira na fujo kuliko wa Simba.
 
149c770bdc4989cbf47c341240b4453a.jpg

Achana na machines hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli ni mashine hizo. Ila wote hao wanini.? Kwa mashindano gani tuliyonayo mpaka uwe nao wote hao. Huo ni uoga wa maisha
 
Baasa ya kutabiri kwa usahihi mechi ya pili ya Simba na Yangaa kwa mara nyingine tena ninatoa utabiri wangu wa mechi ya jumatano.

Katika mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Yanga itafugwa goli 2 bila majibu. Na goli hizo zitafugwa na kati ya Emanuel Anold Okwi,John Boko na Shiza Ramadhani Kichuya. Kama ikitokea Kichuya akafunga,magoli yake yatakuwa yale yale ya ajabu ajabu aliyowafunga Yanga mechi mbili zilizopita. Nazungumzia yale magoli ya kisayansi.

Mkuu utaratibu Wa tiketi za mpira wa kesho ikoje Niko njiani narudi Dar
 
Baasa ya kutabiri kwa usahihi mechi ya pili ya Simba na Yangaa kwa mara nyingine tena ninatoa utabiri wangu wa mechi ya jumatano.

Katika mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Yanga itafugwa goli 2 bila majibu. Na goli hizo zitafugwa na kati ya Emanuel Anold Okwi,John Boko na Shiza Ramadhani Kichuya. Kama ikitokea Kichuya akafunga,magoli yake yatakuwa yale yale ya ajabu ajabu aliyowafunga Yanga mechi mbili zilizopita. Nazungumzia yale magoli ya kisayansi.

Mkuu utaratibu Wa tiketi za mpira wa kesho ikoje Niko njiani narudi Dar
 
Back
Top Bottom